KAMA ilivyo ada elimu bora hutolewa katika mazingira bora yenye kiwango kizuri kisicho na kasoro ila iwapo eneo la utoaji huduma likawa katika hali ya ubabaishaji ni wazi huduma itakayotolewa pia ni ya kibabaishaji.
Awali ya yote nitumie nafasi hii adimu kuwapongeza wazalendo wote walioamua kuwekeza katika elimu hasa ya vyuo vya Hotel na utalii mkoani Iringa amani mnapaswa kupongezwa kwa kuendeleza jitihada za serikali katika ukuzaji wa utalii katika mikoa ya nyanda za juu kusini nasema hongereni sana.
Mbali ya pongezi hizo kwa wale walioamua kuanzisha vyuo ila bado nitaendelea kuweka ukweli hapa juu ya vyuo tunavyovitaka kwa ajili ya utoaji wa elimu bora hasa tukizingatia kuwa walendwa wa vyuo hivyo ni watoto wetu ambao wamevutiwa kuingia katika tasnia ya Hotel na utalii hivyo mategemeo yao ni kuja kupata elimu bora itakayomuwezesha kupata ajira tena si ajira inayotokana na mkuu wa chuo ama mwalimu kuhonga kwa mmiliki wa Hotel ama afisa husika ili mwanafunzi wako apate nafasi ya kazi hapa tutakuwa tunajidanganya na kuwatumia watoto wetu kama kitega uchumi na huo ni ufisadi mbaya unaopaswa kukemewa.
Ni matumaini vyuo hivi viendeshwe kwa misingi na taratibu za VETA kama wasimamizi wakuu wa vyuo hivyo na mamlaka zote zinazohusika na si vinginevyo.
Kama hivyo ndivyo hebu tujiulize sasa katika mkoa wa Iringa pekee una vyuo zaidi ya 6 vinavyojitangaza eti kuwa ni vyuo vya Hotel na utalii ambavyo vimeendelea kutafuna fedha za watoto wa waokota matunda ( masikini) lakini vyuo vilivyo vingi kwa mujibu wa uchunguzi wa mtandao huu wa www.matukiodaima.com na www.francisgodwin.blogspot.com ni vyuo feki ambavyo vimeshindwa kabisa kukaribia sifa za kuitwa chuo na kupewa barua ya kuruhusiwa kuendeshwa ama usajili ila kila chuo ukiuliza eti unaambiwa kina usajili wa VETA hii ni aibu kubwa .
Cha kushangaza vyuo ambavyo sifa zake zinaendana na zile zinazohitajika na VETA kama wasimamizi wakuu wa vyuo hivyo ndivyo VETA kanda ya nyanda za juu chini ya mkurugenzi wake mama angu Monica Mbele ndivyo vinavyotangazwa katika vyombo vya habari kuwa havina sifa .
Sina shaka na uamuzi wa mkurugenzi wa kanda wa VETA Bi Monica Mbele wa kuvitangaza vyuo hivi kama ni feki kutokana na kutotimiza sifa kama yeye anavyosema ila ni wasiwasi na utendaji kazi wake ama wasaidizi wake ambao binafsi sina hakika kama maamuzi yao wamekuwa wakiyafanyia kazi kwa maana ya kutembelea chuo kimoja hadi cha mwisho na kuangalia ni kipi chenye sifa ya kuitwa chuo na kipi kinapaswa kuitwa kijiwe cha wahuni wachache kuwaibia watanzania kwa kupokea ada za kutoa elimu wakati si sehemu ya kutolea elimu hiyo ya chuo cha Hotel na utalii.
Ushauri katika hili Bi Monica Mbele unapaswa kujisahahisha kama ni wewe mwenyewe umetenda haya ya kuvifunga baadhi ya vyuo vyenye sifa na kuziacha vyuo hivi ila kama ni wasaidizi wako walikuletea ripoti hii ya vyuo nikueleze wazi kuwa hao wasaidizi hawakutakii mema na waogope kama ukoma kwani wanataka kukuchafulia sifa yako kubwa ambayo binafsi bila kushurutishwa huwa naamini kama ni mmoja kati ya wanawake wa chuma katika kazi .
Ila pia kwa upande wako kabla ya kuvifunga vyuo hivyo ni vema ungejiridhisha kuliko ilivyo sasa kila mmoja kwa wamiliki hawa wa vyuo anakuchukia wewe kuwa umefanya upendeleo katika hili .
Japo si mtendaji wa VETA ila kidogo nina uelewa juu ya sifa za kuitwa chuo cha Hotel na Utalii sifa ambazo mmiliki anapaswa kuzifuata na hizi ndizo sifa nilizopata kuzitumia katika uchunguzi wangu katika vyuo hivyo na leo kuona ni wazi kuna makosa katika kuvitambua vyuo hivi kuwa ni bora na kushindwa kuvitambua hivi bora kuwa si bora.
1. darasa kubwa
2.viti na meza za kutosha
3.Pratical rooms
4.jiko
5.Restaurant
6.bar
7.Standard ya walimu (CV)
8. Vitabu vya kufundishia
N.K
Hizi ndizo sifa nilizopata kuzitumia katikakufanya utafiti wangu sifa ambazo kwa haraka haraka hata leo tukiondoka mimi na jopo la wanauchunguzi wengine nje ya VETA Iringa kuvizungikia vyuo hivi ambavyo bila woga naviita ni vyuo feki ambavyo wao wamevipasisha kuwa ni vyuo vyenye sifa ukweli hakuna kinachokaribika mfano upande wa CV za walimu, ukubwa wa darasa , Pratical room na sifa nyingine nyingi ni vituko ni kama vyuo vinavyoigiza katika elimu.
Kwa leo nitavitaja vyuo viwili vya awali ambavyo nitaomba uchunguzi wa timu ya VETA Taifa kama utafika kuanzia kwa uchunguzi kama kweli vilipaswa kutangazwa kuwa ni vyuo visivyo na sifa vyuo hivyo ni Ruaha na Delima hebu leo VETA tuweke chini tofauti zetu na wamiliki wa vyuo hivyo na tutende haki katika kugawa sifa za macho ama zile za VETA kama kweli vyuo hivi ni feki ama wale waliotumwa kuvitazama vyuo hivyo walirejesha majibu feki ?hapana siwafundishi kazi ila katika ukweli tusemezane kweli tupu na asiwepo wa kutoa vitisho wala kuchukia kwa kuelezwa ukweli ila narudia tena sina shaka na uelewa wa watendaji kazi wa VETA lakini katika hili mnasafiri katika mtumbwi wa mhongo mnaruhusu mmoja wenu kuendelea kuutafuna mtumbwi huo kabla ya kuvuka bahari .
Sasa nasema sitaki kuona VETA mkifanya kazi kwa kujuana na kuacha kutenda ukweli na sitaki kuona wala kusikia mtu akilalamika kwa mtazamo wangu huu .