mke wa Rais salma Kikwete akihutubia
..................................................................................................................
Na Magreth Kinabo – Maelezo
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amewataka Watanzania kuongeza juhudi za kuzuia maambukizi ya Virusi
Vya Ukimwi(VVU) kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ili katika Tanzania iweze kuwa na kizazi kisichokuwa na VVU na ugonjwa wa Ukimwi.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) wakati akifungua mkutano wa kitaifa wa wadau wa kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Aidha mama Kikwete aliwataka Watanzania kuchangia sh. 100 katika kupambana na tatizo kwa mchango utawapa nguvu wadau wengine kuwaunga mkono.
Aliwataka wadau wamaendeleo kuendele kuunga mkno katika juhudi za kuondokana na tatizo hilo.
“ Lazima juhudi za makusudi zifanyike bila kuchoka kwa maeneo yote Serikali, NGO’s, taasisi za dini mashirika ya kiraia na watu binafsi .
Hii itasaidia kunusuru kizazi chetu na kuwa na nguvu kazi iliyobora, kizazi kisichokuwa na maambukizi na VVU na Ukimwi,” alisema Mama Kikwete huku akisisitiza Tanzania bila Ukimwi inawezekana.
Aliongeza kuwa mikakati imara na endelevu ni lazima iwepo kama vile kutoa huduma za kuzuia maambukizi ya VVU na Ukimwi kwa kushirikisha jamii na kutoa tiba kikamilifu zinaweza kupunguza maambukizi hayo.
Alisema asilimia 98 ya wakina mama wajawazito wanahudhuria kiliniki angalau mara moja na asilimia 43 mara nne wakati wa ujauzito kati ya hao, asilimia 81 wanapimwa VVU.
Aliwataka wakina mama wajazito kuhudhuria kiliniki wakati wa ujauzito kuanzia siku ya kwanza hadi watakapoajifungua ili idadi ya wanahudhuria kiliniki iweze kufikia asilimia 100.
Naye Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid alisema hivi sasa Tanzania imefanikiwa kupunguza maambukizi hayo kwa asilimia 15 mwaka 2012 kutoka asilimia 19 mwaka 2011 na lengo ni kufikia asilimia 5 ifikapo mwaka 2015.
Alisema asilimia 90 ya wakina mama wajawazito wamepimwa VVU kati yao asilimia 64 wamegundulika wanaishi na VVU , pia asilimia 55 ya watoto wanapatiwa dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo.(ARV’s).
Kaimu Mkurugenzi wa Kinga kutoka wizara hiyo , Dk .Neema Rusibamayilla alisema alisema awamu ya pili ya kupambana na tatizo hilo itaanza Januari mwaka huu katika mikoa mingine 16.
Mratibu wa huduma hiyo kutoka Malawi, Dk. Michael Eliya alisema ni muhimu kuweza katika utoaji wa huduma, kuboresha miundombinu ,ikiwemo rasilimali fedha na watu katika kufanikisha malengo hayo.