UTAPELI wa kutumia majina ya viongozi wa ngazi za juu serikali umeendelea kuchukua kasi hapa nchini baada ya mwanamke mmoja mfanyabiashara mjini Iringa kuponea katika tundu la sindano kutapeliwa kiasi cha Tsh 800,000 na mtu aliyejifanya ni dereva wa waziri wan chi ofisi ya waziri mkuu sera na uratibu wa bunge Wiliam Lukuvi .
Akizungumza na mtandao huu wa matukiodaima.com mfanyabiashara Janeth Mbalazi amesema kuwa tukio hilo limetokea asubuhi ya leo .
Amesema awali mtu huyo ambae alijitambulisha kwa jina moja la Mlelwa alifika dukani hapo majira ya saa 5 asubuhi akiulizia huduma ya M-Pesa na baada ya kuelezwa kuwa huduma hiyo ipo ghafla alianza kujieleza kuwa yeye ni dereva wa mbunge wa jimbo la Isimani Wiliam Lukuvi ametokea Isimani ambapo gari limeharibika hivyo simu yake ilipotea na kuomba namba ya mwanamke huyo ili aweze kuituma kwa boss wake (Lukuvi) ili atumiwe pesa.
“ Nilikubali kumpa namba yangu na hapo hapo aliituma kwa boss wake na kuniuliza jina nikamwambia naitwa Jeneth na yeye akamueleza boss wake kuwa mimi naitwa Janeth ….baada ya hapo aliniambia kuwa atatumiwa kiasi cha Tsh 260,000 na kuondoka eneo hilo”alisema Janeth
Kuwa baada ya dakika kama 30 ilipigwa simu kwa namba ngeni na kueleza kuwa amepata namba hiyo kwa dereva wake na hivyo atatuma kiasi cha Tsh 400,000 si muda mrefu kwa madai ni fedha kwa ajili ya dereva huyo.
“ Nilimuuliza kuwa kwanini atume 400,000 wakati dereva wake amesema anataka kiasi cha Tsh 260,000 alidai kuwa kuna tatizo jingine limeongezeka na kuwa yeye kwa sasa yupo katika kikao akitoka atatuma ..japo baada ya muda dereva wake alipiga kuwa uliyekuwa ukiongea nae ni waziri Lukuvi “
Hata hivyo haukupita muda kama dakika 10 hivi akapiga simu Mlelwa ambae anadai ni dereva wa Lukuvi na kuuliza kama boss wake amepiga simu na baada ya kujibiwa kuwa amepiga bado alimtaka mwamamke huyo kumpigia simu Lukuvi ili kumueleza kuwa aongeze pesa atume Tsh 800,000 jambo ambalo lilikuwa zito kwake kumpigia Lukuvi isipo kuwa alimtaka dereva huyo feki ndie afanye kazi hiyo ya kupiga simu.
“ Sikuweza kukubali kumpigia simu nilimtaka apige simu mwenyewe sio mimi ila nilipojaribu kutuma fedha zaidi ya salio langu ili kujua jina linalotumiwa katika namba 0767 946751 hiyo ya mtu anayejiita ni Lukuvi kweli jina lilikuja Wiliam Lukuvi “
Pia alisema kuwa tapeli huyo anajiita ni dereva wa Lukuvi namba yake ni hii 0768990282 na kuwa baada ya muda alipiga simu na kuuliza kama ametuma pesa ila nilipomueleza kuwa hajatuma alisema anaomba nimtumie yangu kiasi cha Tsh 300,000 kwa madai kuwa amepata kifaa eneo la Isimani hivyo anataka kwenda kufuata na pindi Lukuvi akituma pesa atakata pesa yake na kumrushia Tsh 500,000 itakayobaki kati ya 800,000 aliziomba kutumiwa na Lukuvi.
“ Ujue nilijiuliza hivi kweli Lukuvi anaweza kutumia njia hii kutaka pesa wakati yeye ni kiongozi mkubwa hapa nchini na pili Lukuvi Iringa ni nyumbani kwake iweje dereva aje katika maduka ya M-Pesa na asiende kwa katibu wake ama kwa viongozi wenzake hapa mkoani “
Pona ya dada huyo ni kutaka kujiuliza kwa mwandishi wa mtandao huu kama ananamba ya Lukuvi na kusimulia mkasa huo na ndipo sura ya utapeli ilipoonekana na kuweka mtego kuwa aje achukue Tsh 250,000 ambazo zipo kwanza huku polisi wakiwa wameandaliwa tayari kwa ajili ya kumnasa tapeli huyo ambaye hata hivyo hakuweza kutokea zaidi ya kupiga simu na kuomba kutumiwa kwa M-Pesa jambo mwanamke huyo hakufanya hivyo. Mwandishi wa mtandao huu alijaribu kumpigia tapeli huyo bila mafanikio ila baada ya kufanya uchunguzi kupitia namba yake ilionyesha kuwa tapeli huyo anaitwa Faustin Mlelwa .
Akizunzumza kwa njia ya simu waziri Lukuvi baada ya kupigiwa na mtandao huu alidai kuwa si kweli kama kuna dereva wake Iringa kwa leo na kuwa yeye yupo Dar es salaam na kuwa mtu huyo ni tapeli ambae amekuwa akifanya hivyo katika maeneo mbali mbali na kusema kuwa kwa upande wake hawezi hata siku moja kutumia njia hiyo . Hata hivyo aliwataka watanzania kuwa macho na watu hao ambao wameendelea kuongezeka kwa kutapeli kwa kutumia majina ya viongozi hapa nchini .
Baadhi ya vijana wanaofanya kazi katika vijiwe na maduka ya M-Pesa ,Tigo Pesa na mitando mingine wamekuwa wakitapeliwa sana kupitia majina na viongozi wakubwa na kuwa baadhi wamekuwa wakitapeli kupitia jina la mtoto wa rais Jakaya Kikwete ,mkuu wa mkoa wa Iringa , wakuu wa wilaya na baadhi wanatumia majina ya watu maarufu wakiwemo wanahabari na kuwa tayari wamelizwa sana Kamanda wa polisi mkoa wa Ramadhan Mungi amewataka wananchi wa mkoa wa Iringa kuchukua tahadhari dhidi ya watu hao na kuwa pale mtu anapotumia mbinu kama hizo wasisite kuripoti polisi ili kuchukuliwa hatua kali. .......VIDEO INAKUJA HAPA ..... |