Deo Filikunjombe
•Hati ya Muungano sio document pekee inayo-justify Muungano. Baada ya hati kusainiwa ilitakiwa ilidhinishwe na pande zote mbili.
Upande wa Tanganyika, bunge lilikutana Jumamosi ya tarehe 25-Apr-1964 na kuidhinisha. Ila upande wa Zanzibar hakuna ushahidi kwamba walipata kuidhinisha.
•Tatizo la pili ambalo lilimkasirisha sana Karume ni pale alipogundua kwamba hati ilikuwa inampa Nyerere uwezo wa kubadili katiba ya Muungano kwa kupitia “presidential decree” muda wowote akitaka bila kuwa na haja ya kumshirikisha Karume.
•Tatizo lilitokana na kwamba mkataba uliandaliwa na mwanasheria wa Nyerere (Attorney General) mzungu anayeitwa Roland Brown. Wakati kwa upande wa Zanzibar, mwanasheria wake mkuu, Wolfango Dourado alikuwa amepewa likizo ya lazima kwenda Uganda. Hivyo Karume hakupata msaada wa kisheria wakati anasaini.