Wakati unaingia nyumbani kwa bilionea Erasto Msuya hili ndio bango lililokua limewekwa.
Hapa utaratibu wa kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Maremu Erasto Msuya.
Hii ndio nyumba ya milele ya bilionea Erasto Msuya ikiandaliwa.
MIRERANI zikiwa ni siku takribani sita zimepita tangu mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite aliyefahamika kwa jina la Erasto Msuya kupigwa risasi zaidi ya ishirini na kufariki dunia papo hapo katika eneo la Bomang'ombe karibu na njia panda ya KIA). Kifo hicho kilichokua na utata mkubwa na kupelekea watu wengi kujiuliza maswali mengi yasiokua na majibu.
Leo ilikua ni siku ya mazishi ya mfanyabiashara huyo ambaye kutokana na kuwa alikua akiishi jijini Arusha maeneo ya kwa Iddi ilibidi jana jumatatu wafanye utaratibu wa kuuga mwili wa marehemu nyumbani kwake na leo jumanne kwenda kuzikwa Mirerani katika kijiji cha Kairo.
Msiba wa Erasto ulikua ni gumzo kubwa sana na watu wamekiri hawajawai kuona msiba kama huu maana kilichokua kikiwashangaza watu ni jeneza lililokua likifunguliwa kwa rimoti, na pia ni mazishi yaliyokua na watu wengi sana. Kila kona kulikua na minong'ono ambayo ilikuwa ikizungumzia utata wa kifo chake.
Kamati ya maandalizi ya mazishi wakishirikiana na ndugu, jamaa na marafiki walijitahidi sana kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa maana haikuwa kazi rahisi kuweza kumudu kuhakikisha usalama wa wingi wa watu uliokuwepo katika mazishi ya Erasto.