Viongozi kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa wakitembelea eneo la hifadhi ya msitu unaosimamiwa na maradi wa shirika la Kidundakyeve eneo la Kiwere Iringa vijijini leo
Aliyekuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira duniani mkoani Iringa ,mwenyekiti wa kamati ya mipango na mazingira katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ,Bw Hamza Ginga ( wa tatu kushoto) ambae ni diwani wa kata ya Kwakilosa mjini Iringa akiwa na viongozi mbali mbali wa wilaya ya mkoa anayeongea nae ni mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa Stivin Mhapa
Mkuu wa utawala ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa mama Mlawi akitambulisha timu yake kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa leo
watumishi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wakicheza kwa furaha katika maadhimisho ya siku ya mazingira ulimwenguni
Idara ya maliasili wilaya ya Iringa vijijini pia ikishiriki kutoa elimu ya ujangili katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha
Aliyekuwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Iringa ,Mwenyekiti kamati ya mipango na mazingira katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ,Bw Hamza Ginga ambae ni diwani wa kata ya Kwakilosa mjini Iringa ( kushoto) akitembelea banda ya maonyesho leo
Aliyekuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira duniani kwa mkoa wa Iringa ,mwenye kamati ya mipango na mazingira katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ,Bw Hamza Ginga ambae ni diwani wa kata ya Kwakilosa mjini Iringa (kulia) akihotubia katika maadhimisho hayo leo ,kulia kwa ni mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa Stivin Mhapa na diwani wa kata ya Kiwere Paschal . Mwamwano.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Chistine Ishengoma ( pichani aliyesimama) kushoto kwake ni mkuu wa wilaya ya Iringa Dr Leticia Warioba
.................................................................................................................................................................
MKUU wa mkoa wa Iringa Dkt Christine Ishengoma ameapa kuwashughulikia kwa kuwachukulia hatua kali viongozi wa serikali kuanzia ngazi ya kijiji hadi tarafa ambao watazembea kuwamakata wananchi wanaochoma moto ovyo kwa lengo la kuharibu mazingira katika maeneo yao
Pia apiga marufuku ulimaji wa maeneo yenye chem chem na vyanzo vya maji huku akisisitiza wananchi wanaokiuka agizo lake kuwajibishwa kisheria.
Mkuu huyo wa mkoa ametoa kauli hiyo leo katika kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira ulimwenguni ambayo kwa mkoa wa Iringa maadhimisho hayo yalifanyika katika kijiji cha Kiwere kata ya Kiwere wilaya ya Iringa vijijini wakati kitaifa yamefanyika mkoani Rukwa na kidunia nchini Brazir .
Siku ya mazingira ambayo ilianzishwa rasmi mwaka 1972 na umoja wa mataifa ili kutilia mkazo hifadhi ya mazingira na kila mwaka huja na kauli mbinu mbali mbali wakati kwa mwaka huu kauli mbiu ni "FiKIRI KABLA YA KULA "Hifadhi mazingira .
Mkuu huyo wa mkoa ambae alipaswa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo hotuba yake ilisomwa na mwenyekiti wa kamati ya mipango na mazingira katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ,Bw Hamza Ginga ambae ni diwani wa kata ya Kwakilosa mjini Iringa .
Alisema kuwa suala la uharibifu wa mazingira katika mkoa wa Iringa linaweza kuepukika iwapo kila kiongozi atawajibika katika nafasi yake kwa kutoa elimu kwa wananchi wake juu ya uharibifu wa mazingira pamoja na kuwachukulia hatua kali wananchi watakaoshindwa kuhifadhi mazingira na wale wanaochoma moto ovyo misitu.
Kwani alisema iwapo kiongozi wa serikali ngazi ya kijiji hadi tarafa atashindwa kuwajibika basi ofisi yake itachukua nafasi ya kuwawajibisha viongozi hao wanaoshindwa kuwajibika kusimamia uhifadhi wa mazingira.
" Mimi nina imani kubwa kuwa mnawajua watu wanaoanzisha moto na ili kupunguza misitu ,vichaka na nyasi ni vema serikali ya kijiji hadi tarafa kuchukua hatua kali dhidi ya wahalifu hao wanaochoma moto ovyo misitu na iwapo viongozi mtashindwa basi serikali itawawajibisha viongozi"
Hata hivyo alisema kuwa viongozi wa vijiji hadi wilaya wanapaswa kuhifadhi mazingira kwa kuwawajibisha wanaolima kando kando ya mito ,wanaoanzisha moto kichaa na wale wote wanaoendesha shughuli zinazochangia mazingira kuharibiwa .
Aidha aliwataka viongozi wa vijiji kutambua na kuweka mipaka ya maeneo ya vyanzo vya maji katika kila kitongoji ili kujulikana na pindi kinapoharibiwa wahusika wachukuliwe hatua kali .
Mbali ya mkakati huo wa mipaka pia alitaka kuwepo kwa utaratibu wa kufanya kampeni za kuzuia ulimaji wa kwenye mabonde (vinyungu) na maeneo yaliyoko kwenye vyanzo vya maji ikiwa ni pamoja na kutengeneza barabara za kuzuia moto kuzunguka vyanzo vyote vya maji.
Awali akitoa taarifa ya ya maendeleo ya hifadhi ya mazingira katika wilaya ya Iringa kama wenyeji wa maadhimisho hayo kwa mwaka 2013 mshauri wa maliasili wilaya ya Iringa Alloyce Mawere alisema kuwa katika kuendelea kuhifadhi vyanzo vya maji Halmashauri hiyo imeainisha vyanzo vya maji 383 kati ya hivyo 183 vimehifadhiwa kwa kupandwa miti rafiki na maji .