Quantcast
Channel: Francis Godwin ::Mzee wa matukio daima::
Viewing all 2596 articles
Browse latest View live

MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO WA TANZANIA YAFANA WASHINGTON DC,MWIGULU NCHEMBA AANDIKA HISTORIA MPYA

$
0
0
Mh:Mwigulu Nchemba akizungumza na Watanzania hapa Washington DC kwenye Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano.Mh:Mwigulu Nchemba akiongozwa na Balozi wa Tanzania hapa Washington DC Bi.Libereta Mulamula Kuelekea Kufungua Sherehe za Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania hapa Washington DC.Mke wa Mh:Mwigulu Nchemba (Kulia)akisalimiana na Mwanamitindo Maarufu wa Mavazi hapa Washington DC na Viunga Vyake Miss Temeke wa "KWETU FASHION".

Ukuta Umependeza kwa Baongo Kubwa la Miaka 50 ya Muungano hapa Ubalozini Washington.Mh:Mwigulu Nchemba akitembelea Mabanda ya Maonesho ya Vitu Mbalimbali vya asili ya Tanzania nje ya Jengo la Ubalozi wa Tanzania hapa Wahsington DC.
Mh:Mwigulu Nchemba akipata maelezo kuhusu Vitenge na Khanga zinazouzwa Nje ya Jengo la Ubalozi wa Tanzania zenye Kutengenezwa Tanzania.
Maonesho yanaendelea hapa Washington DC,Ubalozi wa Tanzania.Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano yamefana sana Washington DC.
 Mh:Mwigulu Nchemba akikata Utepe Kuashiria Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano hapa Washington Dc Zimefunguliwa rasmi,Kulia Kwake ni Balozi Libereta Mulamula na Kulia Kwake ni Waziri anayeshughulikia Muungano-Zanzibar Mh:Mwinyihaji Makame.

Ubunifu:Miaka 50 Ya Muungano wa Tanzania hapa Washington DC.Viongozi wakionja Chakula cha Asili cha Tanzania kilichopikwa hapa Washington DC,Ugali wa Mihogo,Makande,Ndizi,Kisamvu n.k Vilikuwepo.Katikati ni Bwana Okoka Sanga akiwa na Viongozi wa Kitaifa waliofika Kuadhimisha Miaka 50 ya Muungano hapa Washington,Okoka Sanga ni Mtengenezaji Maarufu wa Kadi na Mifuko ya Zawadi hapa Washington DCMaadhimisho yanaendelea huku Kuta za Jengo la Ubalozi zikiwa Zimepambwa Picha za Viongozi wetu wa Kitaifa.
Bidhaa za Bakharesa pia Zilikuwepo kwenye Sherehe hizi za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano,Hakika Zimefana sana.
Tanzania Nchi inayopendwa na Mataifa Yote Duniani,Kisiwa cha Amani na Upendo.

I love Tanzania,Bibi huyu wa Kizungu alipata Kuishi Tanzania na Kufanikiwa Kupandisha Sehemu ya Mlima Kilimanjaro,Hapa anahamasisha Watu Kupanda Mlima Kilimanjar.
Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Kutoka Huston-Texas Waliofika hapa Washington DC Wakiwa katika Picha ya pamoja na Mh:Mwigulu Nchemba mara baada ya Kuzungumza Machache kuhusu Kuimarisha Chama hapa Marekani,
Mh:Mwigulu Nchemba akimvisha Skafu ya Tanzania huyu Mtoto wa Kizulu-South Africa aliyepiga Ngoma na kufanya Umati Kushangilia kwa Shangwe,Baba yake wa huyu Mtoto aliwahi Kuishi Tanzania Mwaka 1982.
 Kikundi cha Wacheza Ngoma ya Asili cha Watanzani waishio hapa Marekani Wakitumbuiza Kwenye Sherehe za Miaka 50 ya Muungano.
Mh:Mwigulu Nchemba akibadilishana Mawazo na Watanzania nje ya Jengo la Ubalozi hapa Washington DC.Kwetu FashionNje ya Jengo la Ubalozi Watanzania wanabadilishana Mawazo,Wamepata Fursa yakuwa pamoja kwa sababu ya Muungano Wetu uliofikisha Miaka 50 hii leo.Mtanzania akiwaongoza wazungu hawa Kula chakula cha Asili cha Tanzania. Miss Tanzania wa hapa Marekani aliyeshinda Mwaka Jana 2013/2014 akiwasili Ubalozini tayari kwa Kuungana na Watanzania Kusherekea Miaka 50 ya Muungano.Tanzani Is All AaboutUkodak Unahusika.
 Watanzania Wamefurahi sana Hapa Washington DC kuadhimisha Miaka 50 ya Muungano,Wamejitokeza Kwa Wingi sana,Hivi ndivyo Muungano Ulivyofana Miaka 50,Nyama Choma na Vyakula vya asili vimepatikana Kwa Wingi hapa TANZANIA HOUS Washington DC.Tanzania Culture is All about.
Maadhimisho yamefana sana,Mtoto akionesha Uwezo wa Kucheza Ngoma ya Asili.Chombo cha Habari "SAUTI YA AMERIKA'VOA nao Walijumuika na Watanzania hapa Marekani,.Mtangazaji Hamza Mwamoyo akiwana Viongozi wa Serikali ya Tanzania Mh:Mwigulu NChemba (Kulia) na Mh:Mwinyihaji(Kushoto) baada ya Kufanya Kipindi kitakacho rushwa Voice Of America.
Balozi Mulamula akimkaribisha Askari wa Jeshi Kutoka Ubalozi wa Nigeria hapa Washington DC.Col.Mutta Kulia wa Ubaliozi wa Tanzania akimkaribisha Kiongozi Kutoka Ubalozi wa Camerron hapa Washington DC.Mapokezi yanaendelea kwa Wageni Kutoka Mataifa Mbalimbali waliofika Kuhudhuria Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania hapa Washington DC.
 Askari wa Mataifa Mbalimbali waliojumuika na Watanzania Kusherekea Miaka 50 ya Muungano Kutoka Kushoto ni Nigeria,Poland,Zimbabwe na Zambia waki kwenye Picha ya pamoja na Mh:Mwigulu NchembaKushoto ni Ndugu Mrisho Mzese Kutoka Maryland na Ndiye Mwenyekiti wa Shina la CCM  Maryland.Mh:Mwigulu Nchemba akiendelea Kusalimiana na Watanzania Mbalimbali walofika kwenye Ukumbio wa Marriott Hotel hapa Washington DC kusherekea Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania.
Mh:Mwigulu Nchemba akisalimiana na Askari wa Jeshi kutoka Ubalozi wa Nigeria aliyefika Kujumuika na Watanzania kwenye Sherehe za Muungano wa Miaka 50 wa Jamhuri ya Muungano Ya Tanzania.Watanzania wakiwa Kwnye Mavazi ya Kiafrica zaidi
Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 zimefana sana hapa Washington DC.Tanzania ianapendwa sana na Mataifa Mengine ya Africa,Kushoto ni Raia wa Nigeria na Kulia ni Raia wa Cameroon wamefika Kuungana na Watanzania hapa Washington DC kusherekea Miaka 50 ya Muungano.
 Mh:Mwigulu Nchemba akibadilishana Mawazo na hawa Wazungu waliopata Kuishi Nchini Tanzania miaka ya 1990's.
Tanzania Is All about kwa hapa Washington DC,Tuudumishe Muungano Wetu.Huyu Dada wa Kitanzania amesafiri Kutoka Calfoni hadi Washington Kwaajili ya Kuuongoza Watanzania kuimba Wimbo wa Taifa wa Tanzania na Marekani,Ameonesha Kipaji chake cha ajabu cha Kuimba Nyimbo zote mbili kwa Ustadi Mkubwa sana.

