Quantcast
Channel: Francis Godwin ::Mzee wa matukio daima::
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2596

RC ISHENGOMA AAGIZA HALMASHAURI KUSIMAMIA FEDHA ZA MIRADI

$
0
0
 Mkuu wa  mkoa  wa Iringa  Dr.Christine Ishengoma akifungua  kikao cha kamati  ya ushauri  ya mkoa katika  ukumbi  wa Siasa ni Kilimo leo


 Vyombo  vya  ulinzi na usalama  mkoa  wa Iringa  vikifuatilia kikao hicho
 Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Dr Christine Ishengoma  akifungua  kikao cha RCC mkoa wa Iringa kulia ni mstahiki meya  wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi na kushoto ni katibu  tawala  mkoa wa Iringa Wamoja  Ayub


 Wajumbe wa  kikao cha kamati  ya ushauri mkoa (RCC)  wakiwa wamesimama kwa kumkumbuka aliyekuwa mkurugenzi wa Halmashauri ya  Kilolo marehemu Mohamed Gwalima aliyefariki ghafla  hivi karibuni ,kutoka  kushoto ni mkuu wa wilaya ya  Kilolo Gerald Guninita, mbunge  wa jimbo la Kilolo Prof Peter Msolla,mwenyekiti  wa Halmashauri ya  wilaya ya  Kilolo Joseph Muhumba na kaimu mkurugenzi wa wilaya ya Kilolo
 Mkuu wa mkoa  wa Iringa Dr Ishengoma Mstahiki meya  wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi na RAS Iringa wamoja  Ayub wakimkumbuka mkurugenzi Kilolo aliyefariki dunia mwezi huu
 Wajumbe wa kikao cha RCC Iringa  wakimkumbuka aliyekuwa mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilolo Mohamed Gwalima aliyefariki dunia hivi karibuni ,kutoka kulia ni mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati, mbunge wa viti maalum mkoa  wa Iringa Lediana Mafulu Mng'ong'o ,mbunge wa jimbo la Mufindi Kusini Mendlad Kigolla ,mku wa wilaya ya Mufindi, Evarita kalalu na mwenyekiti wa Halmashauri ya  Mufindi Peter Tweve










Mkuu  wa mkoa  wa  Iringa  Dr Christine Ishengoma  ameziagiza Halmashauri  mkoa  wa  Iringa  kuhakikisha  wanasimamia  vema fedha  za miradi  zinazotolewa na serikali katika maeneo yao.

Mkuu   huyo wa  mkoa  ametoa agizo hilo leo  katika  ukumbi  wa Siasa ni Kilimo   wakati  akifungua  kikao  cha kamati  ya  ushauri ya  mkoa (RCC).

Amesema kuwa  lengo la  serikali  kutuma fedha za miradi katika Halmashauri  husika ni kuwezesha kusukuma mbele  kasi ya  miradi ya maendeleo katika Halmashauri.

Hivyo  alisema haitapendeza  kuona  fedha za miradi katika Halmashauri  zinakosa usimamizi mzuri na  kupelekea  miradi  kukwama  kumalizika kwa wakati.

Aidha  alitaka viongozi  wa Halmashauri kubuni miradi  ya kuziwezesha  Halmashauri  zao  kuongeza mapato  zaidi.

Kwani  alisema bila ya  Halmashauri kubuni  miradi  ya  kiuchumi uwezekano  wa Halmashauri  kujiendesha utakuwa mdogo  zaidi.

Kuhusu  watumishi  wasiojituma katika kazi  mkuu wa mkoa  ametoa onyo kwa  watumishi hao  na kuwa kamwe  hata wavumilia.

Katika  hatua  nyingine  mkuu  huyu  wa mkoa ametoa agizo kwa jeshi la polisi  mkoa  wa Iringa kupitia  askari  wake wa usalama barabarani  kuwakamata na  kuyakamata  na  kuyatoza fani  magari  yote  ya abiria ambayo yatapita katika mkoa  wa Iringa  bila kuwa na  vifaa vya  kuhifadhia  taka na  yale  yatakayobainika yakichafua mazingira  ovyo.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 2596

Trending Articles