Quantcast
Channel: Francis Godwin ::Mzee wa matukio daima::
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2596

VETA IRINGA YAVIFUNGIA VYUO VYA MFUKONI .......

$
0
0

Mhitimu  wa ukweli  wa VETA Iringa Perida Erasto akionyesha  cheti kinachotambulika


 ...............................................................................................................................................
Na Eliasa Ally, Iringa
Mkurugenzi wa VETA wa Kanda ya Nyanda za Juu, Bi, Monica Mbelle amevifungia
Vyuo wa Utalii zaidi ya vitatu mkoani Iringa ili visiendelee kuendesha mafunzo ya Utalii na kuwaibia wazazi ada na gharama zingine kutokana vyuo hivyo kushindwa kukidhi vigezo vilivyowekwa na VETA na kuendesha mafunzo hayo bila kuwa na usajiri na kuchukua wanafunzi ambao wamekuwa wakilipishwa wanafunzi wa vyuo vya Utalii ada kubwa bila kuwa na matumaini ya kupata ajira katika maisha yao.

 Akizungumza jana na ofisini kwake,Mkurugenzi wa VETA wa Nyanda za Juu Kusini, Bi. Monica Mbelle alisema kuwa maamuzi ya kuvifunga vyuo hivyo vya Utalii, umefanyika baada ya yeye mwenyewe kuvitembelea na kuthibitisha kuwepo kwa mapungufu makubwa na mengi ambapo vyuo hivyo wanafanya makosa kuanza kuwapokea wanafunzi kabla VETA haijawaruhusu baada ya vyuo husika kukidhi vigezo sitahiki vinavyotakiwa na VETA.

Bi. Monica Mbelle alivitaja Vyuo vya Utalii ambavyo amevifungia na kuvitaka viache kuwapokea wanafunzi na kuendesha mafunzo yao kuwa ni pamoja na chuo cha Utalii ya Ruaha Utalii College, Capricon College na Delima Hotel and Tourism School vyote vipo mjini Iringa ambavyo amesema kuwa kutokana na kukosa vigezo havitaruhusiwa kuendesha mafunzo na kuwa ametoa taarifa polisi, ofisi za Mkurugenzi Manispaa ya Iringa pamoja na ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Iringa ili kuwakamata mara moja endapo wataendelea kuendesha mafunzo na kuwalaghai wanafunzi wao.

Aidha alisema kuwa ameshangazwa na wamiliki wa vyuo hivyo vya Ruaha Utalii College, Delima Hotel and Tourism School na Capricon College kwa kutoa vyeti vya Diploma na Satefiketi vilivyo feki wakati masomo ambayo wamekuwa wakiyaendesha hayafuati mitaala yoyote ambayo imewekwa na VETA na ameonya kuwa endapo wapo wengine wenye mipango kama hiyo anawaasa wafuate sheria na taratibu zilizowekwa na serikali.


Aliongeza kuwa ujenzi wa vyuo vya ufundi na utalii ambavyo vinatakiwa kutoa elimu hiyo awali ya yote hutakiwa kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wa vyuo ambao ni VETA ambako kunakitengo maalumu na baadaye vyuo hivyo endapo vitakuwa vimekithi vigezo hutakiwa kupatiwa mitaala ya kufundishia na VETA na siyo kujifanyia wanavyotaka.

Alisema kuwa hata hivyo ofisi yake itavitambulisha vyuo ambavyo vimekithi vigezo vyote na vinatoa elimu ya ufundi na utalii ambavyo tayari VETA imeviruhusu kuendesha masomo yake kuondoa utata unaowakumba wanafunzi na wazazi kwa sasa kwa kuingia gharama zisizo na msingi ambapo pia amewataka wazazi kufika ofisi za mkoa za VETA kujirithisha kama vyuo vinavyojitangaza tayari vimesajiliwa.

Mwisho;

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2596

Trending Articles