Quantcast
Channel: Francis Godwin ::Mzee wa matukio daima::
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2596

HIFADHI YA TAIFA YA ARUSHA NI HIFADHI PEKEE AMBAYO WANYAMA WAKE NI WATULIVU .

$
0
0
Twiga   wakiwa  wametulia katika  hifadhi ya taifa ya Arusha kama  walivyokutwa na camera ya matukio daima.com
Hifadhi  ya Taifa  ya Arusha  ilianzishwa  mwaka 1960 ni  hifadhi yenye ukubwa  wa  Kilomita za mraba 322 likijumuisha  mlima Meru wenye  urefu wa  mita 4566 juu ya usawa  wa bahari  huku madhari  nzuri  ya Mlima Kilimanjaro  huonekana na  kuvutia mno watalii wanaofika katika  hifadhi ya Arusha na kupanda Mlima Meru.

Historia ya hifadhi  ilianza mwaka 1976 ambapo Mhangari aitwaye Count Teleki alipotembelea maziwa ya Momella na kuhadithia juu ya wingi wa viboko na faru aliowaona japo hivi sasa faru hawapatikani tena  katika hifadhi hiyo ya taifa Arusha 

Mwaka 1907 familia ya mzungu aitwaye Trappe ilihamia Momella kwa  shughuli za ufugaji na uhifadhi  wa  wanyama  pori,wakati hifadhi  ilipoanzishwa mwaka 1960 eneo la shamba hili lilijumuisha ndani ya hifadhi.

..........Itaendelea.......



Viewing all articles
Browse latest Browse all 2596