Quantcast
Channel: Francis Godwin ::Mzee wa matukio daima::
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2596

WAZIRI KAGASHEKI ASEMA RUSHWA NI CHANZO CHA MAKONTENA YA PEMBE ZA NDUVU KUVUSHWA BANDARINI

$
0
0
Waziri Kagasheki 
Ofisa Uhusiano wa Tanapa Paschal Shelutete akieleza malengo ya warsha hiyo kwa  washiriki wa warsha ya  wahariri  wa vyombo  vya habari nchini leo katika  ukumbi wa Siasa ni Kilimo 
Mkuu  wa  wilaya ya  Iringa Dr Leticia  Warioba kulia akiwa na wanahabari pamoja na washiriki wa warsha hiyo  leo
Majaji wa  tuzo ya Tanapa  wakiongozwa na mwanahabari nguli nchini Tanzania Bw Ayub Rioba  kulia


 MBALI  ya serikali kuendelea  kuchukua hatua  ya kupunguza kasi ya tembo kuuwawa kutoka  tembo 55,000 kwa  miaka  ya sitini hadi tembo 110,000 kwa mwaka 2009,waziri  wa maliasili na utalii balozi Khamis Kagasheki amevishukia vyombo la ulinzi katika  bandari  kuu ya Dar es Salaam kuwa inatisha kwa  rushwa  .

Waziri Kagasheki  ametoa kauli  hiyo leokatika ukumbi wa Siasa ni Kilimo mjini Iringa  wakati akifungua warsha  ya  siku  tatu iliyoanza jana  kwa  wahariri   wa vyombo vya  habari Tanzania .

Alisema  kuwa inashangaza kuona  kontena na meno ya tembo linakamatwa nchi  ya  Tanzania  kwa  kupitia bandari ya Dar es Salaam bandari ambayo kimsingi idara  zote za ulinzi zinapatikana katika bandari hiyo .

“Tunalilitetea vipi kontena la meno ya Tembo….huku  tukiambiwa na  wakamataji   kuwa orijino  yake ni bandari ya Dar e s Salaam bandari ambayo imetawaliwa na polisi , TRA na  watu wa usalama wa kada mbali mbali sasa  limepitaje  nasema rushwa ndio inayoendelea kumaliza  hifadhi zetu Tanzania hivyo tusaidiane ili vizazi vijavyo visituhukumu kwa yale tunayotenda” alisema  waziri Kagasheki

“Lazima tuwe na majibu kwanini, tusaidieni, kupunguza ujangili unaosababishwa na mambo mbalimbali, rushwa ndani ya Mahakam, serikali na polisi wamechangia  kupungua kwa tembo”

Hata  hivyo alisema  kuwa mchango mkubwa uko miongoni wanahabari wakiwemo  wanahabari pamoja na wahariri  wa  vyombo  vya habari katika kusaidia kupiga vita  vitendo vya ujangili ikiwa ni pamoja na kukemea  rushwa, maadili  pia tama za watu wamefika mahali wanataka kufanya lolote lile ili kutimiza  matakwa  yao.
Waziri Kagasheki  alisema  kuwa kwa kawaida watalii huvitiwa sana kumuona tembo japo  tafiti zinaonesha kuwa ujangili na uharibifu wa mazingira umechangia kupungua kwa tembo katika  hifadhi  zetu .

Alisema  kuwa  mwaka 1930 Tanzania  kulikuwa na tembo milioni 50  wakati kwa  sasa  kuna tembo 402,067 tu hali ambayo  inaonyesha  ni kwa kiasi gani tembo wamepungua.

“Wahariri jaribu kutafakari hilo tuendako si kuzuri  Tanzania ni nchi ya pili Botwasan ina tembo 154, 658  wakati  Tanzania tunapoteza tembo wetu idadi imepungua kutoka 250,000 na 300,000 katika miaka ya sitini hadi 55,000 katika miaka ya 1980”

Alisema kuwa baada ya serikali kuchukua hatua sasa  tembo 130,00 mwaka 20002 na mwaka 2006 tembo 141,000 wakati takwimu zinaonyesha kwa mwaka  2009 imepungua  hadi 110,000 kwa mujibu wa takwimu za ujangili .


“Mnatakiwa kuepuka  vitu hivi tunajua kuna risks, lazima wawepo watu wa kujitolea wenye uzalendo na uchungu wa taifa lao…. Vyombo vya habari vinaweza kuifanya kazi hiyo”

Alisema  kuwa ujangili  huo  sit u  kwamba unahatarisha kupotea kwa tembo, lakini unaathiri utalii kwa ujumla wake hali  hiyo  inaashiria kutokuwepo kwa amani hifadhinina  uchumi wa  nchi kwa ujumla.