Balozi Libereta Mulamula akiwa na Mme wake alipomuita Kwaajili ya Kumtambulisha kwa Watanzania waliofika kusherekea Miaka 50 ya Muungano.
Viongozi wakisikiliza Kwa Makini maneno ya Balozi Mulamula(hayupo Pichani).
 Mmoja ya Viongozi wa Serikali ya Marekani akifurahia Umoja na Urafiki wa Tanzania na Marekani kidiplomasia,Na ameomba uendelee Kudumishwa.
Hapa akitosi Glasi na Balozi Mulamula Kuonesha Upendo na Mshikamano Miongoni Mwa Watanzania na Serikali ya Marekani.
Mh:Mwinyohaji Makame akizungumza n Watanzia hapa Washington DC kuhusu Umuhimu wa Muungano Kwa Wananchi wa Zanzibar,Amesisitiza Watanzania Wajikite kujadili maswala ya Maendeleo na sio Kuongeza Idadi ya Serikali kitu ambacho kinapoteza Muda na hakina Manufaa kwa Wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa Ujumla.Mh:Mwigulu Nchemba akizungumza n Watanzania na Wananchi wa Mataifa Mbalimbali waliofika Kusherekea Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania,Mh:Mwigulu amesema ni Wajibu kwa Kila Mmoja wetu katika Kizazi hiki kuandika historia ya kipekee kwa Kuulinda na Kuudumisha Muungano wetu kwa Miaka 50 zaidi,Kizazi kijacho kitawahukumu Watanzania endapo Muungano Utavunjika kwa Sababu tu ya Kupenda Vyeo na Ukosefu wa Utashi wa Kisiasa.
 Watanzania hawa Wakipata UKODAK kwenye sherehe za Muungano hapa Washington DC.

Nafasi ya Kupata Ukodak na Mh:Mwigulu na Mke wake(Kushoto).Viongozi wa Chama Cha mapinduzi Kutokea TEXAS.
Mh:Mwigulu Nchemba akiingia na Mh:Balozi Libereta Mulamula kwenye Usiku wa Muungano hapa Washington DC.
 Mc akiendesha Shughuli kwenye USiku wa Miaka 50 ya Muungano.
Usiku wa Muungano Umefana sana,Watanzania wapo Wamoja.Tutaulinda Muungano Wetu.
 Watanzania Wanaipenda Tanzania yao.
Viongozi wa Mataifa Mbalimbali katika Picha ya Pamoja na Balozi Libereta Mulamula,Mh:Mwigulu Nchemba na Mh:Mwinyihaji Mara baada ya Mh:Mwigulu NChemba kumaliza Kuzungumza na Watananzania.Safu ya Viongozi wa Jumuia za Watanzania kwenye Majimbo mbalimbali hapa Marekani wakiwa katika Meza ya pamoja na Mh:Balozi Mulamula na Mh:Mwigulu Nchemwa wakati wa Usiku wa Muungano hapa Washington DC.Sehemu ya Umati wa Watanzania waliofika Kwenye Usiku wa Muungano hapa Washington DC.
Usiku wa Muungano Ulipambwa na Nyimbo za Kitanzania tu,Hapa Mziki unaendelea Kusherekea Miaka 50 ya Muungano Wa Tanzania.
Mh:Mwigulu Nchemba akizunguma na Watanzania Kwenye Usiku wa Miaka 50 ya Muungano hapa Washington DC.Mwigulu amezungumzia Kuhusu Uraia Pacha na Kuwaahidi Watanzania Kuungana nao Kuipata haki hiyo Kikatiba na Chama cha Mapinduzi kimependekeza hilo kwenye Rasimu ya Katiba Mpya,Pia amezungumzia Sababu za Kiuchumi kuhusu Mzigo wa Serikali ya tatu inayopendekezwa na Rasimu huku akiwapa Uhuru Wataanzania Kutafakari kwa Kina kuhusu Jambo hilo,na Mwisho amezungumzia kuhudu dhamira ya Wazi ya UKAWA kuvuruga Mchakato wa Katiba,na dhamira hiyo imepangwa kutoa awali wakati wa Ukusanyaji wa Maoni na hata Kwenye Uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la katiba.Hivyo Kususia kwao Bunge ni jambo walilopanga na Wamelitekeleza.Mh:Mwigulu amepeleka pongezi kwa Watanzania Wote kwa Kupuuzia Kitendo hicho walichokifanya UKAWA kwsababu hakikuwa cha Kizalendo na Kimelenda Kuligawa Taifa.
 Picha/Maelezo na Sanga Festo-Washington DC
26/04/2014

MAKAMU ASKOFU ASISITIZA KATIBA BORA

$
0
0


MAKAMU wa Askofu Jimbo la Mashariki Kaskazini, Mch. Spear Mwaipopo amesema Kanisa litaendelea kuliombea Taifa na viongozi wake lakini akawataka viongozi wa nchi hii nao watimize wajibu wao kwa kutenda haki.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumapili, Aprili 27, 2014) wakati akizungumza na waumini wa Kanisa la Tanzania Assemblies of Mwenge (TAG) katika ibada ya kuadhimisha miaka 75 ya Kanisa la TAG hapa nchini.

Mchungaji Mwaipopo ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo alisema: "Kama kanisa tutaendelea kuliombea Taifa lakini na Viongozi wa nchi hawana budi kutimiza wajibu wao wa kulitendea haki Taifa letu kwa kudumisha Muungano, amani na mshikamano na kutupatia  Katiba bora inayotokana na maoni ya wananchi."

"Sasa hivi kuna mabishano ya kiitikadi yanayoendelea, na sisi tusingependa kuwa na Katiba ya Chama bali ya Watanzania wote... hakuna chama chenye watu zaidi ya milioni 45. Tukiruhusu hali hii tutakuwa hatuwatendei haki Watanzania walio wengi."

Alisema kila jambo jema husuhuka kutoka kwa Baba wa mianga na kwamba kama Kanisa wamekuwa wakiliombea jambo hilo hivyo anaamini kwamba Mungu atalisimamia hadi mwisho.

Aliwataka waumini wa Kanisa hilo kuendelea kuomba bila kuchoka. "Kwa hiyo wapendwa msiangalie malumbano tu ndani ya TV, bali endeleeni kuomba ili jambo hili aliloliazimia Bwana liweze kutimia," alisema.

Alisema anafurahishwa na ukweli kwamba kanisa la TAG linaadhimisha miaka 75 wakati Taifa la Tanzania limetimiza miaka 50 hapo jana tu (Aprili 26, 2014).

