Bw James Lembeli
Mwenyekiti kamati bunge ardhi mazingira na maliasili James Lembeli amesema pamoja na jitihada mbali mbali zinazofanywa na TANAPA kwa kuelekeza nguvu ya kutangaza utalii wa mikoa ya kusini ila bado Hoteli nyingi za mkoa wa Iringa gharama yake ni kubwa huku huduma ni mbaya.

Limbeli ameyasema hayo mapema leo katika warsha ya wahariri wa vyombo vya habari inayoendelea katika ukumbi wa Siasa ni kilimo mjini Iringa.
Akichangia mada juu ya kuendelea utalii wa mikoa ya kusini Limbeli alisema kuwa mbali ya jitihada hizo ila zipo changamoto mbali mbali zinazopaswa kufanyiwa kazi katika mkoa wa Iringa ikiwemo ya Hoteli zake kuwa na gharama kubwa huku huduma wanazotoa zikiwa chini ya kiwango.
Kwani alisema kuwa inashangaza kuona baada ya Hoteli katika mji wa Iringa huduma zake zikiwa chini ya kiwango kwa kuuza kuku zaidi ya Tsh 40,000 bei ambayo ni kubwa ambayo bila kufanyiwa marekebesho suala la kutangaza utalii wa mikoa hiyo ya kusini inaweza kuwa ndoto.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Iringa mjini na waziri kivuli wa wizara ya maliasili na utalii mchungaji Peter Msigwa mbali ya kuwaomba radhi wahariri hao kwa kuhuduma mbaya ambayo wameipata katika baadhi ya Hoteli mjini Iringa bado alisema anafanya mkakati wa kukutana na wamiliki wa Hoteli hizo ili kuangalia jinsi ya kuboresha.
Wakati kaimu katibu tawala wa mkoa wa Iringa Adam Swai alisema kuwa mkoa wa Iringa utaendelea kukutana na wadau ili kusaidia kuhamasisha utalii mikoa ya kusini