Quantcast
Channel: Francis Godwin ::Mzee wa matukio daima::
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2596

WATATU WAFARIKI DUNIA KTK MATUKIO TOFAUTI

$
0
0

RPC Iringa 

Mwandishi  Diana Bisangao wa  matukiodaima.com Iringa 
Watu watatu wafariki dunia mkoani Iringa na mwingine kujeruhiwa katika matukio manne tofauti likiwemo la Alestina Mwayiga (35) mkazi wa Mapanda wilayani Mufindi kufariki baada ya kupigwa ngumi na mateke sehemu mbali mbali za mwili wake.

Akizungumza na mtandao huu wa www.matukiodaima.com ofisini kwake leo Kamanda wa polisi mkoani Iringa Ramadhani Mungi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Kamanda Mungi alimtaja mtuhumiwa huyo jina Tedy Kileo umri bado haujafahamika ambaye ni mume wa marehemu ndiye aliyefanya mauaji hayo ya kusikitisha na kukimbia.

Chanzo cha tukio hilo bado hakijafahamika na mtuhumiwa wa jambo hilo anatafutwa na JESHI la polisi.Katika tukio lingine Madaraka Teleka (18) mfugaji wa Igunga anatafutwa na polisi kwa kosa la kumpiga na fimbo sehemu mbalimbali za mwili na kumsababishia kifo mkulima wa Igunga aitwaye Mashaka Mhembe (38).

Mungi alisema chanzo cha tukio hilo ni baada ya mfugaji huyo kuingiza ng’ombe wake ndani ya shamba la marehemu.

Tukio lingine mtu mmoja amefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wamepanda aina ya Noah lenye namba za usajili T.876 BZN mali ya Ally Makula mkazi wa Mbeya lililokuwa likiendeshwa na Emmanuel Benjamini (37)  kuacha njia na kupinduka maeneo ya Kijiji cha Mkunguru barabara kuu ya Iringa- Dodoma.

Mungi alisema tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 09 februari majira ya saa 10 kamili na kulitaja jina la marehemu ni Upendo Filango (30) mkazi wa Migori, ambapo majeruhi watatu wamelazwa katika Hospitali ya mkoa Iringa na dereva amekamatwa.

Mbali na matukio hayo ya vifo Kamanda Mungi alisema jeshi  la polisi mkoani Iringa linamshikilia mwanamke mmoja jina Joyce Mkumbwike umri haujafahamika kwa kosa la kumjeruhi Amoni Kyando (82) mkulima wa Kilolo kwa kumkata na panga sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo kichwani, usoni na mkono wa kushoto pamoja na sehemu za siri na kumsababishia maumivu makali.

Kamanda Mungi alithibitisha kutokea tukio hilo lililotokea mnamo tarehe 06 februari majira ya saa 2 kamili usiku na kusema majeruhi huyo amelazwa katika Hospitali ya Mafinga huku chanzo cha tukio hilo ni wivu wa mapenzi.
 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2596

Trending Articles