Waziri mkuu Mizengo pinda
..........................................
Na Elizabeth Ntambala
Katavi
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda ametoa msaada wa sh milioni 20 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya Msikiti wa Tawfiq wa mjini hapa.
Msaada huo umetolewa na Mbunge wa Mlele,ambaye ni waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania uliokabidhiwa juzi na msadizi wake Charles Kanyanda kwa Sheikh Mkuu wa Mpanda,
Akikabidhiwa msaada huo Ali Hussen ambaye ni sheh''kutoka kwa Kanyanda alisema waziri mkuu ametimiza ombi lililotolewa kwake na viongozi wa msikiti huo alipokutana nao Januari mwaka huu.
Sheikh Hussein ambaye pia ni kaimu Sheikh wa Mkoa wa Katavi, alimshukuru Pinda kwa kuwajali huku akiwataka viongozi wengine waige mfano huo na kuzisaidia asasi za kidini zenye nia ya kusogeza huduma muhimu za kijamii kwa wananchi.
Akizungumzia ujenzi wa zahanati hiyo, alisema kukamilika kwake kutapunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali ya wilaya.
Imamu wa msikiti huo, Sheikh Mashaka Kakulukulu alisema shughuli za ujenzi zitaanza hivi karibuni na kwamba hospitali hiyo itakapokamilika, itakuwa na wodi ya wazazi na huduma nyingine muhimu.