Hatimaye serikali ya Tanzania imeziruhusu Timu za Simba, Yanga na Falcon ya Zanzibar kwenda kushiriki Michuano ya Kombe la Kagame nchini Sudan baada ya kupata barua kutoa serikali ya Sudan ikizihakikishia ulinzi wa uhakika Timu hizo.
Katika barua hiyo serikali ya Sudan imeihakikishia Tanzania kuwa wachezaji, viongozi na Mashabiki wa Timu zote watakuwa salama katika kipindi chote cha mashindano hayo yatakayokuwa ni ya wiki mbili nchini Sudan.
Tayari timu za Simba na Yanga zilishatangaza kujitoa na kuvunja kambi walizoweka kwa ajili ya kujiwinda na mshindano hayo huku kukiwa na taarifa kuwa Baraza la Michezo kwa Nchi za Afrika Mashariki na Kati-CECAFA nao kuzialika timu nyingine kuziba pengo hilo.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, AMOSI MAKALLA ameiambia Uhuru FM kuwa amethibitisha kupata barua kutoka serikali ya Sudan ingawa hata hivyo amesisitiza kuwa timu za Simba, Yanga na Falcon wao ndio watakakuwa waamuzi wa mwisho wa kuamua kuzipeleka timu zao au la.
Michuano hiyo ya Kagame inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 18 mwaka huu nchini Sudan.