Mwandishi ,Dominic Joseph Maro wa matukiodaima.comTanga
........................................................................
HALMASHAURI ya jiji la Tanga inatarajia kutumia kiasi cha sh, 4.5 bilioni ktk kipindi cha mwaka wa fedha wa 2014/15 kwaajili ya kuendesha mradi wa kupeleka maji safi ya bomba ktk vijijini 10.
Meya wa jiji la Tanga Omari Guledi amesema kuwa ktk kipindi hicho Halmashauli ya jiji la Tanga imepanga kufikisha maji safi ya bomba ktk vijiji 10 vilivyo ktk upande wa kaskazini na magharibi ya wilaya ya Tanga.
Amevitaja vijiji hivyo vitakavyonufaika na mradi huo kuwa ni pamoja na Chongoleani, Ndaoya, Kibafuta, Mleni, Mpirani, Marungu, Geza, Mapojoni Mwarongo na Kirare.
Guledi amesema kuwa mradi huo wa kupeleka maji ktk vijiji hivyo unakuja kufuatia jiji la Tanga kujitosheleza kwa usambazaji maji kwa wananchi wake wa mjini kwa kiwango kikubwa ambapo ametanabaisha kuwa kwa sasa nguvu zinaelekezwa kwa wananchi walio vijijini