mshindi wa kura za maoni jimbo la kalenga mwanasheria SINKALA MWENDA akipongezwa |
wajumbe wa mkutano wa kura za maoni jimbo la kalenga wakifuatilia matokeo ya uchaguzi leo
msimamizi mkuu wa uchaguzi huo Bw Benison Kigaila akitoa maelekezo ya chama
kada aliyeshika nafasi ya pili ktika mchakato huo GRACE TENDEGA kushoto akiwa na wagombea wenzake
Kada muuza magazeti Aidani Pungili kushoto akiwa na wagombea wenzake
Mwenda ametangazwa mshindi wa kura za maoni katika uchaguzi uliofanyika leo toka majira ya saa 4 asubuhi na kumalizika majira ya saa 4 usiku katika ukumbi wa St Dominic mjini Iringa .
Uchaguzi huo uliosimamiwa na mjumbe wa kamati kuu ya Chadema Taifa Chiku Abwao na Benison Kigaila wajumbe wa mkutano wa Halmashauri kuu ya Chadema jimbo la kalenga waliumiza vichwa vyao kuwasikiliza wagombea wote 13 kabla ya kuwachuja na kumchangua mwanasheria Mwenda kwa kura 132 dhidi ya kura 122 alizopata mpinzani wake wa karibu Grace Tendega ambae pia alikuwa akipewa nafasi kubwa ya kushinda kutokana na kuwa na historia ya kugombea kupitia chama cha Jahazi Asilia na kutoa ushindani mkali kwa CCM kabla ya kuhamia Chadema.
Mbali ya wapinzani hao wakubwa kuvutana vikali bado kada muuza magazeti maarufu mjini Iringa Aidan Pungili ambae pia alikuwa akipewa nafasi ya kufanya vizuri katika uchaguzi huo aliambulia kura 2 pekee huku mwenzake Daniel Luvanga akipata kura moja ya kufutia machozi .
Wagombea wengine ambao wameonyesha kufanya vema kiasi baada ya kujiunga na Chadema wakitokea CCM ni pamoja na Dr Evaristo Mtitu aliyepata kura 32,Ancent Sambala ambae amepata kuwania ubunge katika kura za maoni CCM kwa zaidi ya mara 2 katika jimbo la kalenga kabla ya kuhamia Chadema pia aliambulia nafasi ya tano kwa kupata kura 22 tofauti na nafasi saba aliyochukua mwaka 2005 akiwa ndani ya CCM kwa kupata kura chini ya 8.
Pia mgombea Akbar Sanga katika uchaguzi huo alipata kura (21),Rehema Makoga (4), Henry Kavina(9), Mussa Mdede(48), Mchungaji Samweli Nyakunga(2) na mwalimu Vitus Lawa akipata kura (14).
Msimamizi mkuu wa uchaguzi huo mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Chadema, Benson Kigaila aliwataka wajumbe wa mkutano huo kutoshangilia zaidi juu ya matokeo hayo kwani kushinda katika kinyang'anyiro ni mwanzo tu wa safari ya kumpata mteule wa Chadema atakayekabidhiwa bendera ya Chadema kuvaana na CCM katika uchaguzi huo mdogo.
Alisema mgombea sahihi ambae watapaswa kumshangilia na kumtangaza kwa wananchi wa jimbo la Kalenga ni yulev ambae atapitishwa na vikao vya juu vya Chama hicho Taifa tarehe 14 mwezi huu.
Hata hivyo aliwataka wagombea wote 13 walioomba kuwania nafasi hiyo kabla ya kupatikana mshindi huo Mwenda kuanza safari mapema kesho Alhamis asubuhi ya kwenda jijini Dar es salaam kwa ajili ya kwenda kujieleza mbele ya kamati kuu ya Chadema kabla ya kumteua mgombea wa jimbo hilo la kalenga.
"Baada ya matokeo haya ndugu zangu wajumbe nawaombeni makatibu kata wote wa jimbo la Kalenga kubaki hapa ndani na wajumbe kuanza safari ya kurudi majumbani leo hata hatutaruhusu wagombea ama mshindi kuongea chochote .....kwani wote watakwenda kuongea mbele ya kamati kuu ila kuanzia kesho Chadema itaendelea na mikutano yake jimbo la kalenga ya kukitambulisha chama zaidi kwa wananchi na sio kumnadi mgombea kwani bado mgombea wetu hajapatikana kampeni zenyewe zitaanza baada ya mgombea wetu atakayeteuliwa kuchukua na kurejesha fomu ya tume"
Kigaila aliwataka viongozi hao wa Chadema jimbo la kalenga kuanza kukijenga zaidi chama hicho na kuwa mara baada ya kampeni kuanza wana Chadema wilaya zote za mkoa wa Iringa wataingia kazini katika jimbo hilo.
mmoja kati ya wagombea walioomba ashindwa kutokea ukumbini atuma mpambe kumsomea maelezo yake huku akieleza kuwa iwapo atapitishwa kuwa mgombea tayari ametenga kiasi cha Tsh milioni 9 kwa ajili ya kampeni zake kitendo cha kutofika ukumbini hapo kilionyesha kuwakwaza wajumbe kuwa hawana shida na pesa zake hivyo kumnyima nafasi hiyo.
Huku kituko namba mbili kutoka kwa wagombea hao ni baada ya mmoja wapo kudanganya kiwango chake cha elimu na kuongopa chuo alichopata elimu yake na kushindwa kutamka vema kiwango cha elimu alicho nacho hivyo wajumbe kushindwa kuamini maelezo yake na kumnyima pia kura.
Kituko kikubwa cha tatu ni pale mmoja kati ya wagombea kutumia CV yake ya kufungwa jela mara kwa mara kama mtaji wa kuombea kura huku wajumbe hao wakishindwa kujua umaarufu wake wa kufungwa na maendeleo ya wana Kalenga vina mahusiano gani hivyo kumpiga chini pia.