Baadhi ya washiriki wakicheza huku na kushangilia katika kongamano lililoandaliwa na mtandao wa kijinsia TGNP jijini Dar es salaam |
Kaimu mkurugenzi wa mtandao wa kijinsia TGNP Lilian Lihundi akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam. |
Mkurugenzi wa chuo cha mafunzo ya jinsia (GTI)Bi Zuki Mihyo akiongea na waandishi wa habari ambao hawapo pichani..
...................................................
Mwandishi Kenneth John wa matukiodaima.com Dar
...................................................
Mwandishi Kenneth John wa matukiodaima.com Dar
Mtandao wa jinsia Tanzania TGNP umetoa wito kwa wanawake nchini pamoja na wadau mbalimbali kutambua mchango wa wanawake katika maendeleo kwa kusisitiza mchakato wa kuandikwa kwa rasimu ya pili ya katiba kuwatetea wanawake.
Wito huo umetolewa jijini Dar es salaam na katika kongamano maalum la jinsia lililoandaliwa na mtandao huo,Wakati wakuelekea siku ya wanawake duniani inayoadhimishwa Machi 8 kila mwaka na huku kauli mbiu ya mwaka huu ikisema Chochea mabadiliko kuleta usawa wa kijinsia kikatiba.
Kaimu mkurugenzi wa mtandao wa kijinsia TGNP LIlian Lihundi amesema kuwa wanahitaji kujadili kwa kina ni masuala gani ya wanawake yaliyoingia kwenye rasimu ya pili sambamba na kuangalia ni masuala gani ambayo bado yanahitajika lakini bado hayajaingia kwenye rasimu hii ya pili, na nini kifanyike ili kuweza kushiriki vizuri katika mchakato huo.
Aidha Lihundi ameongeza kuwa wananchi watanzania wanajua kuwa rasilimali kubwa ya walipa kodi imetumika katika kuandaa mchakato wa katiba mpya hivyo kuwasihi wabunge wa bunge la katiba kuweka mbele maslai ya wananchi na kuweka kando maslai yao binafsi, sambamba na kuwasihi kutumia muda vizuri ili kukamilisha kazi hiyo kwa wakati
Akizungumzia malengo ya millennia yanayotarajia kukamilika baada ya mwaka 2015 , Mkurugenzi wa mtandao wa jinsia TGNP Usu Mallya amesema kuwa malengo hayo katika nchi mbalimbali yamefanikiwa kwa kiwango tofauti tofauti kulingana na hali halisi ya nchi kisiasa kiuchumi kihistoria na kiutamaduni, na kuongeza kuwa kikubwa ambacho dunia imejifunza juu ya malengo hayo ya millennia ni kuwa malengo mengine yalikuwa mapana na huku malengo mahususi ya utekelezaji kutokuwekewa misingi ya kubomoa mifumo inayoendeleza tofauti mbalimbali duniania.Huku akitolea mfano wa lengo la kuondoa umasikini.
“Ili lengo la kuondoa umasikini lifanikiwe lazima dunia ikubali kwamba umasikini unatokana na mifumo ya ukandamizaji wa kirasilimali kati ya nchi zinazoitwa tajiri na nchi masikini,ambapo kwa kiwango kikubwa nchi masikini zimekuwa zinapokea misaada na vitu vingine lakini zinatoa rasilimali zake kwa kiwango kikubwa”Alisema Mallya.
Akifafanua juu ya malengo ya TGNP kuadhimisha siku ya wanawake duniani Mkurugenzi wa chuo cha mafunzo ya jinsia (GTI) Bi Zuki Mihyo amesema lengo la kongamano hilo ni kutafakari maendeleo katika kufikia usawa wa kijinsia kwa kuzingatia malengo ya millennia baada ya mwaka 2015,pamoja na kujenga mikakati na mshikamano, kuhakikisha madai ya wanawake yanasimamiwa ili katiba mpya iwe na mlengo wa kijinsia, Sambamba na kupashana habari.