Majeruhi wa ajali ya Bajaji Iringa Karim Raphael (14) mkazi wa Mshindo ' A' katika Manispaa ya Iringa akiwa katika Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa
Majeruhi wa ajali ya Bajaji Idd Waziri Ng'eng'ena (17) mkazi wa kijiweni mjini Iringa akiwa na majeraha usoni baada ya ajali hiyo mbaya ya Bajaji iliyosababisha kifo cha dereva wa Bajaji hiyo
Muuguzi katika Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa akimpatia matibabu majeruhi Karim
Idd na Karim wakisubiri kupelekwa wodini baada ya kupatiwa matibabu ya awali OPD |
AJALI mbaya ya Bajaji yasababisha kifo cha dereva wake ambae ni mfanyakazi wa maduka ya Mzalendo mjini Iringa Bw Sudi Hashimu (22) mkazi wa Mtwivila huku wengine wawili wakijeruhiwa vibaya.
Ajali hiyo mbaya imetokea majira ya saa 2 usiku wa kuamkia leo katika eneo la Mshindo mjini Iringa wakati dereva huyo wa Bajaji akijaribu kukimbia baada ya kudaiwa kusababisha ajali katika eneo la Miyomboni mjini Iringa.
Wakizungumza na mtandao wa www.matukiodaima.com majeruhi wa ajali hiyo Karim Raphael na Idd Waziri Ng’eng’ena walisema kuwa kabla ya ajali hiyo dereva huyo alikuwa amesababisha ajali kwa kumgonga mwendesha Bajaji mwenzake na baada ya tukio hilo aliamua kutimua mbio kwa kutumia usafiri wake wa Bajaji.
Kwani walisema kufuatia ajali hiyo eneo la Miyomboni ulizuka ugomvi kiasi cha aliyegongwa kupokonya kofia (Helmenti) ya Bajaji ya Sudi kabla ya marehemu huyo kufanikiwa kupokonya na kukimbia .
“Katika Bajaji marehemu alikuwa ametupakia abiria watatu ambapo mmoja aliruka kabla ya Bajaji hiyo kuchanganya zaidi hivyo tukabaki abiri wawili na dereva mwenyewe …hata hivyo alionekana kuendesha Bajaji hiyo kwa sifa zaidi na kuonyesha kuwa yeye ni bingwa wa kukimbiza Bajaji hiyo” alisema majeruhi Karimu
Hata hivyo alisema baada ya kufika eneo la Mshindo Kanisani katika tuta kubwa dereva huyo alishindwa kupunguza mwendo na hivyo kulivaa tuta hilo wakati akitaka kukata kona na Bajaji hiyo kuacha njia na kugonga ukuta wa uzio wa Kanisa la RC mshindo na dereva huyo kutanguliza kichwa katika ukuta huo huku wao wakifunikwa na Bajaji hiyo.
Walisema kuwa dereva huyo alikufa papo hapo huku wao wakishuhudia kifo chake kabla ya wasamaria wema kufika na kuwaokoa.
Kwa upande wake mmoja kati ya shuhuda wa tukio hilo Mood Mambo alisema kuwa alifika eneo hilo na kukuta wananchi wakiendelea kutoa msaada kwa watoto hao ambao walikuwa wamejeruhiwa vibaya na mwili wa marehemu ukiwa umepasuka kichwa .
Majeruhi hao walikimbizwa katika Hospital ya rufaa ya mkoa wa Iringa huku mwili wa marehemu huyu ukihifadhiwa katika chumba cha maiti katika Hospital hiyo.
Ajali hiyo ni ya pili kusababisha kifo kwa mkoa wa Iringa na ajali ya tatu mbaya kutokea katika mkoa wa Iringa toka mwaka 2014 ulipoanza ambapo ajali ya kwanza kusababisha kifo ilitokea wilaya ya Mufindi nay a pili kujeruhi ilitokea eneo la Ilala wakati wa mkesha wa Mwaka mpya ikiwa ni dakika 20 kuukaribisha mwaka mpya na kupelekea dereva wa boda boda kukatwa mguu wake nah ii ni ya tatu .
Hata hivyo ajali hizo zimeendelea kutokea mbali ya kuwepo jitihada kubwa zinazoendelea kufanywa na kamati ya usalama barabarani mkoa wa Iringa chini ya mwenyekiti wake Salim Asas katika kutoa elimu ya usalama barabarani kwa madereva boda boda mkoa wa Iringa ila bado ajali za boda boda zaendelea kutoa roho za vijana wanaofanya kazi hiyo
Sikiliza Video hii chini Shuhuda Karim anavyoshuhudia ajali hiyo na jinsi walivyopona kifo
Sikiliza Video hii chini Shuhuda Karim anavyoshuhudia ajali hiyo na jinsi walivyopona kifo