Quantcast
Channel: Francis Godwin ::Mzee wa matukio daima::
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2596

MBUNGE LUKUVI AKABIDHI GARI LA WAGONJWA NA PIKIPIKI TARAFA YA PAWAGA ,AMPONGEZA RAIS KIKWETE NA DR MWINYI

$
0
0



 Mbunge  wa  jimbo la Isimani ambae ni  waziri  wa nchi  ofisi  ya  waziri mkuu  sera na uratibu wa bunge Bw Wiliam Lukuvi kulia akimkabidhi msaada wa gari  la  wagonjwa mganga mkuu wa wilaya ya Iringa Dr Ignesa Mlowe kwa ajili ya  kituo  cha afya Kimande gari lenye  thamani ya Tsh milioni 180 lililotolewa na serikali kupitia wizara  ya afya na ustawi  wa jamii
  Mbunge  wa  jimbo la Isimani ambae ni  waziri  wa nchi  ofisi  ya  waziri mkuu  sera na uratibu wa bunge Bw Wiliam Lukuvi akimkabidhi  msaada  wa fedha kiasi cha Tsh milioni 2.2 kwa ajili ya kusafisha mfereji wa umwagiliaji anayepokea  kulia ni mwenyekiti  wa jumuiya ya  wakulima wea mpunga katika mfereji wa Mlenge Bw Fundi Maleva leo
...............................................................................................................................................................
MBUNGE  wa jimbo la  Isimani  mkoani  Iringa  Wiliama  Lukuvi amekabidhi  gari  la  wagonjwa  lenye  thamani  ya  zaidi  ya Tsh milioni 180 kwa  kituo cha afya  Kimande Pawaga  na   kumwondoa  aliyekuwa  dereva wa gari la awali ambaye alituhumiwa  kupakia meno  ya  tembo katika gari la  wangonjwa.

Hata  hivyo  alisema  kuwa hakuna mwenye  uhakika  na  tuhuma za dereva  huyo  kujihusisha na kitendo  cha kubeba  meno ya  tembo kupitia gari la  wagonjwa kama ambavyo moja kati ya magazeti  hapa nchini  yalipata  kutoa  tuhuma  hizo kwa  dereva  huyo.

"Nimeamua  kutumia busara  zaidi  kumwondoa dereva aliyekuwa akiendesha  gari hilo la  wagonjwa na  kumweka mwingine   kutokana na upotoshwaji uliofanywa na moja kati ya magazeti kwa  kuandika kuwa  dereva   huyo anabeba meno ya tembo katika gari hilo ....japo  tambueni  kuwa sifa  mbaya  si kwa dereva ni kwa wananchi  wote wa tarafa ya pawaga ila tumemleta  dereva mwingine"

Huku  akimpongeza Rais  Jakaya  Kikwete  kwa  kutekeleza ahadi  yake  ya pikipiki na ujenzi  wa majengo  ya   jumuiya  ya  watumiaji maji pamoja na kutoka  usafiri  wa  pikipiki  wa viongozi wa  jumuiya  hiyo.Akizungumza  leo  na wananchi  wa  tarafa  ya

 Mbunge  wa  jimbo la Isimani ambae ni  waziri  wa nchi  ofisi  ya  waziri mkuu  sera na uratibu wa bunge Bw Wiliam Lukuvi akijaribu  pikipiki mbili zilizotolewa na rais Dr Jakaya  kikwete kwa jumuiya ya  watumiaji maji Pawaga .
.........................................................................................................................................................
Pawaga baada ya  kukabidhi  msaada wa  gari  hilo la wagonjwa ambalo  limetolewa na wizara  ya afya  , Lukuvi  alisema  kuwa magari kama  hayo  yametolewa katika maeneo  mbali mbali  ya  nchi na katika  mkoa  wa  Iringa ni  gari  moja  pekee ndilo  limetolewa kwa wananchi  wa Pawaga.

Hata  hivyo  alisema  kuwa anampongeza waziri wa afya na ustawi  wa  jamii Dr Husein Mwinyi ambae  alifika katika  eneo  hilo akiwa  naibu  waziri  wa afya na kuahidi  kutatua  kero ya  vifo  vya  wanawake  wajawazito ambavyo  vilikuwa  vikitokea kutokana na eneo  hilo  kukosa  gari la  wagonjwa .

Kuhusu  huduma ya  maji katika  eneo  la Mlenge  alisema  kuwa kiasi cha  Tsh  bilioni  2 zinahitajika kwa  ajili ya  wananchi  wa  eneo  hilo la Mlenge ambao kwa  sasa hawanahuduma  ya  maji.

Alisema  jumuiya ya  watumiaji  maji  ya Pawaga  inayonafasi  ya  kutumia  vema mradi  huo wa maji  ili ikiwezekano  kuwezesha  wananchi  wa jirani na kijiji  hicho  kuweza kupata  huduma ya maji na kuwa wasisite  kuwachukulia  hatua  wafugaji  jamii ya kimasai na  wasukuma ambao  wameendelea  kuhujumu  miundo mbinu ya maji kwa  kukata mabomba ya  maji.

Lukuvi  ambae ni  waziri  wa nchi  ofisi ya  waziri mkuu sera na uratibu  wa  bunge  alisema  kuwa  ndoto  yake  ya maendeleo katika  jimbo  hilo hasa  pawaga ni kuona wananchi  wa eneo hilo  wanaunganishwa na barabara ya uhakika na  badala ya  kwenda  mjini Iringa  kupata  usafiri  sasa  wakatengenezewa  barabara  itakayounganisha  eneo hilo na barabara ya Iringa- Dodoma.

Alisema  kuwa  zipo  fedha  ambazo  zimetolewa na ofisi ya  waziri mkuu kwa ajili ya  kuwa na barabara  za mfano  kwa ajili ya  kuinua uchumi  wa  wananchi wa Halmashauri   ya wilaya ya  Iringa  ambapo katika mradi  huo  watahakikisha  wanajenga  ghara  la kuhifadhia  mazao  ya  wakulima hasa zao la mpunga.

Lukuvi  alisema  kuwa  timu  ya  wataalam  itafika  katika  eneo la Pawaga   ili  kutoa  elimu  kwa  wakulima  wa  mpunga  ili  kuboresha  zaidi  kilimo na soko la mchele  wao kupitia  mradi  huo ambao umetengewa  fedha  na ofisi  ya  waziri  mkuu.

Wakati  huo  huo Lukuvi  amekabidhi  msaada  wa Tsh  milioni 2.2  kwa  wakulima wanaotumia  mfereji wa  umwagiliaji  wa Mlenge  ili   mtambo wa  kusafisha  mfereji huo  baada  ya  kuombwa na wananchi hao  wa tarafa ya pawaga

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2596

Trending Articles