Wadau wa kupinga masuala ya ukatili wa kijinsia wakiwa ktk maandamano ya kupinga ukatili wa kijinsia |
Kijana mkazi wa Mwangata katika Manispaa ya Iringa akichezea kichapo baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kumbaka mtoto wa miaka 12 hivi karibuni (picha na maktaba ya Francis Godwin Blog)
................................
Taarifa ya Demografia na Afya 2010 ilibaini kuwa wanawake wawili katika kila watano Tanzania wamewahi kukumbwa na ukatili wa kimwili tangu wakiwa na umri wa miaka 15 na mmoja katika kila watano wamewahi kukumbwa na ukatili wa kingono.
Â
Mwanaharakati wa mradi wa Champion mkoani Iringa Esther Majani anasema taarifa hizo za hali ya Ukatili wa Kijinsia nchini Tanzania zilitolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (National Bureau of Statistics) kama mojawapo ya vipengele kwenye Taarifa ya Demografia na Afya Tanzania ya mwaka 2010 (Demographic and Health Survey).
Alisema kuwa kimsingi siku hizo pia ni Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake.
Kauli mbiu ya kitaifa ya Kampeni ya Siku 16 mwaka 2013 ilikuwa ni
FUNGUKA! Tumia mamlaka yako kuzuia ukatili wa kijinsia
na ilimlenga kila mtu kujiangalia jukumu lake kama mhanga, mtenda ukatili na shuhuda katika kupinga ukatili wa kijinsia.
Wadau wa mkoa wa Iringa wanaofanya kazi za kupinga ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto waliandaa shughuli mbalimbali ndani ya manispaa na wilaya za Mufindi na Iringa Vijijini ambazo zililenga kuijumuisha jamii ya Iringa kufunguka na kuongelea tatizo hili mtambuka.