Na Francis Godwin Blog MDAU wa maendeleo na mwekezaji katika wilaya ya Iringa vijijini Arif Abri amekuchangia vifaa mbali mbali zikiwemo ,mizinga ya nyuki ya kisasa 20 Tanki la kuhifadhia maji meza 40 za chakula kwa wanafunzi pamoja na saruji mifuko 100 vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya Tsh milioni 13.5 kwa ajili ya kutatua changamoto zinazoikabili Nyerere High School Migoli .
Abri ambae alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya nne ya kidato cha sita yaliyofanyika shuleni leo alitoa ahadi hiyo kufuatia maombi ya wanafunzi na uongozi wa shule hiyo waliyoyatoa wakati wakisoma risala na taarifa ya shule mbele yake .
Katika risala ya wanafunzi wahitimu wa kidato cha sita iliyosomwa na mwanafunzi Ally Godda walimueleza mgeni huyo rasmi kuwa mbali ya shule hiyo kuendelea kuwa na mafanikio makubwa ya kitaalum ila wamekuwa wakikabiliwa ni pamoja na viti na meza ambao umepelekea kupungua kwa ufanisi wa kujisomea kwa wanafunzi pia tatizo la kukatika mara kwa mara kwa umeme ,ukosefu wa meza katika ukumbi wa chakula ambao unapelekea wanafunzi kushindwa kula chakula kwa raha hasa wakati wa mvua ,pamoja na kukosekana kwa jenereta na tanki la kuhifadhia maji .
Aidha walisema kuwa katika shule hiyo kuna ujenzi wa bweni la wavulana limefika hatua za mwisho ila bado halijasakafiwa na hivyo kuomba kusaidia msaada wa saruji ya kumalizia kazi hiyo ili kulifanya bweni hilo kutumika na wanafunzi shuleni hapo.
Hata hivyo katika kuanza kukabiliana na changamoto hizo Abri aliahidi kusaidia maeneo matatu kati ya manne yanayoikabili shule hiyo likiwemo la meza kubwa 40 za chakula ukumbini, saruji mifuko 100 na Tanki la kuhifadhia maji kubwa pamoja na kuwaahidi kuwapa mizinga ya kisasa 20 kwa ajili ya ufugaji nyuki shuleni hapo.
Hata hivyo aliwapongeza wanafunzi wa shule hiyo kwa jitihada kubwa za kujisomea na kuendelea kuipa heshima kubwa shule hiyo katika ufaulu na kuwataka kuongeza jitihada zaidi na kuachana na kufikiria changamoto za shule badala ya kufikiria namna gani watafaulu katika mitihani yao.
Kwa upande wake katibu wa mbunge wa jimbo la Isimani Thom Malenga aliwataka wahitimu hao wa kidato cha sita kuongeza jitihada za kusoma katika muda huu uliobaki kabla ya kufanya mtihani wao .
" Nawaombeni sana wanafunzi mnaohitimu leo hapa tumieni vizuri muda uliobaki kwa kujisomea zaidi ilikuendelea kuipa heshima shule hii na watanzania waendelee kuiona Nyerere High Shool kama shule bora nchini"
Awali mkuu wa shule hiyo Laurent Manga mbali ya kumpongeza Abri kwa kujitolea kuisaidia zaidi shule hiyo na pia alimpongeza mbunge wa jimbo hilo Wiliam Lukuvi na kamanda wa UVCCM mkoa wa Iringa Salim Asas Paroko Salvatore Riccerri na mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo ni miongoni mwa wadau wakubwa waliofanikisha maendeleo ya shule hiyo.
Aidha alisema kuwa shule hiyo iliyojengwa mwaka 2003 kwa ufadhili wa Paroko wa parokia ya Migoli Padre Salvatore Riccerri na kufunguliwa na rais wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa mwaka 2005 imeendelea kuwa miongoni mwa shule bora nchini na kufanya idadi ya wanafunzi kuendelea kuongezeka mwaka baada ya mwaka na kuwa hadi sasa shule ina jumla ya wanafunzi 940 wakiwemo wasichana 361 na wavulana 579 kwa kidato cha kwanza hadi cha sita na kuwa jumla ya wanafunzi 68 ndio wanahitimu mwaka huu.
|