Quantcast
Channel: Francis Godwin ::Mzee wa matukio daima::
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2596

MWENYEKITI WA CHADEMA NJOMBE NA WAFUASI WAKE MATATANI KWA KUVAMIA KIKAO CHA NDANI CHA CCM NA BASTOLA

$
0
0
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe SACP Fulgency Ngonyani
...............................................................................................................................

MWENYEKITI  wa chama  cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) kata ya  Njombe  mjini  jimbo la Njombe kusini mkoa wa Njombe Ally Mhagama Maarufu kwa jina la Dr   Sagasaga na  wafuasi  wake  matatani kwa  kuvamia kikao  cha ndani  cha chama  cha Mapinduzi (CCM) huku  wakiwa na bastola.


 Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Njombe SACP Fulgency Ngonyani Amesema Kuwa Jeshi  lake  limekamilisha taratibu zote za Uchunguzi na Upepelezi Kufuatia Kukamatwa kwa watu watano wanaodaiwa kufanya fujo na Kukutwa na Silaha Katika Mkutano wa Ndani wa Chama cha Mapinduzi CCM Mjini Njombe hivi Karibuni.

Kamanda Ngonyani  alisema  kuwa  Mwenendo wa Kisiasa Katika Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Udiwani Unaotarajiwa Kufanyika Februari Tisa Mwaka Huu Katika Vituo Mbalimbali Vya Uchaguzi Katika Kata ya Njombe Mjini,Unao Vihusisha Vyama vya CCM na Chadema  unaendelea  vema  mbali ya  kuwepo kwa matukio kama  hayo

Hata  hivyo alisema kuwa tayari Jeshi la Polisi limefunga upelelezi wa  tukio hilo na Kupeleka jalada la kesi hiyo Katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mkoa wa Njombe na Kinachosubiriwa Kwa Sasa ni Maamuzi Kutoka  Ofisi Hiyo Ikiwa Kesi hiyo Itapelekwa Mahakamani au lah
 

Kamanda Ngonyani Amesema  kuwa kesi ya hiyo ya aliyekamatwa na  Silaha Katika eneo la Vurugu Hizo,Uchunguzi umeonesha Kuwa mtuhumiwa Huyo Anamiliki Silaha hiyo kwa mujibu wa Sheria licha ya kuwa bado anaendelea kukabiliwa na kosa  kutembea na  silaha hiyo katika mikutano ya kampeni  ya  Chadema.


Kamanda wa Polisi Mkoani Njombe Fulgency Ngonyani  kwa  upande wa Chadema wanaoshikiliwa na mbali ya mwenyekiti  wao   Sagasaga mwingine ni Howard Kalonga na Robert Shejamabu Wote Wakazi wa Mjini Njombe.
 

Pia alisema Jeshi la Polisi linawashikilia wafuasi wawili wa Chama Cha Mapinduzi CCM kwa tuhuma za kumshambulia askari Polisi aliyefika eneo la tukio kwa  ajili ya kusaidia kuwanusuru viongozi na  wanachama wa CCM waliovamiwa na wafuasi hao wa Chadema wakiwa na silaha  hiyo mtaa wa SIDO mjini  hapa

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2596

Trending Articles