Quantcast
Channel: Francis Godwin ::Mzee wa matukio daima::
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2596

HABARI INAYOKUMBUKWA ZAIDI ,DIWANI ALIYEMWITA CHILIGATI FISADI SASA AMGEUKIA MBUNGE WAKE

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Kalenga mkoani Iringa Dr.Wiliam Mgimwa
Diwani kata ya Mgama Denis Lupala

SAKATA la Diwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Mgama, Wilaya ya Iringa Vijijini, Denis Lupala, ambaye alimwita Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Kapteni John Chiligati kuwa ni fisadi limeendelea kuchukua sura mpya ndani ya CCM baada ya diwani huyo sasa kumvaa Mbunge wa Jimbo la Kalenga, Dk. William Mgimwa, kwa madai kuwa amekuwa na tabia ya kuendekeza makundi na kukitaka chama hicho kumvua gamba.

Akizungumza na mtandao huu  wa  www.matukiodaima.com , Lupala alisema kuwa upo uwezekano wa serikali ya CCM iliyopo madarakani kuendelea kuchafuliwa na viongozi wake na kutoa nafasi kwa vyama vya upinzani kama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuendelea kupata umaarufu kutokana na wale waliochaguliwa kuendeleza chuki za kura za maoni ndani ya CCM.

“Ujue wapo wabunge ambao hawaamini kama wamekuwa wabunge na hawaamini kama uchaguzi mkuu umemalizika ...wabunge hawa ndio ambao bado wanaendekeza makundi hadi sasa kwa kuwachukia wale waliokuwa upande wa wagombea wengine wakati wa mchakato…mfano mbunge wetu wa Jimbo la Kalenga, Dk. Mgimwa, yeye bado anaendelea kuwatumia wapambe wake kwa kila jambo na kuwatenga wale ambao hawakuwa upande wake,” alisema.

Diwani huyo ambaye wakati wa mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM alikuwa akimuunga mkono Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro, alisema kuwa hivi sasa Mbunge wa jimbo hilo, Dk. Mgimwa amekuwa akimtenga katika shughuli nyingi ambazo amekuwa akizifanya katika kata yake ya Mgama.

Akitolea mfano alisema kuwa hivi karibuni mbunge huyo alifika katika kata hiyo kwa ajili ya kukabidhi madawati katika Shule ya Sekondari ya Mgama ila yeye kama diwani hakushirikishwa katika zoezi hilo, jambo ambalo linaonyesha wazi mbunge huyo bado anaendekeza chuki kwa wana CCM ambao hawakumuunga mkono katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Hivyo diwani huyo alikitaka Chama Cha Mapinduzi kutowavumilia wabunge wanaoendekeza makundi kwa kipindi hiki na kuwa ni vema nao kuvuliwa magamba ndani ya chama ama kupewa onyo.

Akielezea kuhusu madai ambayo alitaka kufikisha kwa Chiligati wakati wa ziara yake kabla kumwita fisadi kuwa ni pamoja na kero ya umeme, uhaba wa walimu na vitabu.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kalenga, Dk. Mgimwa akizungumzia madai ya diwani huyo kwa njia ya simu alisema kuwa madai hayo si ya kweli na kuwa siku ya kwenda kukabidhi madawati alipewa taarifa ila hakufika.

“Mimi nilimpa taarifa ila hakufika katika zoezi hilo la kukabidhi madawati japo hata mimi mwenyewe sikwenda nilituma wasaidizi wangu,” alisema Dk. Mgimwa.( habari hii ni ya maktaba ya matukiodaima.com ya April 2011)

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2596

Trending Articles