Waswahili wanasema ukiona mtu mzima analia uje yamemkuta. Mwanalibeneke Francis Godwin aibuka na kulia na wezi wa kazi zake. Siku hizi tasnia ya uandishi wa habari imevamiwa na watu wasiojua kanuni na taratibu za fani hii uandishi.
Cha kusikitisha zaidi, unakuta baadhi ya taasisi na mashirika makubwa binafsi na umma yanaunga mkono wimbi hili la Makanjaja, na kuacha kusaidia na kuunga mkono waandishi wenye taaluma na uzoefu wa kazi zao. Inasikitisha kuona mwaka mzima mtu anamiliki blog, lakini hakuna hata story moja aliyoandika ya kwake zote ka-copy. Sisi Swahili TV kampuni ya kihabari ya nchini Marekani tunamuunga mkono Francis Godwin juu ya wezi wa kazi zake.
Kilio cha Mwanalibeneke