Quantcast
Channel: Francis Godwin ::Mzee wa matukio daima::
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2596

FILIKUNJOMBE KUWAONDOA GIZANI WANANCHI WAKE WA LUDEWA

$
0
0
Wananchi wa kata ya Manda Ludewa wakiwa  wamembeba mbunge wao Deo Filikunjombe baada ya kufurahishwa na utendaji kazi wake 
........................................................
> Awataka wajiandae kutumia nishati ya umeme
> Wananchi  wafurahia  wasema  hawajapata  kuwa na mbunge  kama huyo 
>Wasema hawataki kumpoteza ,wataendelea kumpitisha hadi akatae  yeye 
 
MBUNGE  wa  Jimbo la Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe amewataka wananchi wa Ludewa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wafanyakazi wa Tanesco ambao hivi punde watakwenda katika baadhi ya vijiji wilayani Ludewa ili kupima maeneo ambayo yatapitiwa na nguzo za umeme kwaajili ya kusogeza huduma ya umeme kwa wananchi walioko vijijini.
 
“Changamoto kubwa  katika miradi  mingi ya umeme  ni  kutokana na wananchi  kuwa wagumu  zaidi katika  kujitolea maeneo  ambayo  nguzo za umeme zinapita  na  kutaka  kulipwa fidia  kwa kila kitu... tunaona katika baadhi ya maeneo hapa nchini wananchi wanataka  kulipwa fidia kwa kila kitu hata kama ni mihogo watu wanataka kulipwa,“ alisema Filikunjombe ambaye aliwaasa wana Ludewa tuwe tayari kupokea mradi  huu wa umeme ambao  utafungua milango ya uchumi Ludewa.
 
Akiishukuru REA kwa kukubali kupeleka huduma ya umeme vijijini kwa wananchi wake, Filikunjombe amevitaja vijiji 14 ambavyo vitapelekewa umeme kuwa ni vijiji vya: Ngalawale, Kimerembe, Nkomang’ombe, Luilo, Lifua, Kipangala, Masasi, Lihagule, Igalu, Mbongo, Nsungu, Ilela, Ngerenge na Kipingu.
 
“Huu umeme nimeupata kwa tabu na kwa mbinde sana,“ alisema Filikunjombe huku akiwasihi wananchi wasimwangushe kweye utekelezaji wa mradi huo.
 
Filikunjombe alisema iwapo wananchi wanaozunguka maeneo ya mradi huo wa  umeme  watakubali kuonyesha ushirikiano wao kwa TANESCO upo uwezekano  wa mradi huo  kuanza mapema.  Amewataka wananchi kuangalia uwezekano wa  kusamehe baadhi ya  miti  ya maembe, mikorosho na mihogo itakayong‘olewa kwa ajili ya kupisha nguzo na nyaya za umeme.
 
Filikunjombe ametoa  kauli  hizo kwa nyakati tofauti hivi karibuni wakati wa ziara  yake ya  kuzungumza na wajumbe wa serikali za vijiji vitakavyonufaika na mradi huo wa umeme vijijini ambao utatekelezwa kwa  mpango wa  pamoja kati ya REA na shirika la ugavi wa umeme nchini (TANESCO) ambao utaanza hivi karibuni. “Lengo la serikali iliyopo madarakani chini ya Rais Jakaya Kikwete,“ alisema Filikunjombe “Ni kuona  wananchi wanatatuliwa changamoto mbali mbali zinazowakabili, ikiwemo ya nishati ya umeme vijijini.“
 
Filikunjombe amevitaja vijiji vingine vitakavyopelekewa umeme kuwa ni vijiji vya Kilondo, Luwana, Ludewa Kijijini, Mholo, Mavanga, Mbugani, Mundindi, Shaurimoyo, Lugarawa, Mkiu, Kiyombo, Mlangali, Milo, Mavala, Mapogoro, Ludende, Madindo, Mkongobaki, Amani, Nindi, Ntumbati na Lupingu.
“Ninajivunia kuwa na mwakilishi makini anayetutetea na kutupigania vyema sisi wananchi wake,“ alisema Stanley Kolimba (63) ambaye kwa sasa ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ludewa.  
 
Kolimba alisema juhudi anazozifanya Filikunjombe za kuwaondoa  gizani wananchi wa vijijini ni nuru ya matumaini katika jimbo hilo kwani toka nchi ipate uhuru wake mwaka 1961 vijiji hivyo havijawahi kuona mwanga wa umeme.
 
“Hiki ndicho tunachohitaji wananchi. Tunataka kuona mbunge  tuliyemchagua anafanya yale ambayo sisi tumemtuma  kule bungeni,” alisema Edwin Haule, Diwani wa Kata ya Ruhuhu, iliyoko pembezoni mwa ziwa Nyasa.
 
“Ludewa tumewahi kuwa na  wabunge  wengi. Lakini kiukweli hatujawahi kuwa na mbunge  mchapa kazi kama Filikunjombe ambaye kimsingi utendaji  wake  unatufanya  wananchi tuzidi kuwa na imani  ya  kuendelea kuongozwa na mbunge  huyu. Na kama inawezekana - kwa utendaji  huu  wa mbunge wetu - tungependekeza   Filikunjombe  awe mbunge wa maisha,” alisema Haule.  
 
Toka amechaguliwa mwaka 2010, Filikunjombe amefanya mambo mengi makubwa kwa ajili ya  wananchi wake; barabara  za  Ludewa  kuanza kuboreshwa kwa kiwango  cha lami, uchimbaji wa madini ya makaa ya  mawe na chuma  miradi ambayo yote imeanza utekelezaji katika kipindi chake; na hivyo kuwafanya wananchi wa Ludewa nao waanze kunufaika na matunda ya uhuru.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2596

Trending Articles