"Nawapongeza Marais wetu wastaafu hayati Mwl. Nyerere na hayati Abeid Amani Karume kwa kudumisha Muungano wetu na kuruhusu kikatiba uhuru wa wananchi kuabudu. Kudumu kwa Muungano kumetusaidia kuweza kuhubiri Injili hadi Zanzibar," alisema.

Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG - Taifa) lilianzishwa mwaka 1939 na kanisa la kwanza hapa nchini lilijengwa katika kijiji cha Igale, mkoani Mbeya.

ASIA IDAROUS AWIKA NA MAVAZI YA UBUNIFU NCHINI NIGERIA

$
0
0
Asia Idarous akiwa na vazi maalum alilolibuni ambalo lilitia fola kwenye  onyesho hilo @ Sheraton Hotel Abuja Nigeria.
Keki ya miaka 50 ya Muungano wa Tanzania, iliyoandaliwa na watanzania, Abuja Nigeria.
Fatma Mwinyi akiwa kwenye pozi katika onyesho hilo la miaka 50 ya muungano Abuja Nigeria
Tanzania family wakiwa kwenye picha ya pamoja nyumbani kwa balozi, Balozi Ole Njoolay,  Abuja Nigeria @ muunganotanzania@50.
Sheraton Hotel Abuja Nigeria presenting Fashion Tanzania @ Muungano Tanzania Inavyoonekana.
Sheraton Hotel Abuja Nigeria presenting Fashion Tanzania. ikionekana kwa ndani eneo la pool
Asia Idarous & Teddy Mapunda @Sheraton hotel Abuja Nigeria Celebrating MuunganoTanzania
Asia Idarous & Salma  wakiwa kwenye pozi
 
Na Andrew Chale wa matukiodaima.com
MBUNIFU mkongwe wa mitindo nchini, Asia Idarous Khamsin mwishoni mwa wiki aliweza kuitangaza vyema Tanzania katika onyesho  kubwa la mavazi ya ubunifu lililokuwa maalum kwa  ajili ya Maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, lililofanyika Abuja, Nigeria.
Onyesho hilo la aina yake, lililofanyika kwenye hoteli ya Kimataifa ya Nyota  tano ya Sheraton Abuja, usiku wa  April 25,  huku likiudhuriwa na watu wengi wakiwemo watanzania na raia wengine wa kigeni walioongozwa na balozi anayewaiwakilisha  Tanzania, nchini humo Balozi Daniel Ole
Njoolay.
Akizungumza na mtandao huu, kwa njia ya simu kutoka Abuja, Nigeria,  Asia Idarous ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fabak Fashions, aliwashukuru watanzania kwa kuandaa onyesho hilo maalum,  kwani limeweza kuitangaza Tanzania kwenye nyanja mbalimbali ikiwemo ya ubunifu, biashara na utalii.
"Hii ni heshima kwangu na kwa Tanzania, kwani wenzetu Wanaigeria wamevutika na bidhaa zetu nyingi zikiwemo zile tulizotumia kwenye mavazi ya ubunifu. Hivyo nasema hii ilikuwa ni nafasi ya kipekee kuwavuta kuja nchini kwa fursa za kiuchumi na uwekezaji” alisema Asia Idarous.
Alisema baadhi ya bidhaa ikiwemo khanga, vikoi, batiki na mashuka ya wamasai kutoka  Tanzania, yalitia fola na kuvutia wengi wakiwemo raia wa Nigeria na wageni wengine waliofika kwenye sherehe hizo.
Sherehe hizo mbali na kuhudhuriwa na balozi wa Tanzania, pia mabalozi mbalimbali wa mataifa wengine nao walijumuika kwa pamoja kwenye onyesho hilo.  Wengine ni pamoja na Mkurugenzi wa Montage Ltd, Teddy Mapunda, Fatma Mwinyi, Salma Maulid  na wengine wengi. 
 “Utanzania wetu ni Muungano wetu, tuulinde, tuumalishe na kuudumisha  ndani na nje ya mipaka yetu, hakika onyesho hili pia litaendelea kuwa la kuongeza tija ya umoja wetu ikiwemo watanzania waishio nje ya mipaka yao ‘Diaspora’” alisema Asia Idarous.
 Nigeria ni miongoni mwa nchi pekee zenye kudumisha utamaduni wake ukiwemo wa mavazi yenye kuwatambulisha watu wa jamii hiyo, tasnia ya ubunifu na mitindo imekuwa ikipewa kipaumbele hali inayopelekea tija  na hata Taifa hilo kuwa juu kiuchumi.
Mwisho

BREAKING NEWS...........RAIS WA ZAMANI WA KENYA DANIEL MOI AFARIKI

$
0
0

                                 Rais wa zamani wa Kenya, Daniel arap Moi

Habari  zilizotufikia  hivi  punde  kutoka nchini  Kenya  zinadai kuwa Rais mstaafu wa nchi  hiyo Daniel Arap Moi  amefariki  dunia  katika Hospital ya Aga   Khan alikokuwa  amelazwa kwa matibabu .

HABARI HII KWA UDHAMINI KWA  KITUO CHA MAFUTA IRINGA ,HOPE SERVICE STATION HAPA HUDUMA NI MASAA 24

 Wengi  hukimbilia  kununua mafuta hapa HOPE SERVICE STATION eneo la CRDB barabara ya Iringa -Dodoma katikati ya mji  wa Iringa  kituo  kinachouza mafuta masaa 24 ,wewe wasumbuka na nini  jiunge  na kituo  cha  wengi  sasa .
 KARIBU  UJAZE MAFUTA KWENYE GARI YAKO HAPA HOPE SERVICE STATION TUPO JIRANI NA BENKI YA CRDB MIYOMBONI BARABARA YA IRINGA DODOMA ,

BARAZA LA WAFANYAKAZI OFISI YA WAZIRI MKUU LAZINDULIWA

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji) Dkt. Mary Nagu akizindua Mkataba wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu mara baada ya kuzindua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, (kulia) Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Regina Kikuli  akimfafanulia jambo Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango Bw. Packshard Mkongwa wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji) Dkt. Mary Nagu (mbele mwenye mkoba) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi mara baada ya kuzindua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, (kushoto kwake tai nyekundu) Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka.picha na
Ibrahim Hamidu

MSIBA SIMBA MZEE ZAHORO AFARIKI

$
0
0

MWENYEKITI wa Klabu ya Simba, Mhe; Ismail Aden Rage(pichani), anasikitika kutangaza kifo cha Mzee Nassor Zahoro (90) kilichotokea leo nyumbani kwake mjini Bagamoyo.
 
Mzee Zahoro alikuwa mojawapo ya wana Simba maarufu hapa nchini, akiwa Mwenyekiti wa Simba Tawi la Bagamoyo kwa miaka mingi tangu enzi klabu ikifahamika kwa jina la Sunderland.
 
Sifa kubwa ya Mzee Zahoro ilikuwa ni kwenye upatanishi ambapo alihusika kwenye utatuzi wa migogoro yote iliyowahi kuikumba klabu tangu enzi za Sunderland.
 
"Mzee Zahoro alikuwa mmoja wa watu muhimu na maarufu ndani ya klabu. Kifo chake ni pengo kubwa, kubwa sana. Yeye ni sehemu ya kizazi cha wana Simba wanaoifahamu vema historia ya klabu kwa vile walizaliwa kabla ya kuanzishwa kwa klabu na wameiona katika nyakati zote.
 
