MTOTO ZAINA HEMED AMBAYE NI WADARASA LA SABA KATIK SHULE YA MSINGI BUGURUNI VIZIWI AKIZUNGUMZA KWA NIABA YA WATOTO WOTE KATKA MKUTANO HUO ALIKUWA NA MKALIMAN AMBAYE KWENYE PICHA HAONEKANI
......................................................................................................................
Mwandishi Kenneth John wa matukiodaima.com ,Dar
......................................................................................................................
Mwandishi Kenneth John wa matukiodaima.com ,Dar
Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na mfuko wa maendeleo ya watoto wa umoja wa mataifa (UNICEF), ujumbe wa umoja wa ulaya (EU) Tanzania ,Shirika la save chidren pamoja na shirika la Plan International (PLAN) leo wamezindua mpango wa pamoja wa kukomesha ukatili dhidi ya watoto Tanzania.
Akizungumza katika uzinduzi huo waziri wa afya na ustawi wa jamii Dkt Seif Rashid alisema kuwa kila hamashauri zinawajibu wa kusajili watoto wote ambao wanaishi katika mazingira hatarishi , pamoja na kutoa taarifa za matokeo yote ambayo yanaenda sambamba na kusababisha athari kwa watoto.
Pia aliongeza kuwa kunahitajika kuwa na maafisa jamii ambao wanauwezo wa kuhakikisha wanampa ushirikiano wa kutosha mtoto pamoja na kuzungumza na mtoto kwa uwazi zaidi.
Mradi huo unalengo la kusaidia uanzishwaji wa mifumo ya kumlinda mtoto ili kuweza kudhibiti na kukabiliana na kila aina ya ukatili dhidi ya watoto , hasa watoto wa kike na hatua hiyo itasaidia utekelezaji wa mipango iliyopo ya kupambana na ajira kwa watoto pamoja na kuanzisha shule salama Zanzibar.
Aidha mradi huo pia unalengo la kusaidia watoto na familia zao,kuimarisha ulinzi katika mazingira ya jamii na shule salama, pia mradi umelenga kufikia malengo ya muda mrefu,kuwa na mfumo wenye jukumu la mstari wa mbele pamoja na kuwa na mfumo endelevu kwa ajili ya kutambua, kuzuia , kukabiliana na kusaidia watoto kwa kuujumuisha katika mfumo wa mamlaka za serikali za mitaa na taratibu za jamii kwa kutumia ,matokeo yatakayopatikana kuhamasisha mgao wa mara kwa mara wa bajeti kwaajili ya ulinzi wa mtoto katika ngazi ya wilaya na katika ngazi ya kitaifa.
Na kwa upande wa mwakilishi wa UNICEF nchini Dkt Jama Gulaid alisema kuwa ushirikiano huo ni hatua muhimu ya kuimarisha mifumo ya ulinzi wa watoto ilikukabiliana na ukatili dhidi ya watoto nchini,pamoja na kutoa fursa ya kuimarisha muungano kwaajili ya maendeleo ya watoto katika ya Umoja wa Ulaya,
Pamoja na hayo yote kwa mujibu wa ripoti ya utafiti wa ukatili dhidi ya watoto Tanzania uliotolewa na serikali ya na UNICEF mwaka 2011 ulidhihirisha kwamba msichana mmoja kati ya watatu na mvulana mmoja kati ya saba nchini Tanzania hukubwa na manyanyaso ya kijinsia kabla ya kufikisha umri wa miaka kumi nane,Pia tafiti ilibaini kuwa viwango vya unyanyasaji wa kimwili viko juu sana kwani karibu wasichana na wavulana watatu kati ya wanne wamepigwa ngumi, kuchapwa au kupigwa mateke wakati wa utoto wao, huku robo ya watoto wote wamefanyiwa ukatili wa kihisia,na ripoti hiyo ilionyesha kuwa watoto wengi hawashtaki matukio hayo,wachache hutafuta huduma stahiki na wachache zaidi hupatiwa huduma ya matibabu au msaada.