Uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa umepania kuwatengea vituo vya kudumu madereva wa pikipiki maarufu kama boda boda ili kuboresha huduma hiyo zaidi.
Mkurungezi wa Manispaa ya Iringa Terresia Mahongo ameyasema hayo leo alipozungumza na mtandao huu wa www.matukiodaima.com kuwa vijana hao wanaoifanya kazi hiyo ni wadau pia wa maendeleo hivyo mbali ya kutegemea kazi hiyo bado wanasaidia kutoa huduma ya usafiri kama madereva wa Taxi hivyo wanapaswa kuwa na vituo vinavyotambulika rasimi.
Hata hivyo alisema wakati huo ambao Manispaa imejipanga kubainisha vituo madereva hao wataendelea kuwepo katika maeneo yao kabla ya kuonyeshwa maeneo ya kudumu.
Hatua hiyo ya uopngozi wa Manispaa kutumia busara katika ufumbuzi wa suala hilo umeungwa mkono na wengi japo mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma alisema kuwa lazima Manispaa kuwatengea vituo vijana hao ambao wamepata kujiajiri katika shughuli hiyo .
Uchunguzi unaonyesha usafiri huo wa boda boda umechangia kushusha bei kubwa ya Taxi ambayo ilianza kupandishwa kiholela mjini hapa na kutokana na ubovu wa barabara zilizo nyingi boda boda zimekuwa zikisaidia kuwanusuru wananchi na kero ya usafiri.