RPC -MUNGI |
MWANDISHI ,DIANA BISANGAO WA MATUKIO DAIMA.COM, IRINGA
JESHI la polisi mkoani Iringa linawashikirilia watu wawili kwa makosa mawili tofauti likiwemo la Ditrick Swadiko (18) mkazi wa Ndiuka kata ya Ruaha kumbaka mtoto wa miaka 4.
Akizungumza na mtandao huu wa www.matukiodaima.comofisini kwake leo Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea tarehe 20 januari majira ya saa 4 na nusu usiku.
Mungi alisema mtuhumiwa huyo alimbaka mtoto Khadija ambaye ni mwanafunzi wa awali katika shule ya msingi Ndiuka na kumsababishia maumivu makali sehemu za siri.
Na katika tukio jingine, Askari polisi wakiwa doria eneo la Mlandege walimkamata Isaya Kimota (27) mfanyabiashara na mkazi wa Ipogoro manispaa ya Iringa kwa kosa la kukutwa na bangi.
Kamanda Mungi alisema tukio hilo lilitokea tarehe 20 januari majira ya saa 5 kamili usiku ambapo mtuhumiwa huyo alikutwa na bangi gramu 200 aliyokuwa ameihifadhi katika bahasha ya kaki.
Mbali na matukio hayo mawili tofauti, Kamanda Mungi alisema huko maeneo ya Lugalo kata ya Gangilonga manispaa ya Iringa, watu wasiojulikana waliiba pikipiki aina ya Sunlg yenye namba za usajili T 969 CEQ yenye chases namba LBRSPJB53C901897 yenye thamani ya shilingi 200,000,000/= ambayo ni mali ya Calist Tairo, watuhumiwa wanatafutwa.