Quantcast
Channel: Francis Godwin ::Mzee wa matukio daima::
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2596

SIPENDI KUONA MVUTANO HUU KILOLO, SASA NI ZAMU YA DC NA MADIWANI YEYE APIGA MARUFUKU MAGARI KULALA MJINI WAO WAJIBU WATAKA AWAPANGIE MAJUKUMU PIA

$
0
0
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilolo Bw Joseph Muhumba
                            Mkuu wa  wilaya ya Kilolo Bw Gerald Guninita
....................................................................................................

KAMA ni mvutano basi huu umezidi  wakati mkuu wa  wilaya ya  Kilolo   mkoani Iringa  Gerald Guninita  akipiga marufuku magari  yote ya Halmashauri  ya wilaya ya Kilolo  kulala nje ya makao makuu ya wilaya  hiyo na kuagiza mkuu wa polisi  wilaya ya Kilolo kuanzia  sasa kuanza kuyakamata magari hayo.

Madiwani wamjibu wasema hana mamlaka ya  kupiga marufuku hiyo kwani  watumishi wa Halmashauri hiyo hawawajibiki kwake  na kama anataka  wawajibike kwake basi awapangie majukumu ya kila  siku.


Pia akishukia  chama cha  wafanyakazi katika  wilaya ya Kilolo kwa kukimbilia  kuwatoa  taarifa katika  vyombo vya habari na kuandika barua   .


Mkuu  huyo  wa wilaya  amesema kuwa  hatua ya  chama cha  wafanyakazi  wilaya ya  Kilolo kukimbilia katika vyombo  vya habari na kusambaza barua  maeneo mbali mbali kulaani  hatua yeye kama mkuu wa wilaya kuwachukulia hatua baadhi ya   watumishi  wa wilaya  hiyo alisema ni utovu mkubwa wa nidham kwani ilipaswa wao kama  waajiriwa wa Halmashauri ya Kilolo kufikisha madai yao kwa mkurugenzi na si vinginevyo.


Hata  hivyo alidai kuwa suala la yeye kutishiwa ameliacha mikononi mwa  vyombo vya ulinzi na usalama ili kufuatilia jambo hilo hata kama yeye ameamua mkusamehe watu hao

Adai  ametumiwa ujumbe wa vitisho  na tayari taarifa amezitoa  polisi na mkononi ana RB ya  taarifa  hiyo ambayo ametumiwa kuhusiana na kuwabana  watumishi  wabadhilifu katika Halmashauri ya  wilaya  ya Kilolo.


Mkuu  huyo wa wilaya  ametoa agizo hilo mchana  wa leo  wakati  akitoa maagizo ya  serikali katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya  wilaya  hiyo.


Alisema kuwa ili kukomesha matumizi mabaya ya matumizi ya  fedha  za Halmashauri kwa kupelekea  watumishi kulala mjini Iringa jambo ambalo ni kinyume na utaratibu.


“Namwagiza  OCD kupitia  kauli mbiu ya matokeo makubwa sasa yanawezekana  kuwakamata  madereva  watakao kutwa mjini  na magari ya  umma”



Kwa upande  wake mwenyekiti wa Halmashauri ya  wilaya ya Kilolo Joseph Muhumba akizungumza huku akipigiwa makofi na watumishi na madiwani katika kikao  hicho alisema kuwa kuna haja ya  mkuu  huyo wa wilaya na viongozi  wengine  kuweza kupeana utaratibu  wa  kuongoza serikali na kuwa kikao kama hicho cha baraza la madiwani ni kikao ambacho kipo kisheria  hivyo anapopewa nafasi ya kutoa maagizo ya serikali asigeuze ni  sehemu ya kutoa hotuba.



Hivyo alisema kuna  haja ya kuelekezana  juu ya  uendeshaji wa serikali za mitaa na kuwa  Kilolo  si  wilaya  changa  kama ambavyo mkuu  huyo wa wilaya anafikiri na kuwa imefika hapo kutokana na ushirikiano  uliopo kati ya  watumishi na viongozi na kuwa anashangazwa  kuona mkuu wa wilaya anasema kamati ya ulinzi na usalama imesema  wakati yeye kama mwenyekiti wa Halmashauri hajui chochote.



Asema kama kila mmoja atakuwa na hali  ya vitisho kwa  watumishi  kazi haitakwenda katika  Halmashauri  hiyo hivyo kuna haja ya mkuu  wa wilaya  kufanya kazi kwa ushirikiano na  watumishi wa Halmashauri  hiyo ya  wilaya na kuwa kabla yake wapo  wakuu wa wilaya ambao wamepita  ila  wamefanya kazi kwa ushirikiano mkubwa .

Ataka  kikao  kijacho  kiwe na mtiririko mzuri na kama kuna maagizo ya  serikali basi mkuu wa wilaya  kutumia muda wa dakika  5  kutoa badala ya  kurefusha  kikao hicho .

Mwenyekiti  huyo alisema  kuwa hapingi kauli ya mkuu wa wilaya  kuwataka  watumishi kutokuwa na nidham ya uoga katika  kuwatumikia  wananchi  wa Kilolo 

Huku  baadhi ya  watumishi wa Halmashauri hiyo wakidai kuwa mkuu  wa wilaya amekosea kupiga marufuku  hiyo kwani wao  wanawajibika kwa mkurugenzi na si kwa DAS wala ofisi ya mkuu  wa wilaya  . 

Hata  hivyo  mwenyekiti  huyo aliwataka  watumishi  kuwa wavumilivu ya  yote  wanayotendewa  ila wasivunjike  moyo na kuwataka  kuendelea kufanya kazi kwa moyo .

Alisema kuwa jambo kubwa kwa kiongozi ni kuhakikisha anafanyakazi zake  kwa kushirikiano na watu  hivyo kama kiongozi hatakuwa na ushirikiano basi hakuna litakalofanyika.

Kuhusu  uadilifu wa viongozi mwenyekiti Muhumba  aliwataka kila mmoja kufanya kazi kwa kujituma zaidi.

Safu  hii ya Sipendi kuona baada ya  kushuhudia mvutano huu kati ya watumishi wa Halmashauri ya Kilolo pamoja na madiwani dhidi ya mkuu wa wilaya  ,unapatwa na maswali mawili matatu ya kujiuliza  hivi hadi mkuu wa wilaya anapingwa hivyo ni kwamba  hajui  wajibu wake? ama watumishi na madiwani hawajui  wajibu wao? pia najiuliza watumishi wa Halmashauri wanawajibika kwa mkuu wa wilaya ama kwa mkurugenzi mtendaji wa wilaya ? kama wanawajibika kwa mkurugenzi ni nani yupo  sahihi kupiga marufuku magari  kulala mjini na je? kwa jografia ya  wilaya ya Kilolo hili litatekelezeka? 

Swali  la mwisho mvutano kama huu  ni nani atakayeumia? 
SASA  SIKIA NASEMA  SIPENDI KUONA MVUTANO HUU UKIENDELEA KILOLO

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2596

Trending Articles