Quantcast
Channel: Francis Godwin ::Mzee wa matukio daima::
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2596

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI YAJIVUNIA MAFANIKIO ILIYOYAPATA

$
0
0
                                Naibu  waziri wa  wizara  ya  mambo  ya  ndani  ya  nchi  mheshimiwa  Pereira  Ame  Silima kati akizungumza na  wanahabari leo 
..............................................................................................
Mwandishi ,Kenneth John ,matukiodaima.com ,Dar es Salaam 

Wizara  ya  mambo  ya  ndani  ya  nchi   imeweka  bayana  miongoni  mwa  mafanikio  waliyoyapata  katika  kipindi  cha  serikali   ya  awamu  ya  nne  ambayo  ni  pamoja  na  kutekeleza  majukumu  yake  kwa  ufanisi   na  kuiwezesha  nchi  kuwa  na  amani  na  utulivu.
Akizungumza  na  waandishi  wa  habari  jijini  Dar   es  salaam  naibu  waziri    wa  wizara  ya  mambo  ya  ndani  ya  nchi  mheshimiwa  Pereira  Ame  Silima  alisema  kuwa  kwa  wastani   wanaweza  kusema    nchi  imekuwa  na  usalama  ambao  unawawezesha  wananchi  na  wageni  kuendelea  kufanya  shughuli  zao   za  kijamii  na  kiuchumi,licha  ya  matukio  ya  hapa  na  pale, ambayo  wizara  inaendelea  kuyachukulia  hatua  na  kuyatafutia  ufumbuzi.
Akibainisha  baadhi  ya  mafanikio  hayo  kupitia  idara mbalimbali  zinazounda  wizara hiyo  ya  mambo  ya  ndani  ya  nchi  mheshimiwa  Silima  alisema  kuwa  kupitia    jeshi   la  polisi  mafanikio  waliyopata  ni  pamoja  na  kudhibiti  vitendo  vya  uhalifu  vilivyokuwa  vimeanza  kukithiri  hapa  nchini   ambapo  vitendo  hivyo  ni  pamoja  na  matukio  ya  ujambazi   wa  kutumia  silaha, wizi  katika  mabenki,  mauaji  ya  watu  wenye  ulemavu  wa  ngozi  yaani  albino  na  makosa  mengine  ya  kijinai .

Pamoja  na  hayo  naibu  waziri  Silima  alisema  kuwa  pia  wamefanikiwa  kujenga  nyumba  491  kwa  ajili  ya  askari  polisi  ambaozo  zimejengwa   kote  nchini  yakiwemo  maghorofa  84  yaliyojengwa  Dar  es  salaam,matatu   Zanzibar  na mengine  matatu   Pemba.Pamoja  na  kuendeleza  ujenzi katika  maeneo   mengine  nchini.

