Quantcast
Channel: Francis Godwin ::Mzee wa matukio daima::
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2596

HAKI IMETENDEKA , SIPENDI KUONA TENA.!!!? NA HONGERA MWANASHERIA MWANISPAA YA IRINGA

$
0
0
 Vijana wasajili line eneo la posta mjini Iringa ambao  walikuwa wakipinda hatua ya  mgambo wa Manispaa ya Iringa  kuwaondoa  eneo hilo na kuliacha   tela la gari ambalo lilikuwa likifanya kazi kama ya kwao eneo hilo wakionyesha furaha yao baada ya kazi iliyofanywa na safu ya SIPENDI KUONA mtandao  huu  wa www.matukiodaima.com katika kupinda tela la gari  lililoegeshwa eneo hilo kuendelea  na shughuli ,ambalo baada ya kutoa masaa 12 kuanzia  saa 7 mchana  Manispaa kutenda haki hivi  sasa limeondolewa mida ya saa 8 mchana hivyo pongezi kwa Manispaa ya Iringa maoni ya mtandao  huu kwa  wafanyabiashara  wanaofanya maeneo yasiyoruhusiwa ni vema  kufuata kanuni ,sheria na taratibu  ili kuuwezesha mji  wetu wa Iringa ambao ni wa pili kwa usafi  kuendelea kuwa mfano  wa  usafi

  HIKI NDICHO  KILICHOPINGWA  AWALI NA MTANDAO  HUU NA  JUU NI UTEKELEZAJI  WAKE

SIPENDI KUONA MGAMBO WA MANISPAA YA IRINGA NA WANASHERIA WAKINYANYASA WASAJILI LINE NA WATOA HUDUMA ZA KIBENK KUPITIA SIMU HUKU GARI HILI POSTA LIKIACHWA

Mwananchi  wa Iringa akipita  eneo la posta jirani na gari  linalotumiwa kutoa  huduma za M-PESA kinyume na sheria

 Hawa ni  wasajili line ambao  wamezuiliwa kufanya shughuli eneo la posta na maeneo mengine mjini Iringa



 Hili ni gari ambalo  linafanya shughuli za M-PESA  langoni mwa Posta  Iringa  licha ya sheria kuzuia  watu kufanya biashara maeneo yasiyo rasmi
 Hawa ndio  wanyonge  waliochukuliwa  meza  zao kwa kudaiwa kufanya biashara maeneo hayo ya posta ambayo si rasmi 
.,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

 Leo Mgambo  wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa  wameendesha msako mkali wa kuwaondoa  wauza vocha za simu na wato  huduma za kifedha kama M-PESA  na mitandao mingine  wote  waliokuwemo maeneo yasiyo rasmi  huku gari  hili lililopo eneo la uzio wa Posta mjini Iringa likiendelea  kufumbiwa macho , sina shaka na utendaji kazi wa mgambo na mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa ila inanitia shaka kwanini kama ni zoezi maalum la kusafisha mji kwa kuwaondoa wanaofanya kazi maeneo yasiyo rasmi gari hili ambalo nalo lipo eneo lisilo rasmi likiachwa ? ama mnataka  kusema sheria ni kwa wanyonge  pekee? ama kuna mkono wa kiongozi mmoja kati yenu ? au ndio kusema mgambo  hili hamlioni? Sasa  safu hii ya Sipendi kuona inatoa muda wa masaa 12 kwa mgambo na  mwanasheria  wa Manispaa ya Iringa pamoja na wote  wanaohusika kusimamia sheria kwa kulitoa gari hili hapa kwani nasema hivi SIPENDI KUONA Sheria ikiwalinda wenye nacho na ikiwakandamiza  wanyonge  nasema  sipendi kuona

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2596

Trending Articles