Quantcast
Channel: Francis Godwin ::Mzee wa matukio daima::
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2596

NG'OMBE HANENEPI SIKU YA MNADA ,LEO NDIO LEO RUAHA MARATHON KUTIMUA MBIO IRINGA ASUBUHI HII

$
0
0


Ndugu zangu, 

Mwaka jana nilikimbia na kumaliza mbio za kilomita 21 kwa muda wa heshima kabisa, chini ya saa mbili.  Ni Ruaha Marathon hapa Iringa.

Na  leo  Jumamosi kuna Ruaha Marathon ya pili. Sitakimbia. Maana, Afrika usiianze safari kabla ya kuupima upepo wa safari yenyewe.
 
Kila jambo na maandalizi. Katika miezi ya karibuni ratiba


zangu za jogging zimevurugika kiasi. Hivyo, siko kwenye physical form ya  kawaida yangu. Na kilomita 21 ni kilomita 21. Ni sawa na kutoka Ubungo hadi Kibamba. Ukizilazimisha unaweza kuzimaliza kwa kubebwa kwenye machela, kama zipo!

Naam, kwa mwanadamu muhimu ni kutambua, kuwa kwa kila jambo unalotaka kutenda, basi, jitahidi kufanya maandalizi. Na maandalizi yasifanywe siku ya tukio lenyewe.

Vinginevyo itakuwa sawa na kisa cha bwana aliyeshtuka siku ya mnada na kuamua kumlisha ng'ombe wangu majani mengi ili aongezeke kilo!

Na Wahenga walisema; ng’ombe hanenepi siku ya mnada!

Nawatakia Marathon njema wote watakaokimbia hiyo kesho.

Maggid,
Iringa
0754 678 252

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2596

Trending Articles