Taarifa kwa Umma:Vipindi vya mvua kubwa vinatarajiwa.
Taarifa Na.
Muda wa Kutolewa
Saa za Afrika Mashariki
Daraja la Taarifa:
Kuanzia:
Tarehe
Mpaka:
Tarehe
Aina ya Tukio Linalotarajiwa
Kiwango cha uhakika:
Maeneo yanayotarajiwa
kuathirika
Maelezo:
Angalizo:
Maelezo ya Ziada
201403-01
Saa 10:00 Jioni
Tahadhari
05 Machi, 2014
07 Machi, 2014
Vipindi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya saa 24
vinatarajiwa.
Wastani (65%)
Ukanda wote wa Pwani (Mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Dar es
Salaam, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba).
Hali hii inatokana na kuimalika kwa mgandamizo mdogo wa hewa
mashariki mwa bahari ya Hindi sambamba na kusogea kwa haraka kwa
mfumo wa mvua za msimu (ITCZ) hivyo kuongeza kiwango cha
unyevunyevu kutoka baharini kuelekea maeneo tajwa hapo juu.
Wakazi na watumiaji wa Bahari pamoja na mamlaka zinazohusika na
maafa, wanashauriwa kuchukua tahadhari stahiki.
Mvua zinazoendelea na zinazotarajiwa kunyesha zinaashiria kuanza
mapema kwa mvua za masika katika baadhi ya maeneo ya pwani ya
kasikazini ikiwemo Dar es Salaam.
Mamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia hali hii na itatoa
mrejeo kila itakapobidi.
Imetolewa na
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.