Mkurugenzi wa Lino International Agency, Hashim “Uncle” Lundenga akisisitiza jambo na kwa warembo wa Redds Miss Sinza 2013 alipotembelea kambi ya mazoezi hayo. Warembo hao watapanda jukwaani Ijumaa kuwania taji la mwaka huu. (Picha/Mpiga picha wetu).
Na Mwandishi Wetu
.....................................................................................................................................................
Mkurugenzi wa kampuni ya Lino International Agency, Hashim “Uncle” Lundenga amewafagilia warembo 12 wanaowania taji la Redds Miss Sinza 2013 kuwa kila mmoja anaweza kutwaa taji hilo katika mashindano yaliyopangwa kufanyika kesho Ijumaa kwenye ukumbi wa Meeda Club uliopo Sinza Mori.
Lundenga alisema hayo katika hotuba yake fupi baada ya kutembelea kambi hiyo akiwa na kamati yake yote ya Redds Miss Tanzania. Wajumbe wengine waliokuwepo katika msafara huo ni Bosco “Mshua” Majaliwa ambaye ni Katibu Mkuu, Albert Makoye (Mkuu wa Itifaki), Hidan Ricco (Afisa Uhusiano) na Yason Mashaka.
Alisema kuwa warembo wa Redds Miss Sinza wanakazi kubwa ya kulinda heshima ya mwaka jana ambapo Brigitte Alfred alitwaa taji hilona baadaye kutwaa taji la Miss Kinondoni na Tanzania.
“Mpo vizuri na ninatarajia kuona ushindai mkubwa, naamini majaji watafanya kazi kubwa na mshindi atakayepatikana atakuwa wa halali, kwani hakuna upendeleo katika kutafuta mshindi, mara nyingi tumekuwa tukitafuta mrembo bora na si bora mrembo,” alisema Lundenga.
Alisema kuwa warembo wote 12 wanatakiwa kujua uwa hakuna rushwa ya ngono katika mashindano hayo na wale wanaosema hivyo wana lengo la kuharibu sifa ya mashindano hayo. Aliongeza kuwa mshindano hayo yana miaka 20 sasa na washindi wamepatikana kwa njia ya halali na kama kuna masuala ya ngon basi hiyo ni tabia ya msichana na wala hayahusiani na mashindano.
Mratibu wa mashindano hayo, Majuto Omary alisema kuwa maandalizi yamekamilika nay a Twanga Pepeta itatumbuiza siku hiyo huku ikitambulisha baadhi ya nyimbo zake mpya zilizomo katika albamu ya 12 ijulikanayo kwa jina la Nyumbani ni Nyumbani.
“Ikukmbukwe kuwa twanga pepeta haijatumbuiza Sinza kwa
kipindi kirefu na hivyo kuandaa zawadi maalum kwa mashabiki wake katika mashindano hayo yaliyo dhaminiwa na Redds Original, Dodoma Wine, Chilly Willy Energy Drink, Fredito Entertainment, CXC Africa, Clouds Media Group, Salut5.com na Sufiani Mafoto blog,” alisema Majuto.
Wakati huo huo, mbunifu wa mitindo, Veronica Lugenzi atawavalisha nguo warembo hao watakaopanda jukwaani kesho, Veronica ambaye alimvalisha nguo Miss Universe Tanzania wa mwaka jana, amechukua jukumu hilo baada ya kuvutiwa na ubora wa warembo hao.
Mwisho…