"Binafsi nimemfahamu Mzee Zahoro kwa muda mrefu na nafahamu kwamba kifo chake si pengo kwa wana Simba pekee bali kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na pia kwa wananchi wa Bagamoyo ambao kwa muda mrefu walikuwa wakichota katika kisima cha hekima na buasara zake. Mungu na ailaze vema roho yo marehemu Zahoro," alisema Mwenyekiti Rage.
 
Rage ataongoza wana Simba katika mazishi ya mwanachama huyo yaliyopangwa kufanyika kesho saa saba mchana kijijini kwake Mangesani, Bagamoyo.
 
Wana Simba wote wanaombwa kujumuika katika mazishi ya mwanachama huyu maarufu.
 
 
Imetolewa  na
 
Ezekiel Kamwaga
Katibu Mkuu
Simba SC

ZIARA YA MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA, KATA YA KAWE

$
0
0

 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM, Taifa, Sadifa Juma (wapili kushoto) akiwasili kwenye Uwanja wa Mkutano eneo la Tanganyika Packers, Kawe Dar es Salaam, Jumapili, Aprili 27, 2014 ambako mbali na kuhutubia mkutano wa hadhara, alikabidhi vifaa vya michezo kwa timu mbalimbali za soka katika kata ya Kawe. Kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Kawe, Lilian Rwebangila na Katibu wa UVCCM wa kata hiyo, Aisha Katundu na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Kata hiyo Said Herry.
 Vijana wa CCM na wananchi kwa jumla wakimsindikiza Sadifa, kwa hamasa kuingia uwanjani
 Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM (Bara) Mfaume Ali Kizigo akihutubia kwenye mkutano wa hadhara wa UVCCM uliofanyika viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe Dar es Salaam, Jumapili ya Aprili 27, 2014, kumkaribisha Sadifa kuhutubia.
 Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Kawe Lilian Rwebangila akimkaribisha Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Hamis Juma, kuhutubia mkutano huo wa hadhara kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe.
 Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Hamis Juma, akihutubia mkutano wa hadhara huku shamrashamra zikitawala, kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe, Dar es Salaam, Jumapili Aprili 27, 2014.
 Sadifa akigawa vifaa vya michezo kwa kiongozi wa timu ya soka ya Ukwamani Shooting, wakati wa mkutano huo
 Mlezi wa UVCCM Kata ya Kawe, Coolman Massawe, akikabidhi vifaa vya michezo kwa kiongozi wa timu ya Ukwamani, Ali Kidogodogo, wakati wa mkutano huo
 Sadifa (kushoto) akishuhudia wakati Katibu wa CCM wilaya ya Kinondoni, Athuman Shemsha, akimtawaza Kada wa CCM, Vincet Massawe, wakati wa mkutano wa hadhara wa UVCCM  uliofanyika Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe, Dar es Salaam, Jumapili, Aprili 27, 2014

 Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Juma Hamis akimwelekeza jambo, Kamanda wa UVCCM Kata ya Kawe, Vincent Masawe wakati wa mkutano huo
 Kamanda wa UVCCM Kata ya Kawe, Masawe akishukuru kwa kupewa ukamanda huo. Kushoto ni Sadifa akimsikiliza
 Katibu wa UVCCM Kata ya Kawe, Dar es Salaam, Aisha Kitundu (katikati) akiwa na Wasanii wa Kikundi cha TOT, Malkia wa Mipasho Nchini, Khadija Kopana na Jane Komba wakati wa mkutano huo
 Viajana wa Kikosi kazi cha UVCCM Kata ya Kawe wakipozi kwa picha maalum ya kumbukumbu wakati wa mkutano huo.
 Baadhi ya viongozi wa CCM na UVCCM Kawe waliohudhuria kwenye mkutano huo. Kushoto ni Kamanda wa UVCCM Kawe,Aisha Voniatis na Mlezi wa Wazazi Muta Rwakatare
 Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM (Bara) Mfaume Ali Kizigo akiwa na viongozi wa Chipukizi, Nimka Lameck (Mwenyekiti wa Chipukizi Taifa) na Maleo Motelo (Mwenyekiti wa UVCCM Kinondoni) baada ya uzinduzi wa Tawi UVCCM la Kawe, Mnarani, Dar es Salaam, Jumapili, Aprili 27, 2014.
 Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Hamis Juma akizindua Tawi la UVCCM, Kawe Mnarani, DSar es Salaam, Jumapili, Aprili 27, 2014.
Kamanda wa UVCCM Kawe, akitoa mchango wa sh.  200,000 kwa Ktb wa tawi la UVCCM Mnarani, Mlangala Zacharia kwa ajili mradi wa maendeleo ya tawi hilo. Picha zote na Bashir Nkoromo-theNkoromo Blog

“TUNALAANI UKATILI MAOVU WANAYOFANYIWA WAANDISHI WA HABARI.” - TIBANYENDERA (MISA-TAN)

$
0
0
DSC_0085
Picha juu na chini ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN), Bw. Mohamed Tibanyendera (wa pili kushoto) akizungumza jijini Dar es Salaam jana kuhusiana maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari yatakayofanyika wiki hii duniani kote. Kushoto ni Meneja wa Maadili na Usuluhishi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Allan Lawa, Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma Ledama (wa pili kulia) na Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania (UTPC), Jane Mihanja (kulia).(Picha na Zainul Mzige).
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Zaidi ya washiriki 200 kutoka ndani na nje ya nchi wanatarajiwa kuhudhuria kwenye matukio ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, inayotarajiawa kuadhimishwa nchini hapa mnamo Mei 3, jijini Arusha, imeelezwa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN), Bw. Mohamed Tibanyendera, amesema kwamba maadhimisho hayo yenye lengo kuu la kulaani maovu wanayofanyiwa waandishi wa habari barani Afrika na duniani kote, yatafunguliwa na Jaji Mstaafu Mark Bomani.

Tibanyendera amesema kwamba, pamoja na mambo mengine maalum ambayo yatakuwa yameandaliwa, matukio ya mwaka huu yataambatana pia na uzinduzi wa kitabu kiitwacho “Hii Ndiyo Demokrasia, Toleo la 20”, kitachokuwa na taarifa muhimu kuhusu waandishi wa habari walionyanyaswa na kufanyiwa vitendo vilivyokiuka haki za binadamu, barani Afrika.
DSC_0053
DSC_0108
Meneja wa Maadili na Usuluhishi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Allan Lawa (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar kuhusu siku ya maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari itakayofanyika jijini Arusha.

“Tunategemea kuwa na wageni zaidi ya 200, kwa siku hiyo pia tuazindua kitabu kitachozungumzia waandishi walionyanyaswa na kufungwa katika maeneo mbalimbali ya Kusini mwa Afrika pamoja na hali ya vyombo vya habari na uhuru wa habari katika nchi hizo ikiwemo Tanzania,” amesema Tibanyendera.

