Ndg.Ridhiwani Kikwete Mgombea wa ubunge katika Kura za Maoni za CCM jimbo la Chalinze akijipigia Kura muda huu , pia akipanga mstari katika uwakilishi wa Kata anayotoka ya Msoga..Zoezi la upigaji kura linaendelea hapa Msata (Chalinze).
MTOTO wa mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Taifa na Rais Dr Jakaya Mrisho Kikwete ,Ridhiwani Kikwete ameshinda kwa kishindo katika kinyang'anyiro cha kuwania kuteuliwa kuwa mgombea wa ubunge jimbo la Chalinze kupitia CCM .
Katika uchaguzi huo uliofanyika leo Kikwete amepata kura kura 758 kati ya kura 1321 zilizopigwa huku mpinzani wake wa karibu mdau wa soka Shaban Iman Madega kura 335.
Katika uchaguzi huo jumla ya kura zote zilikuwa ni 1363 wakati kura zilizo Haribika 5 na Halali ni kura 1316 hivyo kwa matokeo hayo Kikwete anasubiri vikao vya juu vya chama ili kutoa baraka kama ateuliwe kuwa mgombea ama vinginevyoWengine walioshiriki uchaguzi huo ni pamoja na Athuman Ramadhan Maneno aliyepata kura 206 na Changwa Mohamed mkwazu aliyeambulia kura 12
Iwapo atapitishwa kuwa mgombea basi atashiriki na vyama vingine kuchukua fomu siku ya tarehe 9/3/2014wakati urejeshaji wa fomu ni tarehe 11/3/2014 KURUDISHA
Tarehe 15/3/2014UZINDUZI RASMI WA KAMPENI ZA CCM( kwa hisani ya JF )