Na Kenneth John matukiodaima.com Dar
Wizara ya ujenzi imesema kuwa ipo katika hatua mbalimbali za ujenzi wa barabara za juu katika jiji la Dar es salaam.
Hayo yamebainishwa na mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa wizara ya ujenzi Bw. Martin Ntemo, ambapo amesema kuwa kunamaeneo kumi na mbili yameshabainishwa yakujengwa,lakini kwa kuanzia wataanza na eneo la Tazara na kufuatia na ubungo na kuendelea,
Ntemo ameeleza kuwa kuhusu eneo hilo la Tazara, tayari Wajapani wameshajitokeza kugharamia ujenzi wake,Huku kuhusiana na ubungo World bank ndio ambao wanasimamia kuanzia ubunifu na kufuatiwa na ujenzi wake.Na kuongeza kuwa kwasasa wanasubiri kupata majina ya wakandarasi kutoka kwa Wajapani , pamoja na gharama sambamba na muda utakaotumika kujenga eneo hilo.
Hata hivyo Ntemo amesema kuwa, wamekuwa wakiendelea kushughurikia barabara za kuondoa msongamano katika jiji la Dar es salaam, ambazo baadhi ya barabara hizo amesema ni pamoja na ile ya Ubungo bus terminal kuelekea Kigogo round about,Kigogo round about kwenda Jangwani,Tabata dampo na ubungo maziwa,Jet kona kuelekea vituka,Mbezi marimba mawili Kinyerezi,Tegeta kibaoni kuelekea Wazo hili,Tank Bovu kwenda Goba,Kimara baruti kuelekea Misiwi Changanyikeni.
Aidha Ntemo amesema kuwa hadi sasa kuna miradi mbalimbali, ambayo inaweza kufunguliwa muda wowote kuanzia sasa, mara baada ya taarifa kutoka ngazi za juu .