Tibanyendera ameongeza na kusema kwamba maadhimisho hayo ya siku mbili, yatakayofanyika kuanzia Mei 2 hadi 3, yataambatana pia na utolewaji wa semina za kuwaelimisha washiriki kuhusu mambo mbalimbali ya habari na uhuru wake, kutoka kwa wataalam wakiwemo wahadhiri watakaotoka vyuo mbali mbali hapa nchini na kwingineko, ambao wameandaliwa rasmi kwa ajili ya shughuli hiyo.

Wakati huo huo, Meneja wa Maadili na Usuluhishi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) ambao pia ni moja ya taasisi zitakazoshiriki kwenye maadhimisho hayo, Bw. Allan Lawa, amesema kwamba MCT itazindua katika maadhimisho hayo machapisho matatu yatakayohusu masuala ya habari ikiwepo ripoti ya uvunjifu wa uhuru wa habari nchini ambayo yatapatikana katika ofisi zao.
DSC_0126
Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa ambao ni mmoja wa wadhamini wa siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani, Bi. Usia Nkhoma Ledama (wa pili kulia), ambaye alisisitiza kwamba uhuru wa vyombo vya habari nchini ni muhimu kusaidia nchi zinazoendela kufika malengo ya milenia.

“Sisi kama MCT tumeandaa machapisho matatu ambayo yatazinduliwa siku hiyo yanayogusia hali ya uhuru wa vyombo vya habari nchini Tanzania 2013, ripoti ya utafiti wa uvunjifu wa uhuru wa habari katika mwaka 2013, na ripoti ya ukiukwaji wa uhuru wa vyombo vya habari nchini.
“Tuna furaha kuwaambia kwamba machapisho yote haya yatapatikana siku hiyo na wote mnakaribishwa kujipatia nakala zenu,” amesema Lawa.

Akimalizia, Bw. Lawa alisema waandishi wa habari wanapaswa kufika katika ofisi za Makao Makuu ya MCT zilizopo jijini Dar es Salaam kuchukua machapisho hayo ili waweze kuyasoma kwa kina na kuweza kutambua haki zao za msingi. Alisema pia kwamba muda si mrefu, nakala za machapisho hayo zitasambazwa na kupatikana kwenye vilabu vya vyombo vya habari (Press Club) vya mikoani ili waandishi ambao wako nje ya Dar es Salaam nao waweze kunufaika na machapisho hayo.

Maadhimisho hayo yamembeba kauli mbiu ya “Uhuru wa vyombo kwa Maendeleo ya Utawala Bora”.
DSC_0144
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania (UTPC), Jane Mihanja ambaye amesema mwandishi wa habari yoyote akizuiwa kuingia kwenye mkutano ambao ni wawazi anatakiwa kutoa taarifa katika juhudi za kuhamasisha uhuru wa vyombo vya habari nchini.
DSC_0033
Pichani juu ni chini ni baadhi ya waandishi wa habari na wadau wa tasnia hiyo waliohudhuriwa mkutano huo.
DSC_0031

Waziri Mwigulu Nchemba akizungumzia suala la uraia pacha Washington DC

$
0
0
Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Nchemba akihojiana na Mubelwa Bandio wa Kwanza Production Washington DC.
Photo Credits: Habari Kwanza blog
Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Nchemba, amesema kuwa anajivunia kiasi cha UZALENDO walichonacho waTanzania hapa nchini, jambo linalompa moyo kuendeleza harakati zake za kusaidia kupatikana kwa uraia pacha, ombi lililo kuu kwa waTanzania waishio nje ya nchi katika mabadiliko ya katiba mpya.

Mhe Nchemba, ambaye alikuwa mmoja wa wageni waalikwa kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanzania yaliyofanyika jijini Washington DC nchini Marekani, amesema kuwa ushiriki wa waTanzania na rafiki zao katika maadhimisho haya, umemdhihirishia nia na mapenzi yao kwa nchi yao, na hilo limemsukuma zaidi kusaidia kupitishwa kwa suala la uraia pacha kwenye katiba mpya
Hii ni ripoti katika kipindi cha Morning Jam, asubuhi ya Aprili 28, 2014

MRATIBU WA KOMBE LA MUUNGANO MUFINDI DAUD YASSIN KUJIUZULU NAFASI YAKE ,TIMU 17 KUSHIRIKI KUMSINDIKIZA BINGWA KUMILIKISHWA KOMBE

$
0
0
Mratibu wa kombe la mUungano Mufindi 2010 Daud Yassin (kulia) akiwa na aliyekuwa mgeni rasmi katika mashindano hayo  waziri wa nchi ofisi ya waziri kiongozi (SMZ) Hamza Hassan
 Rais Jakaya Kikwete  (kushoto) akisalimiana na mratibu wa kombe la Muungano Mufindi Daud Yassin  ambae ni katibu mwenyezi wa CCM wilaya ya Mufindi hivi karibuni wa kati wa ziara yake mkoani Iringa katikati anayeshuhudia ni kamanda wa UVCCM mkoa wa Iringa Salim Asas
..........................................................................................
WAKATI Taifa likiadhimisha miaka 50 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar   wadau  wa  soka  nchini  wataanzimisha maadhimisho hayo kwa  historia kubwa katika  wilaya ya  Mufindi ambapo timu 17 zinazoshiriki zitamuaga rasmi mratibu wa kombe hilo Daud Yassin katika mashindano ya kombe la Muungano Mufindi 2014 ambapo atajiuzulu nafasi hiyo.

Akizungumza na  mtandao huu wa www.matukiodaima.com,  Yassin ambae ameratibu mashindano hayo toka  mwaka 1996 alishatangaza kujiuzulu nafasi hiyo  ili  kutoa nafasi  kwa  wadau wengine kuratibu mashindano hayo  yenye historia  kubwa hapa nchini .

Hata  hivyo  alisema  kuwa  bingwa wa mashindano hayo kwa mwaka huu atapata  zawadi ya kombe ambalo litakuwa ni mali yao ya  kudumu  ikiwa ni  kumbukumbu ya  kustaafu kwake  pia.

Alizitaja  timu 17   zilizoteuliwa kuhiriki mashindano  hayo  kwa mwaka  huu kuwa ni pamoja na  mtetezi wa  kom be hilo Maspo ya Mbeya ,Mbeya City  zote kutoka mkoa wa Mbeya , Zamaleck ya Njombetimu ya  Benki ya  wananchi Mufindi (MUCOBA) ,Igowole,sekondari, na chuo cha Veta Incoment zote za wilaya ya Mufindi timu nyingine ni Black Stars ya Iringa 

Yassin  Alisema  kuwa mashindano hayo kama  ilivyo  siku zote  yanasusisha  vijana  chini ya miaka 20yanategemea kuanza katikati ya mwezi ujao huku miongoni mwa  wadhamini wa mashindano hayo ni kampuni ya magazeti ya Mwananchi kupitia  gazeti  lake la spoti .

Serikali imetumia zaidi ya Shilingi Bilioni 111 kununua mazao kwa wakulima.

$
0
0
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula Bw. Charles akiongea na waandishi wa Habari( Hawapo Pichani) kuhusu mafanikio yaliyopatikana na wakala hao ikiwamo kutumia Zaidi ya Bilioni 111 kununua mazao kwa wakulima katika kipindi cha Mwaka 2013/2014. wakati wa Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mipango na Uendeshaji wa wakala huo Bi. Anna Mapunda.