 Hakuna jinsi huko tunakokwenda, ujangili unaathiri kwa kiasi kikubwa utalii na pato la taifa asilimia 17.

“Hivi  sasa West africa hakuna tena wanyama, ivory coast ilikuwa kinara wa kusafirsiha tembo, leo hawana kitu tusione haya muda umekwenda kama tunataka kuzungumzia maslai ya nchini tusemezane ukweli”

Alisema  kuwa ili kukabiliana na mtandao mkubwa ujangili wa ndani ya nchi unaotumia silaha za kisasa ni lazima kujizatiti na njama hizo zinazotishia kupotea kwa tembo katika uso wa dunia,

Kwani litakuwa jambo la kusikitisha vizazi vijavyo vikianza kusimuliana kwamba kulikuwa na wanyama wakubwa wanaitwa tembo iwapo wadau kwa pamoja  kwa  sasa hatutaungana kupambana na  wahujumu  hao  wa  hifadhi  zetu .

“Vyombo vya habari vina wajibu wa kuhakikisha ujangili unaondoka, msaada wenu ni muhimu, onesheni kwa vitendo, to focus kwenye issue ili mamlaka zinazohusika zichukue hatua”

Hata  hivyo  alisema  kuwa Serikali ipo tayari kupokea maoni ya  wanahabari  katika shughuli hii ya uhifadhi ikiwa ni pamoja na  yeye kama  waziri  kujiwekea utaratibu  wa kukutana na  vyombo vya habari mara moja kila mwezi ili kutoa taarifa zaidi zinazohusiana na mikakati hiyo na masuala mengine yanayohusu wizara.

Kwa  upande  wake mwenyekiti kamati bunge  ardhi mazingira na maliasili James Limbeli alisema  kuwa ni vema mwandishi wa habari akafa kwa kutetea taaluma yako, mambo ya msingi yenye tija kwa nchi. Kwa Tanzania kwa kuwafichua wanaoua  tembo ambao ni laslimali ya Taifa .


“Wanaendesha biashara ya ujangili wanapesa, na inahusisha pia viongozi. …Wahariri zipeni nafasi stori zinazohusu ujangili zisomeni kwa macho mawili”

Hata  hivyo  alisema takwimu ya ujangili  dhidi ya  tembo zilizotolewa na  waziri Kagasheki kwa  upande wake haziamini  kwa sababu wanaoziandaa ni watumishi wa serikali na wanafanya hivyo kulinda hadhi ya serikali.

“Takwimu ni za wale wa hifadhi, katika maeneo nje ya hifadhi hali ni mbaya zaidi  hakuna bajeti, watumishi wachache na hakuna motisha kwa wale  wachache  hivyo  wanaandaa takwimu bora mradi ili  kumfurahisha waziri japo sina shaka na utendaji kazi mzuri  wa waziri Kagasheki ”.
                            
Alisema  kuwa  taarifa  za kuuwawa  kwa tembo ambazo  waziri Kagasheki anazo ni zile zinazoandaliwa na  wahifadhi ambao hata hivyo  wanaziandaa ndani ya  hifadhi  ila  wameacha nje ya  hifadhi na  kuwa idadi ya  tembo kuuwawa ni kubwa  zaidi ya ile ambayo  serikali inayo.

Hata  hivyo  Lembeli  aliwataka  wahariri kuwa na  forum yao ya  big five, ili kusaidia suala la utalii  ambayo ni sekta pekee inayoweza kulinusuru  taifa kiuchumi

“Nawaombeni  sana tusikubali ujangili kuendelea  kupukutisha  hifadhi zetu …... Serengeti inaingiza zaidi ya sh bilioni 30 kila mwaka sasa  iwapo  tutaacha  iteketezwe na majangili  fedha  hizi tutazipata  wapi”

Awali waziri  kivuli  wa maliasili na utalii mchungaji Peter Msigwa alishauri kuwepo kwa  umuhimu wa kutunza rasilimali hizo kwa kuhubiri uadilifu.

Pia  alisema  kuwa  warsha kama  hizo ni nzuri  iwapo  zitahusisha  wadau  wote  wanaozunguka  hifadhi  hizo kama  sehemu ya kuweka nguvu ya pamoja katika  kuzilinda.

Mchungaji Msigwa alisema  kuwa  kinachochangia ujangili ni kutona na watu kukosa uzalendo kwani hivi  sasa  sehemu kubwa ya  watu waliopewa kusimamia sheria hawajui  chochote .

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2596

Trending Articles