Akizungumza na wananchi wa Kigamboni, Kinana ameahidi kulichukua suala linaloonekana kuzua mgogoro mkubwa baina ya wananchi na serikali la ujenzi wa mji wa kisasa wa Kigamboni, Kinana ameahidi kulifikisha kwenye vikao vya ngazi ya juu kabisa vya CCM kwa uamuzi wa uhakika na wa kudumu.
Kinana amesema, baada ya kulifikisha kwenye vikao vya juu ya CCM atarejea tena Kigamboni kuzungumza na wananchi ili kuwapa majibu sahihi.
"Hapa ni lazima tujue, wazo la kubuniwa mradi huu lilianzishwa na nani, kwa lengo na maslahi gani, na wananchi ninyi mnaoishi hapa mlihusishwa kwa kiwango gani kuhakikisha mchakato mzima unakuwa halali kwa mujibu wa sheria za nchi", alisema Kinana.
Maelfu ya wananchi wakimsikiliza Kinana alipoowahurubia katia mkutano huo
Kassim Abdallah mkazi wa Vijibweni Kigamboni akitoa hoja zake mbele ya Kinana kuhusu mradi huo
Khalfan Iddi ambaye alikuwa kada wa CUF akikabidhi kadi yake kwa Kinana baada ya kuridhiwa na hotuba ya katibu mkuu huyo kwenye mkutano huo wa Kigamboni
Kinana akiagana na wananchi baada ya mkutano
Kinana akiongdoka uwanjani baada ya mkutano. Kulia ni mwenyekiti wa CCM Temeke, Yahya Sikunjema. Picha zote na Bashir NKoromo wa theNkoromo Blog