Quantcast
Channel: Francis Godwin ::Mzee wa matukio daima::
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2596

WAKATI WA KUCHEKEANA NA KUNUNIANA NI HUU ,HII NI BARABARA YA KUELEKEA NYUMBANI KWA MBUNGE WA JIMBO LA IRINGA MJINI MCHUNGAJI PETER MSIGWA ENEO LA KIHESA KILOLO

$
0
0

Hapa  kulia kwenye bendera  ya  Chadema ndipo nyumbani kwa  mbunge Msigwa  

Hii ni  barabara  mbadala  ya  kwenda  kwa  nyumbani kwa  mbunge Msigwa 
Barabara  ya  kwenda  nyumbani kwa mbunge Msigwa  hii hapa ni  noma sana

Hii ni  barabara ya  pili ya  kuingia kwa Msigwa ni kama  kisiwa

Hii ni barabara  ya  kupandisha  nyumbani kwa mbunge Msigwa
Hapa ni eneo la Kihesa  kilolo Bwawani
Nyumba  za karibu na mbunge Msigwa

hapa  kulia ni  nyumbani kwa mbunge Msigwa
Hili ni dimbwi la maji  lililopo nje ya  geti la mbunge Msigwa ni  kifusi  lori  moja  pekee 
Jitihada za  wananchi  katika  kunusuru  barabara ya  mbunge Msigwa
maeneo ya  nyumbani kwa mbunge Msigwa


Usishangae  ni barabara  ya  mbunge wa  jimbo la Iringa mjini  kuelekea  kwake












  
Mbunge Msigwa 
Hii  ni  barabara  ya  kuelekea  nyumbani kwa  mbunge wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa (chadema) ni mbovu  kuliko mfano wapiga  kura  wake wanatabika  usiku na mchana  ni kiasi cha  mbunge kujitolea kifusi  kuondoa adha  hii ama mbunge Msigwa   hajaliona  hili?chonde chonde  mbunge jaribu  kulitazama  hili kwa  jicho la  pili.

Pia napenda  kumshauri  mbunge wangu Msigwa kuna ahadi  mbali mbali alipata  kuziahidi mwaka 2010  wakati wa kampeni  ikiwemo ya uboreshaji wa miundo mbinu kama barabara na pia kila  wakati  alilalamikia  gari la  aliyekuwa mbunge enzi  hizo Monica Mbega  kuwa anatembea na Zahanati mbili  ila cha ajabu  nae amenunua gari la gharama kuliko  hilo pia aliahidi kama atakuwa mbunge atahakikisha anapanda  basi la King Cross kwenda  Bungeni Dodoma na ahadi nyingine ni ile ya  kuweka mwanasheria ofisini kwake , kumwajiri  Frederick Mwakalebela kama mtaalam wa michezo na nyingine nyingi  sasa sijui ameanza ahadi  ipi kuitekeleza ,ni ushauri  japo najua atayakana  yote kama ilivyo siku  zote mazuri ya Kwake mabaya  yakiwemo ya uchafu ni ya serikali ya CCM  

Safu  hii  ya  wakati  wa kununuana na  kuchekeana  itaendelea  kuangazia kona  mbali mbali  pamoja na kutazama ahadi za  madiwani ,wabunge na Rais hivyo iwapo unaikumbuka  ahadi ya  kiongozi  wako waweza itupia  hapa na picha kwa  email .fgodwin94@gmail.com ama  tupigie  simu 0754026299

Kesho  itakuwa ni barabara ya  kuelekea  nyumbani kwa  meya Mwamwindi na naibu meya usikose
kufuatulia safu  hii

Ubovu  wa barabara  ya  kuelekea  nyumbani kwa  mbunge Mafulu  wa CCM eneo la Mkimbizi msikitini
Wananchi wakilazimika  kushuka katika  daladala  ili  iweze  kupita
........................................................

Hii  ni  barabara  ya  kuelekea  nyumbani kwa  mbunge wa  viti maalam mkoa  wa Iringa Lediana Mafulu (CCM) ni mbovu  kuliko mfano wananchi wanatabika  usiku na mchana  ni  mwendo  wa mbunge kujitolea kifusi  kuondoa adha  hii ama mbunge Mafulu  hajaliona  hili?chonde chonde  mbunge jaribu  kulitazama  hili kwa  jicho la  pili.

Safu  hii  ya  wakati  wa kununuana na  kuchekeana  itaendelea  kuangazia kona  mbali mbali  pamoja na kutazama ahadi za  madiwani ,wabunge na Rais hivyo iwapo unaikumbuka  ahadi ya  kiongozi  wako waweza itupia  hapa na picha kwa  email .fgodwin94@gmail.com ama  tupigie  simu 0754026299



Viewing all articles
Browse latest Browse all 2596

Trending Articles