Baadhi ya waandishi wa Habari waliohudhuria Mkutano huo wakimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula Bw. Charles wakati wa Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Leo Jijini Dar es Salaam.
Picha na Georgina Misama


Na Frank Mvungi
SERIKALI imetumia zaidi ya Shilingi Bilioni 111 kununua mazao kwa wakulima katika kipindi cha mwaka 2013/2014 ikiwa ni malipo  kwa wakulima  baada ya kuiuzia  nafaka Serikali.
Hayo yamesemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Charles Walwa wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam wakati alipokuwa akieleza mafanikio yaliyofikiwa na  wakala huo.
Walwa alisema kuwa wakala huo umeweza kuongeza kiasi cha nafaka zilizonunuliwa kutoka kwa wakulima kutoka  tani 61,587.784 mwaka 2008/2009 hadi tani 219,377.282 mwaka 2013/2014 ikiwa ni matokeo ya kuboreshwa kwa mifumo ya utendaji wa wakala huo.
“Hadi kufikia Desemba 31 mwaka 2013 wakala ulinunua tani 219,377.282 za nafaka sawa na asilimia 110 ambapo tani 218,878.600 ni mahindi na tani 498.682 ni mtama” alisema Walwa.
Aliongeza kuwa wakala umeingia makubaliano ya mashirikiano ( Memorandum  of Understanding(MOU)  na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) ili kuwahakikiishia wakulima soko la uhakika.
Katika kutekeleza makubaliano  na WFP  Walwa alisema kuwa wakala umeuza tani 80,000 mwaka 2011/2012 ambapo kwa sasa wakala unaendelea kutekeleza mkataba mwingine wa kuuza tani 23,000 kwa mwaka 2013/2014.
Katika hatua nyingineWalwa alisema kutokana na mfumo mzuri wa manunuzi ya nafaka kutoka kwa wananchi,  ajira za muda kwa wananchi takribani 3000 zizizalishwa na makundi mbalimbali ya wananchi wakati wa kukusanya nafaka tatika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula umepanga kuongeza uwezo wa kuhifadhi nafaka kutoka tani 241,000 za Sasa hadi tani  laki 400,000 ifikapo mwaka 2016 na Tani 700,000 ifikapo mwaka 2024.

Wastaafu watakiwa kuhakiki taarifa za mafao yao ya uzeeni

$
0
0
Baadhi ya waandishi wa Habari waliohudhuria Mkutano huo wakimsikiliza Meneja Uhusiano na Masoko kutoka Mfuko wa Pensheni wa PPF Bi. Lulu Mengele wakati wa Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Leo Jijini Dar es Salaam.
Picha na Georgina Misama

HOT News Basi la kampuni ya Hood inaungua moto muda huu wami watu wamepona mizigo yote imeungua

$
0
0
Basi la kampuni ya  Hood likiteketea kwa  moto  eneo la Wami na kupelekea  mizigo yote ya abiria  waliokuwa  wakisafiri na basi hilo  kuwaka moto picha na mdau wetu J Swiga

MAMA SHUJAA WA CHAKULA WAINGIA RASMI KIJIJI CHA MAISHA PLUS, PROFESA ANNA TIBAIJUKA MGENI RASMI KATIKA SHEREHE HIZO.

$
0
0
Profesa Anna Tibaijuka Waziri wa Nyumba Ardhi na  maendeleo ya Makazi wa pili kutoka kulia pamoja na Babu wa Kijiji cha Maisha Plus akiwasalimia akina mama Shujaa wa Chakula ambao wameingia Rasmi Kijiji cha Maisha Plus Jana usiku.
Akina Mama Shujaa wa Chakula Wakiwa wanamuimbia wimbo maalum Profesa Anna Tibaijuka Waziri wa Nyumba Ardhi na  maendeleo ya Makazi mara baada ya kuwasili Kijijini hapo.
Hawa ndio Mama Shujaa wa Chakula ambao jana usiku wameingia Rasmi katika Kijiji Cha Maisha Plus
Baadhi ya wageni waalikwa waliofika kushuhudia Kukaribishwa Rasmi kwa Mama shujaa wa Chakula katika Kijiji cha Maisha Plus.
Mshindi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2012 Sister Anna Mwasu wa tatu kutoka kulia akiwa katika sherehe za kuwakaribisha mama Shujaa wa Chakula ambao  wameingia rasmi katika Kijiji cha Maisha Plus Jana.
Mwakilishi kutoka Forum CC Faidhari akizungumza jambo wakati wa kuwakaribisha Mama Shujaa wa Chakula katika Kijiji cha Maisha Plus.
Teresa Yates Mwakilishi kutoka OXFAM akitoa salama za Shukurani kwa wadau wote
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mh. Ahmed Kipozi akiwakaribisha Rasmi wageni wote katika Kijiji cha Maisha plus pia kumkaribisha Mgeni Rasmi Profesa Anna Tibaijuka Waziri wa Nyumba Ardhi na  maendeleo ya Makazi  ili aweze kutoa hotuba yake
Profesa Anna Tibaijuka Waziri wa Nyumba Ardhi na  maendeleo ya Makazi wa katikati akitoa hotuba yake fupi wakati wa Sherehe za kuwakaribisha Mama Shujaa wa Chakula katika Kijiji cha Maisha Plus, katika Hotuba hiyo aliwapongeza waandaaji na wabunifu wa Shindano hilo, pia Grow kupitia OXFAM kwa kuungana na Maisha Plus kuwaleta Mama Shujaa wa Chakula, Mwisho aliahidi kuongeza Milioni 5 kwa Mama Shujaa wa Chakula atakaye nyakua ushindi, Kutoa Milioni mbili na nusu kwa Mama Shujaa wa Chakula aliyepita ili zikamsaidie katika kilimo na Mwisho Kutoa Milioni Mbili kwa Washiriki wa Shindano la Maisha Plus ambao sasa wamebakia 16 mpaka mwisho wa Shindano Tarehe 18.05.2014
Mmoja wa washiriki wa Maisha Plus akisoma Jina la Mama yake ambaye atakuwa naye katika Kipindi hiki kilicho bakia cha Shindano la Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula.

Vijana na Washiriki wa Maisha Plus wakiwa na Mama zao walezi ambao ndio wameingia Rasmi kijijini Jana
Huyu Ndiye Mama Shujaa wa Kwanza kupata nafasi ya Kuwa Markia wa Kijiji cha Maisha Plus Mary J. Mwanga, na wa kwanza kulia ni Rais wa Kijiji cha Maisha Plus Abisai Caron kutoka kenya hapa akiwa anavishwa kofia ya utambulisho na Epheta Msiga Meneja Miradi kutoka DMB
Picha ya Pamoja Mgeni Rasmi  Profesa Anna Tibaijuka Waziri wa Nyumba Ardhi na  maendeleo ya Makazi, Wakina Mama Shujaa wa Chakula, Vijana wa Maisha Plus pamoja na wadau mbalimbali waliofika katika sherehe za kuwakaribisha Mama Shujaa wa Chakula  Kijiji cha maisha Plus
Mkurugenzi Mtendaji wa DMB ambao ndio waendeshaji wa Shindano la Maisha Plus/Mama Shujaa wa Chakula Ally Masoud(Masoud Kipanya) Akitoa utaratibu wa jinsi Akina mama Shujaa wa Chakula watakavyo ishi na vijana hao katika kijiji hicho
Mama  Shujaa wa Chakula wakipata maelekezo Mbalimbali juu ya Kijiji Hicho
Moja ya Bendi Matata kutoka Bagamoyo wakiwa wanatumbuiza nyimbo Nzuri wakati wa kuwakaribisha Mama Shujaa wa Chakula katika Kijiji Cha maisha Plus

Wakipokea maelekezo kadha wa kadha
MAISHA PLUS/ MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2014

GARI LA MANISPAA YA IRINGA LAUA MMOJA

$
0
0
Mstahiki meya  manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi
Mtu mmoja  aliyetambulika kwa jina la Mika Mhemeli (16) afariki dunia baada ya kugongwa na gari la Manispaa mkoani Iringa.
 
