Quantcast
Channel: Francis Godwin ::Mzee wa matukio daima::
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2596

ABIRIA AFIA NDANI YA BASI MKOANI IRINGA

$
0
0
 
Watu watatu wafariki dunia katika matukio matatu tofauti mkoani Iringa likiwemo la abiria mmoja kufariki ndani ya basi akiwa safarini.

Akizungumza na mtandao huu wa www.matukiodaima.com ofisini kwake Kamanda wa polisi mkoani Iringa Ramadhani Mungi alithibitisha kutokea kwa matukio yote matatu.

Tukio la kwanza lilitokea mnamo tarehe 5 machi katika eneo la kituo cha ukaguzi wa magari cha polisi kilichopo Igumbilo na kulitaja jina la marehemu ni Selemani Saidi (43) ambapo abiria huyo alikuwa anasafiri kwa basi la Super Feo lenye namba za usajili T.384 CAY akitokea Dar Es Salaam kuelekea Songea.

Kamanda alisema katika uchunguzi wa awali ulionyesha abiria huyo alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya upungufu wa kinga mwilini.

Katika tukio lingine mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Paul Kolija (60) alikutwa chumbani kwake akiwa amejinyonga kwa kutumia kamba aina ya katani.

Tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 5 machi majira ya saa 8 kamili mchana katika kijiji cha Mbuyuni, kata ya Itunundu, tarafa ya Pawaga wilaya ya Iringa Vijijini, huku uchunguzi wa awali ulionyesha kuwa marehemu alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa akili.

Mbali na matukio hayo mawili, Kamanda Mungi alisema mtu mmoja jina Alfred Mapembe (43) amejinyonga kwa kutumia kamba ya chandarua.

Tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 5 machi majira ya saa 10 kamili alfajiri katika kijiji cha Uhambingeto tarafa ya Mazombe wilaya ya Kilolo.

Uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa marehemu huyo alikuwa hana mahusiano mazuri na mwenza wake wa ndoa kwa muda mrefu, ambapo siku ya tukio alienda kujinyongea kwenye mti uliopo nje ya nyumba yake.

NA DIANA BISANGAO WA MATUKIO DAIMA.COM, IRINGA.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2596

Trending Articles