=============================================================================
Na Gustav Chahe, Iringa
MBUNGE wa viti maalum Chiku Abwao (CHADEMA)Pichani , amesema wanawake nchini wamegeuzwa kuwa chambo ya watu wabinafsi wasiopenda maendeleo ya watu wengine.
Abwao ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akiunda kikundi cha wanawake katika Mtaa wa Kinegamgosi Kata ya Ruaha katika Manispaa ya Iringa ili kuwasaidia wanawake katika kujitegemea.
Akitoa elimu ya ujasiriamali kwa wanawake hao amesema amefikia maamuzi hayo baada ya kuona akina mama wengi wanakuwa wanyonge katika maendeleo na kutumia kama chambo kwa watu waroho na wabinafsi nyakati za uchaguzi.
“Akina mama wengi tumejifunga na kukata tama lakini tikisaidia na kupiga hatua mbele tunaweza kujifungua. Wanawake wengi ndiyo wapiga kura waaminifu lakini tunatumika vibaya na watu, tukishawawezesha kuingia madarakani wanakuwa hawana muda na sisi tena. Tulikatae hilo” amesema.
Alisema umasikini katika nchi hii si wa bahati mbaya bali unatengenezwa na watu ili waendelee kuwepo madarakani kwa kugawa kofia, kanga na fulana wakati wa uchaguzi ili waonekane wa maana zaidi kuliko wengune.
Pia amesema kuunda vikundi vya akina mama na kuviwezesha ni utekelezaji wa mipango ya Chadema ili kuwatengenezea mazingira mazuri ya maisha pamoja na uendeshaji wa familia zao.
“Umasikini wetu si wa bahati mbaya kwa chama cha Mapindizi (CCM) bali ni makusudi yao. Wanatengeneza mazingira ya umasikini ili wapate nafasi ya kuwarubuni watu. Tumekuwa kama kuku wa kienyeji” amesma.
Alisema ili kuondokana na umasikini ni lazima kuwa na dhamira ya kweli kuukataa ikiwa ni pamoja na kuwakata wanaosababisha wengine kuishi kama watumwa.
Mwenyekiti wa kikundi hicho Judith Muhali amesema umefika wakati wa kuachana na watu wanaotumia majukwaa wa kati wa uchaguzi kwa kuwanunua wananchi ama kwa pesa ama kwa kuwagawia vitenge au kofia kwa kuwa hivyo havileti maendeleo ba badala yake amewataka akina mama kuungana na kufanya mambo ya maendeleo kwa kuwapima viongozi wanaowajali.
Amesema Abwao amefika wakati mzuri ambao wanawake wanahitaji kukombolewa na wimbi la umasikini ambalo lilionekana kama halina dawa.
Hata hivyo amewataka akina mama wenzake kuwa waaminifu katika mikopo ili kuweza kusadia mikakati ya kujikwamua inasonga mbele.