Akizungumza na mtandao huu wa www.matukiodaima.comofisini kwake Kamanda wa polisi mkoani Iringa Ramadhani Mungi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea mnamo tarehe 27 Aprili majira ya saa 11 kamili jioni maeneo ya Kising’a Isimani barabara kuu ya Iringa – Dodoma iliyopo wilaya ya Iringa Vijijini.
 
Kamanda aliitaja gari hilo ni aina ya Toyota land Cruser lenye namba za usajili STK 5636 mali ya Manispaa ya Iringa iliyokuwa ikiendeshwa na David Kumwenda (47) mkazi wa Kihesa na kusema marehemu alifariki dunia mara baada ya kufikishwa Hospitali, hata hivyo dereva amekamatwa.
 
NA DIANA BISANGAO WA MATUKIO DAIMA.COM, IRINGA

MBUNGE MSIGWA AONYA WANAOCHAGUA VIONGOZI KWA KUPEWA CHOCHOTE ASEMA NI HATARI ,USHINDI MKUBWA KWA MSIGWA WAJA UCHAGUZI WA 2015

$
0
0
 Mbunge wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa akihutubia moja kati ya mikutano  yake mjini Iringa ................................................................
MBUNGE wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa ameonya wananchi wa  jimbo hilo na majimbo mengine nchini kuacha tabia ya  kuwachagua viongozi wanaotoa hongo ndogo ndogo ili waweze  kutawala kuwa ni hatari sana katika maendeleo yao.
Msigwa alisema  kuwa kiongozi  bora apimwe kwa uwezo  wake na sio kwa hondo ndogo ndogo anazozitoa kwa  wapiga  kura na kuwa hata kama ni yeye watamuona kama hafai wasisite kumwajibisha kwa kumnyima kura ila sio kumpa kura kwa kutegemea kupewa zawadi ndogo ndogo.
"katika baadhi ya maeneo nchini, viongozi wamekuwa wakichaguliwa kwa zawadi za thamani haba badala ya maono na uwezo wao wa kuongoza"

“Lazima tupate viongozi bora kama tunataka maendeleo, viongozi hao ni wale wanaoweza kufanya yote mawili kwa wakati mmoja, wawe na moyo wa kutoa lakini pia wenye uwezo na maono katika kuongoza,” alisema.

Akitoa mfano, alisema baadhi ya madiwani na wabunge wamechaguliwa kushika nyadhifa hizo muhimu kwa maendeleo ya wanaowachagua tu kwasababu wametoa seti moja ya jezi yenye thamani ya Sh 80,000.

Alisemwa watanzania wanatakiwa kubadilika kwa kuthaminisha vitu wanavyopewa na wanasiasa na utu wao kabla ya kutakari sababu za wao wenyewe kushindwa kununua vitu vidogo vidogo wanavyopowa kwa malengo ya kisiasa.

“Lazima tubadilike na tuachane na zile fikra za zamani za kusubiri hata mambo yaliyo ndani ya uwezo wenu yaletwe na wanasiasa,” alisema.


Alisema  iwapo  kiongozi atakuwa na fikra yakinifu za kimaendelea  atakumbukwa kwa  utendaji kazi  wake na hata pale ambapo ataondoka madarakani  maendeleo yataendelea  kuwepo

“Tukipigwa chini ubunge tuwe na mahali pengine pa kukutana na watu, na hapo si pengine zaidi maeneo ya  kimaendeleo ambayo tuliwekeza"


Mbunge Msigwa ambae  alipata kuingia madarakani mwaka 2010  kufuatia chama  cha mapinduzi (CCM) kumuengua aliyekuwa mshindi wa kura  za maoni wakati  huo Frederick Mwakalebela aliyeshinda kwa kishindo na kumpa nafasi hiyo ya kugombea mshindi wa pili Monica Mbega .

Hata  hivyo  hali ya kisiasa katika  jimbo la Iringa mjini bado si nzuri  kutokana na kuwepo kwa makundi mbali mbali ya  wana CCM ambao  wanatamani  kuwania ubunge katika  jimbo hilo hali ambayo inaweza kumuwezesha mbunge Msigwa  kushinda kwa  kishindo zaidi ukilinganisha na mwaka 2010.

Airtel yazindua whatsapp, Facebook na Twitter bure kupitia Vifurushi vya yatosha

$
0
0
Meneja Masoko wa Airtel akionyesha kipeperushi wakati wa uzinduzi wa huduma mpya itakayowawezesha wateja wa Airtel kupata whatsapp, Facebook na Twitter bure kupitia Vifurushi vya yatosha
·       Yatangaza facebook, whatsapp and twitter BURE
·       Sasa wateja kupatawhatsapp, Facebook na Twitter bure kupitia yatosha bando
  kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayoongoza kwa kutoa huduma bora imezindua huduma ya kibunifu itakayowawezesha wateja wake kupata na kuunganishwa kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook, Whatsapp na twitter BURE kupitia huduma ya Airtel yatosha
Akiongelea kuhusu huduma hiyo Mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Mallya alisema” sasa ni bure kabisa kwa wateja wetu wote wa Airtel kuunganishwa na mitandao ya kijamii ya Whatsapp, Facebook na Twitter. Airtel tunayofuraha kutoa nafasi kwa wateja wetu kuwasiliana na marafiki na familia kupitia mitandao hii ya kijamii bure bila makato yoyote, huku tukiendelea kuthibitisha kuwa Airtel Yatosha ni BABA LAO!”
Aliongeza kwa kusema mteja yoyote atakayenunua kifurushi cha data cha yatosha kuanzia sasa iwe ni cha siku, Wiki au Mwezi vifurushi vyao vya internet vya MB au GB  hazitakatwa katika matumizi ya Facebook, Whatsapp na Twitter na badala yake wataweza kutumia vifurushi vyao vya data kwenye kuperuzi katika mitandao mingine kama vile YouTube na mingine mingi kadri ya mahitaji yao”
Akiongea kuhusu namna ya kujiunga Meneja Masoko wa Airtel Bi Upendo Nkini alisema” ili kupata Whatsapp, Facebook na Twitter BURE wateja watatakiwa kupiga *149*99# kisha kuchagua kifurushi kinachowafaa na kuanza kufurahia BUREWhatsapp, Facebook na  Twitter”
“Sambamba na hilo katika kuendeleza ubunifu na kurahisiaha upatikanaji wa vifurushi vya Yatosha,  tumewawezesha wateja wetu  kutumia simu za kununua vifurushi vya yatosha kwa ajili ya marafiki zao familia na kubaki wakiwa wameunganishwa na kufurahia mitandao hii ya kijamii ya Whatsapp, Facebook na  Twitter BURE, furahia kuunganishwa katika mawasiliano kupitia mtandao wa Airtel” aliongeza Nkini

