Bw Geofrey Mungai kushoto akiwa na watoto yatima wa kituo cha Tosamaganga baada ya kuwakabidhi msaada wa chakula.
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya ujenzi wa barabara nchini ya GNSM Contractors Co. Ltd Bw Geofrey Mungaikushoto akila chakula na watoto yatima wa kituo cha DBL mkimbizi sanjari na mganga Oscar Gabone kulia.
...............................................................
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya ujenzi wa barabara nchini ya GNSM Contractors Co. Ltd Bw Geofrey Mungai ametoa msaada wa chakula kwa watoto yatima wa kituo cha
Daily Bread Life Tanzania (DBL) mkimbizi mjini Iringa.
Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo wa chakula Bw Mungai alisema kuwa imekuwa ni kawaida ya kampuni yake kuwakumbuka watoto hao yatima wa kituo hicho na vituo vingine kama njia ya kuikumbusha jamii kuelekeza upendo wao kwa watoto hao yatima.
Hata hivyo alisema kuwa jamii ya nchini inapaswa kubadilika kwa kuelekeza michango yao kwa watoto yatima ambao wanaishi kwa misaada ya watanzania baada kupoteza wazazi wao .
Kwani alisema kuendelea kuwasaidia watoto hao ni kuwasogezea faraja ya pekee ambayo watoto hao wanahitaji kutoka kwa jamii inayowazunguka badala ya kuwasusa .
Aidha alisema kuwa yeye kama mmoja kati ya makandarasi mkoa wa Iringa anaendelea kufanya mazungumzo na wenzake ili kuweka mpango wa kuendelea kutembelea vituo vya yatima kila mwaka kwa ajili ya kuwasaidia misaada mbali mbali.
Huku akiishauri serikali kuangalia uwezekano kupitia ofisi za maendeleo ya
Jamii, Jinsia na Watoto kuweka utaratibu wa kuwakumbuka watoto waliopo katika vituo vya yatima kwa kuwapa mahitaji yao ya kila siku .
Jamii, Jinsia na Watoto kuweka utaratibu wa kuwakumbuka watoto waliopo katika vituo vya yatima kwa kuwapa mahitaji yao ya kila siku .
Bw Mungai alipongeza jitihada kubwa zinazoendelea kufanywa na uongozi wa kituo hicho cha DBL Mkimbizi chini ya mchungaji Mpeli Mwaisumbi na kufanya kituo hicho kuwa miongoni mwa vituo vinavyoongoza kwa kuwa na watoto wenye malezi bora ya kiafya na elimu mkoani Iringa
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho mchungaji Mpeli Mwaisumbi mbali ya kumpongeza Mungai kwa kuendelea kusaidia watoto hao bado alisema wengine ambao wamepata kufika kusaidia watoto hao ni pamoja na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu, taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (TAKUKURU) mkoa wa Iringa ,mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Iringa , mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Rita Kabati (CCM)
Mchungaji Mpeli alisema kuwa Mungai wadau hao wamekuwa ni msaada mkubwa wa kituo hicho na kuwa karibu miaka yote wamekuwa wakifika kusaidia watoto hao misaada mbali mbali ikiwemo ya elimu .
Alisema kuwa kituo hicho kinafanya kazi chini ya shirika lisilo la kiserikali ya Daily Bread Life Tanzania lililosajiliwa kwa usajili 12903 chini ya wizara ya mambo ya ndani ya nchi pia kituo kimesajiliwa na ustawi wa jamii kwa kupewa usajili wa makao ya watoto namba 00049995.
Hata hivyo alisema kuwa kituo kilianza kupokea watoto 14 mwaka 2004 na sasa kuna watoto 37 waliopo kituoni hapo na kuwa toka kituo kianzishwe jumla ya watoto 51 wamelelewa hapo
Alisema kutokana na misaada wa wadau mbali mbali kituo kimeendelea kupata mafanikio makubwa kama kuwa na shamba ,basi moja ,mradi wa cherehani pia kuanza mchakato wa kukamilisha shule ya sekondari ambayo inajengwa umbali wa kilomita 6 kutoka mjini Iringa kwa lengo kuwawezesha watoto hao kupata elimu ya sekondari.
Pia alisema changamoto kubwa katika uendeshaji wa kituo hicho ni michango mingi katika shule za msingi ambako watoto hao wanasoma ,kukosa ruzuku toka serikalini na changamoto nyingine nyingi.
Mchungaji Mpeli aliwaomba watanzania na wadau mbali mbali pale walipo iwapo wanahitaji kusaidia kituo hicho kutuma michango yao kupitia akaunti namba Benki ya Exim ni 5435526007 Daily Bread Life Childreans home ,ama kwa njia ya M-PESA 0754362536