Ubalozi wa Jamhuri ya Indonesia kwa kushirikiana naWizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, unapenda kuvijulisha vyombo vyote vya habari nchini kuwa kutakuwa na Mkutano wa pili wa ushirikiano baina ya nchi za Mashariki mwa Asia kuhusu Maendeleo ya Palestina (2nd Conference of Cooperation among East Asian Countries for Palestinian Development - CEAPAD II) ambao utafanyika Jakarta, nchini Indonesia kuanzia tarehe 28 Februari hadi tarehe 2 Machi 2014.
Vyombo vya Habari vitakavyopenda kushiriki mkutano huo viwasiliane na Ubalozi wa Jamhuri ya Indonesia nchini.
Imetolewa na: Idara ya Habari - MAELEZO