Na Gerson Msigwa TBC1 Uganda Timu ya Netiboli ya Bunge la Tanzania imefanikiwa kuibuka mabingwa kwa mara ya pili mfurulizo katika michuano ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyofanyika Jijini Kampala nchini Uganda kuanzia Desemba 07,2013 mwaka huu Fainali za michuano hii zimefanyika katika uwanja wa Mandela Namboole jijini Kampala Uganda Bunge Tanzania imenyakua ubingwa huo baada ya kuichalaza timu ya wenyeji Bunge la Uganda kwa Jumla ya Mabao 35-32, na hivyo kutetea kombe lake ililoshinda kuanzia mwaka jana. Mshindi wa tatu timu ya Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki imefanikiwa kuchukua nafasi ya tatu baada ya kuichapa timu ya Bunge la Kenya. Katika Soka timu ya Bunge la Uganda imefanikiwa kutetea ubingwa wake kwa mara ya tatu mfurulizo baada ya kuichapa timu ya jumuiya ya Afrika Mashariki 3-0, mshindi wa tatu katika Soka ni timu ya Bunge la Kenya iliyoichapa timu ya Bunge la Rwanda 2-1 Rais wa Uganda Yoeri Kaguta Museven alikua mgeni rasmi katika fainali za mashindano haya ambapo amesema anafurahishwa na jinsi mashindano yanavyowaleta wana Afrika Mashariki pamoja na kwamba mshindi wa mashindano haya ni Afrika Mashariki. Museven pia amesema anawapongeza wote huku akisema nchi zote ni watoto wake. |