Na  kwa  upande  wa  Jeshi  la  magereza  mheshimiwa  Silima  alisema  kuwa  katika  jeshi  hilo  wamefanikiwa  kuimarisha  shughuli  za  utunzaji  na  urekebishaji  wafungwa, pia  wizara  kupitia  jeshi  la  magereza  imefanikiwa  kukarabati  majengo  na  miundombinu  ya  magereza  likiwemo  Gereza  lenye  ulinzi  mkali  la  Butimba  na  ukarabati  wa  majengo  mengine  ya  ofisi  za  utawala  ambao  umefanyika  katika  magereza  ya  Uyui,Lilungu,Maweni, Isanga,Keko  na  Ukonga.hata  hivyo  naibu  waziri  aliongeza  kuwa  ukarabati  na  ukamilishaji  wa  mabweni  ya  wafungwa  katika  magereza  24  nchini kwa  lengo  la  kuhakikisha  kuwa  usalama  wa  wafungwa  unaimarishwa.
Vile  vile  mheshimiwa    Silima  alisema  kuwa  katika  jeshi  la  zimamoto  na  uokoaji  wameweza   kupunguza  majanga  ya  moto  kwa  kiasi  kikubwa, Pia  ofisi  za  zimamoto  na  uokoaji  zimeanzishwa  katika  mikoa  yote  nchini  na  zinaongozwa  na  makamanda  wa  zimamoto  wa  mkoa.Aidha  aliendelea  kusema  kuwa  vituo  vipya  vya  zimamoto  na  uokoaji  vimejengwa   katika  maeneo  ya  Lugalo,wilaya  ya  kinondoni  na  mchicha  wilaya  ya  Temeke  jijini  Dar  es  salaam  na  vituo  vidogo  katika  maeneo  ya   Karatu, wilayani  Karatu  mkoani  Manyara  na  Same,wilayani  Same  mkoani  Kilimanjaro.
Pia  naibu  waziri  alisema  kuwa  katika  jeshi  hilo  la  zimamoto  na  uokozi  wameweza  kufanikiwa  kununua  jumla  ya  magari  ya  kuzimia  moto  25   na  askari  379   na  watumishi  raia  28  wameajiriwa  kwa  lengo  la  kuongeza   nguvu kazi.
Na  kwa  upande  wa  mafanikio  katika   Idara  ya  uhamiaji  naibu  waziri  mheshimiwa  Pereira  Ame  Silima  alisema  kuwa  wizara  imefanikiwa  kutoa  pasi  za  kusafiria  za  kawaida  534,855,  za  kiutumishi  4,035,  za  ki-balozi  2,172  na  za  Afrika  mashariki  13,220. Aidha  katika  kipindi  cha  januari  2006  hadi  Desemba  2013  wahamiaji  haramu  65,675  walikamatwa  na  kuchukuliwa  hatua  mbalimbali  za  kisheria  na  kati  ya  wahamiaji  hao  haramu  31,203  walipatikana  wakati  wa  operesheni  kimbunga,iliyotekelezwa  kati  ya  mwezi  Septemba  na  Oktoba  mwaka  2013.
Pamoja  na  mafanikio  yote  hayo  katika  idara  mbalimbali  za  wizara  hiyo  mheshimiwa  naibu  waziri  Pereira  Ame  Silima  pia  alibainisha  baadhi  ya  changamoto  zinazoikabili  wizara  hiyo  ambapo  ni  pamoja  na  ongezeko  la  kasi  la  mahitaji ya  huduma  ya  ulinzi  na  usalama  wa  raia  ikilinganishwa  na  rasilimali  na  vitendea  kazi  vilivyopo,kubadilika  kwa  mbinu  za  kutenda  uhalifu, Ongezeko  la  makosa  makubwa  na  madogo  yanayofanywa  kwa  njia  ya  mtandao,  ufinyu   wa  bajeti  ambao  unakwamisha  utekelezaji  wa  baadhi  ya  majukumu  na  miradi  ya  maendeleo,kama  vile  shughuli  za  ujenzi  wa  ofisi  na  makazi  ya  watumishi  na askari,  ununuzi  wa  vifaa   na  dhana  mbalimbali  za  kazi  na  uhaba  wa  watumishi, Ujenzi  holela  katika  maeneo  ya  mjini  ambao  unachangia  kukwamisha  juhudi  za  kuboresha  huduma  za  zimamoto  na  uokoaji  pamoja  na  kujengeka  kwa  tabia  ya  baadhi  ya  wananchi  kujichukulia  sheria  mkononi na  kufanya  vitendo vya  uharifu.   


NYUMBA INAUZWA BEI POA IPO IRINGA MJINI ENEO LA MKIMBIZI BIMA JIRANI NA KITUO CHA CHA YATIMA CHA DAILY DREAD













Nyumba  hii   ipo katika hali nzuri  na  kuna  wapangaji wanaishi

Sifa  zake
> Ina vyumba  vitatu  vya kulala ,choo cha  ndani ,stoo,jiko na Sebule kubwa
>Hati  ipo nyumba   ipo na  vielelezo vyote nyeti

>Eneo ambalo  limejengwa ni alisimia 30  ya  uwanja

> uwanja una  ukubwa wa Skwea mita 525
>Maji na umeme  upo

> Barabara inafika hapa nyumbani
Nyumba  hii  inauzwa  Tsh  milioni 60  maelewano  yapo 

> Nyumba  ipo  eneo la Mkimbizi Bima  katika Manispaa ya  Iringa jirani na kituo cha  Yatima  cha  Deily Bread
Kwa mawasiliano piga simu namba 0754 026 299/0789281030/0712750 199



Viewing all articles
Browse latest Browse all 2596

Trending Articles