Vijana wawili wa kiume wenye asili ya nchi ya Kiasia wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kujihusisha na matukio ya utekaji nyara.
Mwandishi Kenneth John wa matukiodaima.com anaripoti kuwa Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Kamanda wa kanda maalum ya Dar es salaam , Kamishina Suleiman Kova amesema kuwa vijana hao wenye umri wa miaka 24 wote,waliamua kuwateka nyara wasichana wawili wa mfanyabiashara maarufu jijini humo ambaye anajishughurisha na biashara ya kuuza simu na vifaa vya umeme eneo la Samora.
Akifafanua zaidi juu ya tukio hilo kamishina Kova alisema kuwa , mpango wa vijana hao wawili ulipokamilika vijana hao walianza kutafuta watu wa kuwasaidia kuwakamata wasichana hao, pamoja na kuwatishia kwa silaa ili ili waweze kuwakabidhi na kisha kuondoka nao mahali walipokuwa wamepanga kwenda kuwaficha.
Kamishina Kova aliendelea kusema kuwa baada ya jeshi la polisi kupata taarifa juu ya mpango wa tukio hilo, makachero wa polisi waliingilia mtandao wa tukio hilo la utekaji nyara na hatimaye kufanikiwa kuwanasa watuhumiwa hao wote wawili.Na kuongeza kuwa waarifu hao walikuwa na mbinu nyingi sana katika kuhakikisha wanafanikiwa,
Kamishina Kova amesema kwa kutumia mbinu za kisasa pamoja na mawasiliano ya jeshi la polisi walifanikiwa kuwakamata , na hadi sasa watuhumiwa hao wameshahojiwa na wamekili kutaka kufanya tukio hilo huku wakisema kuwa endapo wangefanikiwa katika tukio hilo wangejipatia takribani shilingi milioni mia tano.Na ndipo wangewaachia wasichana hao.
“Suala la utekaji nyara ni makosa ambayo yanatishio kubwa sana katika jamii, na ndio maana sisi jeshi la polisi tukajitokeza na kufanya kazi hiyo zaidi ya masaa 24 bila kulala na kuhakikisha kwamba kweli tunaokoa wasichana wasitekwe Nyara”Alisema Kamishina Kova.
Pamoja na hayo kamishina Kova amewashukuru familia ya mfanyabiashara huyo , kwa kujitahidi sana kwa hali na mali na kushirikiana vizuri na jeshi la polisi hadi kufikia hatua ya wasichana hao kuwa salama hadi sasa.Huku akiwataka wasichana hao kutokuwa na wasiwasi na kuwahakikishia jeshi la polisi lipo na hao watuhumiwa hawajaachiwa na wala hawatapewa dhamana, ila kwasasa kinachosubiriwa ni mwanasheria wa serikali atakapotimiza mashitaka ndipo watapelekwa mahakamani na sheria kuchukua mkondo wake.