Quantcast
Channel: Francis Godwin ::Mzee wa matukio daima::
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2596

WANANCHI WATAKIWA KUTOA TAARIFA ZA UHALIFU MAPEMA

$
0
0
Wito umetolewa kwa wakazi wa Manispaa ya Iringa kutoa taarifa mapema kwa jeshi la polisi pindi wanapoona uharifu unataka kutokea.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa polisi mkoani Iringa Ramadhani Mungi alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu uhalifu wa kutumia tindikali unaoendelea katika mikoa tofauti tofauti.

Kamanda alisema wao kama jeshi la polisi wamejipanga vizuri katika kuzuia uhalifu wa namna hiyo ambapo kwa kutumia askari wanaovaa sare za kazini na wale wasiovaa sare itakuwa rahisi sana kuwakamata watu wa aina hiyo endapo kama watatokea.

"tunawashukuru sana wananchi kwani wamekuwa mstari wa mbele kutupa taarifa mbalimbali za uhalifu hivyo tunawaomba waendelee kutupa taarifa pindi wanapomuona mtu ambaye hana nia nzuri katika mazingira yao ili sisi kama jeshi la polisi tulishughulikie mapema kabla halijaleta madhara mengine katika mkoa huu wetu" alisema kamanda.

pia amesema kupitia wananchi, viongozi mbalimbali pamoja na vyombo vya usalama vikishirikiana hiyo itasaidia mji huu kuendelea kuwa shwari  na wa amani siku zote.

Kwa upande wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Kalenga zinazoendelea amesema kwa sasa hali bado shwari na salama hivyo amewataka wananchi kutosikiliza maneno ya uvumishi, lugha za kichochezi pia kwa upande wa vyama vya siasa viongelee mambo yenye kuleta amani.

hata hivyo Kamanda alisema ana imani kampeni za uchaguzi mdogo wa Kalenga zitamalizika salama na katika hali ya utulivu na amani.

NA DIANA BISANGAO WA MATUKIO DAIMA.COM, IRINGA.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2596

Trending Articles