Afisa Mfawidhi SUMATRA Kanda ya Ziwa Japhet Leisimaye Ole akiwatuliza abiria ambao walikuwa wakihitaji kusafiri katika eneo la Kamanga kufuatia mgomo wa wafanyakazi wa kivuko cha MV. Orion. |
'Abiria wetu tunawaomba mtuvumilie, tunahitaji haki zetu' Lilisomeka moja ya bango la waaandamanaji hao. |
Safari ilisitishwa kwa muda mpaka kieleweke. |
Mv. Orion |
Kapteni wa MV. ORION Adam Yusuph akiongoza meli yake huku Afisa Mfawidhi wa SUMATRA Kanda ya Ziwa Japhet Leisimaye Ole akijiridhisha juu ya ubora wa usafiri huo katika utoaji huduma. |
Safari inasonga. |
Ratiba. |
Mfanyakazi wa Kamanga Ferry akitoa maelekezo kwa abiria jinsi ya kuvaa jaketi la kujiokoa wakati wa ajali. |
Safari imefikia ukingoni. |
Mahojiano na wananchi. |
Hatimaye mgomo umepatiwa utatuzi nacho chombo kinaendelea na utoaji huduma. |
Mwandishi,William Bundala wa matukiodaima.com ,Mwanza
......................................................................................................
WATUMISHI wa Kampuni ya Kamanga Fery ya Wilayani Sengerema leo wameweka mgomo ukishinikiza kuondolewea kwa watumishi wenzao wawaili na kusimamisha utowaji huduma ya usafiri wa abiria na magari Jijini hapa.
Hatua hiyo ilielezwa na Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi Adamu Yusufu ambaye pia ni Kepteni wa kivuko cha MV Orion cha Kampuni ya Kamanga Fery Ltd. kinachotoa huduma kati ya Kamanga Wilayani Sengerema na Kamanga Jijini Mwanza.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za kampuni hiyo Mwenyekiti Kapteni Yusufu alisema kwamba wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa ujumla wao wameamua kugoma kutoa huduma ili kushinikiza Mkurugenzi Wiebke Gaetye kuwaondoa watumishi Renatus Manyanda (Meneja rasilimali watu) na Anna Malapa (Mhasibu matumizi) kutokana na kuwanyanyasa wafanyakazi wa Kampuni hiyo.
Mwenyekiti huyo alitaja sababu za mgomo huo kuwa ni pamoja na Manyanda kuwafukuza watumishi bila kosa, kushindwa kulipa makato ya mishahara yao kwenye Mfuko wa Jamii (NSSF), kushindwa kulipa mishahara zao kwa wakati ambapo wanadai tangu mwezi Novemba mwaka jana na kushindwa kufanya matengenezo ya vivuko vya kampuni hiyo kwa wakati.
“Bila Mkurugenzi kuyashughulikia haya tunayolalamikia ikiwa ni pamoja na kutuondolea watumishi hawa wanaolalamikiwa na wenzao, nasi hatuko tayari kufanya kazi na tutaendelea na mgomo hadi kilio chetu kitakaposikilizwa na kutolewa majibu” alisisitiza.
Kwa upande wa Mhasibu Malapa alisema kwamba amekuwa akiwanyima malipo yanayoizinishwa na Mkurugenzi ama uongozi wa Kampuni hiyo na hata amekuwa akitoa kauli za kuwakejeli watumishi wenzake jambo ambalo wamedai kuchoshwa nalo.
Kufatia mgomo huo uliodumu kwa masaa kadhaa na kupelekea Mkurugenzi Gaetye kuchukua jukumu la kukaa na wafanyakazi ili kusikiliza hoja na malalamiko yao ambapo aliamua kumfukuza kazi kwanza Manyanda kisha kusikiliza malalamiko mengine ili kupoza hasira za wafanyakazi hao.
Akizungumza madai ya wafanyakazi hao Mkurugenzi huyo alisema kwamba tayari amemfukuza kazi huku hoja za malipo ya mishahara yao ataifanyia kazi haraka na ile ya NSSF huku Mhasibu Malapa akisimamishwa kwanza kuchunguzwa na uamuzi wake ukisubili kikao cha uongozi wa Kampuni.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi (Cotwu) tawi la Kampuni hiyo Kapteni Jorwa Magesa (MV Orion) alisema kwamba kufatia kikao na Mkurugenzi wao wamelidhika na hatua alizochukua na wamempatia muda kushughulikia mambo mengine yaliyosalia ikiwa ni malalamiko yao ya msingi.
Hatua ya kuondolewa kwa Manyanda imepongezwa na wafanyakazi na wananchi wa Kijiji cha Kamanga Wilayani Sengerema ambao juzi majira ya jioni waliandamana na mabango kumpinga kuendelea kuwa mfanyakazi wa Kampuni hiyo hali hiyo ilipelekea jana kuwepo mgomo mkali kwa wafanyakazi hao nao wakipinga kuendelea kuwepo kwa watu hao katika Kampuni hiyo.
Manyanda pia amelalamikiwa na baadhi ya wafanyakazi waliokataa kutajwa majina yao hadharani kwa madai kuwa Manyanda alikuwa akitumia pia Jina la Mama Salma Kikwete kumtishia Mkurugenzi huyo raia wa Taifa moja la Ulaya kuwa akimfukuza naye ataondolewa nchini.
Hadi tunakwenda mitamboni hali ya eneo la Kamanga fery ilikuwa shwari baada ya Mkurugenzi na wafanyakazi wake kukubaliana kuendelee kutolewa huduma ya usafiri wa abiria na magari wakati madai yao mengine yakishughulikiwa na kuchukuliwa hatua za haraka kama walivyokubaliana.