Rais Barack Obama wa Marekani akisalimiana na Rais Jakaya Kikwete alipotembelea nchini Marekani hivi karibuni |
Rais Obama |
Hali ilivyo kwa sasa eneo la Posta mpya jijini Dar es Salaam baada ya wafanyabiashara ndogo ndogo machinga na wauza magazeti na vocha eneo hilo kuondolewa na mgambo wa jiji katika zoezi la kusafisha jiji kwa ajili ya ugeni huo mkubwa nchini |
..................................................... ZIKIWA zimebaki siku chache kabla ya Rais wa Marekani Barack Obama kufanya ziara yake chini Tanzania ,wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama Machinga na wauza magazeti na vocha eneo la Posta mpya jijini Dar es Salaam wamedai kunyanyasika na mgambo wa jiji kupitia msako mkali unaofanyika . Msako huo umeanza mapema asubuhi ya leo katika eneo hilo la Posta na maeneo mbali mbali ya jiji la Dar es Salaam ambako msafara wa Rais Obama utapita kutokea uwanja wa kimataifa wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kuelekea Ikulu ya Dar es Salaam Wakizungumza na mtandao huu wa www.matukiodaima.com baadhi ya wafanyabiashara hao ambao wamelazimika kusitisha shughuli za biashara zao eneo hilo ,wamesema kuwa mbali ya ujio huo wa Rais Obama nchini kuwa ni heri kwa Taifa ila kwa upande wao wanapinga hatua ya mgambo kuwanyanyasa kwa kuwatimua eneo hilo ambalo siku zote wamekuwa wakifanya kazi na mbaya zaidi wameamua kuwatimua hadi wauza magazeti . Alisema mfanyabiashara Ally Husein kuwa kutokana na siku ya ziara ya Rais Obama kuwa bado kama takribani siku 12 mbele ni vema uongozi wa jiji na mkoa wa Dar es Salaam ukatumia busara zaidi kwa kuwaacha kwa siku hata 7 mbele ama tano ili waendelee na biashara kwa ajili ya kujitafutia mahitaji yao ya kila siku kuliko kuwazuia kuanzia leo . "Kweli ujio huu wa Rais Obama unatutesa sana sisi walalahoi ambao tunategemea kuendesha maisha yetu kwa kuwepo hapa Posta kwa kufanyabiashara za kuuza magazeti na vocha.....Serikali ya mkoa wa Dar es Salaam tunaomba ilitazame kwa undani zaidi suala hili la kutulaza njaa kwa siku zote 12 bila kufanya shughuli" Hata hivyo alisema kuwa idadi kubwa ya wafanyabiashara eneo hilo wamekuwa wakiendesha biashara zao kwa kupitia mikopo hivyo kuzuiwa kwa muda wote huo kutawaharibia mwelekeo wa kimaisha . Hivyo alishauri serikali kuwa katika maandalizi ya ujio wa Rais Obama nchini bado kutumia njia nzuri ya kuweka jiji safi pasipo kuwaumiza wananchi wenye kipato cha chini wanaofanya shughuli zao katika eneo hilo. "Hivi kama siku zote tumekuwa tukiuza magazeti katika eneo hilo na hakukuwa na uchafuzi wowote wa mazingira leo serikali inatuondoa eneo hili na kutuona kama ni uchafu ....kweli katika hili ni kutunyanyasa wanyonge " KWA UDHAMINI WA SHABIBY BUS LINE NI USAFIRI WA UHAKIKA NA SALAMA KABISA NA HOPE SERVICE STATION IRINGA
|