MOTO WATEKETEZA MALI ZA WAFANYABIASHARA NA SEHEMU YA JENGO LA NHC IRINGA

$
0
0


uzimaji moto huo na uokoaji ukiendelea
Ilikuwa hali tete
Wenye mali wakisaidiwa kuokoa mali zao
Shughuli yaa uokoaji iliendelea
Baadhi ya mali zilizookolewa kutoka katika jengo hilo
MOTO mkubwa ambao chanzo chake kimeelezwa kuwa ni itilafu ya umeme, umeunguza mali za wafanyabishara mbalimbali na kuteketeza sehemu ya jengo la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) lililopo jirani na kituo cha redio cha Nuru FM cha mjini Iringa.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema moto huo ulianza majira ya saa 3.45 usiku wa jana katika moja ya vyumba vya jengo hilo.
Baada ya tukio hilo kikosi cha zimamoto cha manispaa ya Iringa kiliwasili mapema na kusaidiana na baadhi ya wananchi waliojitokeza kuzima moto huo.
Hata hivyo miundombinu ya jengo hilo ilionekana kukwamisha juhudi za uzimaji wa moto huo uliokuwa ukiendelea kutambaa katika vyumba vingine.
Hadi tunakwenda mitamboni majira ya saa 5.45 usiku moto huo ulikuwa bado ikiendelea kuwaka huku jitihada za kuuzima zikiendelea.
Baadhi ya wamiliki wa maduka ya biashara katika jengo hilo walikuwa wakisaidiana na Polisi kuhamisha mali zilizosalimika.
Mali za wafanyabishara wengine katika jengo hilo akiwemo Dickson Lulandala ziliteketezwa na moto huo.

Lulandala alikuwa na ofisi inayojishughulisha na uchapishaji mkubwa na mdogo katika jengo hilo na mitambo yake ya kazi hiyo ilielezwa na mashuhuda hao kuteketezwa na moto huo.

Afisaa mkuu wa UN azuru Sudan Kusini

$
0
0

Vurugu zinashuhudiwa nchini Sudan pande za kisiasa zikizozana kuhusu mamlaka
.............................................................................................
Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la haki za binadamu , Navi Pillay yuko nchini Sudan kusini kutathmin hali huko baada ya miezi minne ya mzozo .

Ziara yake inakuja siku kadhaa tu baada ya watu wenye silaha kushambulia kambi ya Umoja wa Mataifa iliyoko Bor, na kuwauwa takriban watu 58 wakiwemo wahudumu na watoto .

Bi Pillay atakutana pia na watu walioyahama makazi yao kutokana na vita. Juma lililopita mamia ya raia waliuawa Bentiu-- mji mkuu wa jimbo lenye utajiri wa Mafuta .

Waziri wa mambo ya nje wa Sudan Kusini , Barnaba Mariel Benjamin ameiambia BBC kuwa serikali yake inataraji Umoja wa Mataifa utalaani mauaji ya raia wanayolaumiwa kuyafanya waasi .

Wakati huo huo wawakilishi wa pande husika na mzozo huo wamerejea mjini Addis Ababa Ethiopia kufufua mazungumzo ya amani

TBL KUPITIA KINYWAJI CHAKE CHA NDOVU YAHAIDI KUENDELEA KUPAMBANA NA MAUAJI YA TEMBO NCHINI.

$
0
0
  
MENEJA MASOKO WA TBL KANDA YA ZIWA UKANDA WA MAZIWA MAKUU SYLIVESTER SIZYAAKIZUNGUMZA NA WADAU WALIOHUDHURIA KATIKA USIKU WA NDOVU ULIOFANYIKA NDANI YA BAR YA CALABASH MJINI KAHAMA.

Na William Bundala
Matukio Daima Kanda ya Ziwa.
Kampuni ya Tanzania Breweries Limited kupitia kinywaji chake cha Ndovu Special Mart kimehaidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kupambana na mauaji ya Tembo Nchini.
 
Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki hii na Meneja Masoko wa Kampuni hiyo kanda ya ziwa ukanda wa maziwa makuu Sylivester Sizyaa wakati akizungumza na wadau katika tamasha la Usiku wa Ndovu linalofahamika kwa jina la Golden Networking Nights lililofanyika katika ukimbi wa Carabash mjini Kahama.
 
Sizya amesema kampuni ya TBL inathamini uwepo wa Tembo katika mbuga za wanyama nchini na kwamba ndiyo maana kinywaji hicho wakaamua kukipa jina la Ndovu hivyo wataendelea kushirikina na Serikali kwa hari na mali katika mapambano dhidi ya majangiri wa tembo.
 
Kwa upande wake mgeni rasmi wa tamasha  hilo mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya katika risala yake iliyotolewa kwa niaba yake na Katibu tarafa wa Msalala Add Mtaule amesema kuwa serikali itashirikiana na kampuni ya Tanzania Breweries kupitia kinywaji chake cha Ndovu katika kuhakikisha wanasaidia kumaliza ujangiri wa tembo ili wasipote nchini.
 
Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiashara wa kinywaji hicho mjini Kahama wamesema kuwa wataendelea kuuza kinywaji hicho kwa wateja wao ili kusaidia kufikisha ujumbe kwa watanzania wote kupitia kinywaji cha Ndovu Special Mart .
 
Tamasha la Golden Networking Nights linaloratibiwa na Kampuni ya Tanzania Breweries Limited kupitia kinywaji chake cha Ndovu special mart kila baada ya miezi mitatu lina lengo la kuwakutanisha wadau katika kufikisha ujumbe wa wa kinywaji hicho dhidi ya mapambano ya ujangili wa Tembo nchini.

MATUKIO KATIKA PICHA:

  
MWONEKANO WA NJE WA ENEO LA KARABASH ULIVYOPAMBWA NA NDOVU.

WAGENI WAARIKWA MEZA YA MGENI RASMI WAKIWA KATIKA USIKU WA NDOVU

WADAU WA NDOVU NDANI YA NYUMBA,MR MKAMA NAYE NDANI YA KIOTA.

NDOVU JAMANI RAHA SANAAAA WADAU WAKIENDELEA NA MOJA MOTO MOJA BARIDI.
WATUMIAJI WA NDOVU WAKIWA WANABADIRISHANA MAWAZO NDANI YA KIOTA CHA CARABASH

 
WADAU NDANI YA KIOTA CHA CARABASH

UKISHATUPIA NDOVU STRESS ZOTE TUPA KULEEEE NI VICHEKO TU KWA KWENDA MBELE,JAMAA ANAITWA NGIBOMBI BONIPHACE KUSHOTO AKIWA NA BEST YAKE.

MKURUGENZI WA CARABASH MR.JIMMY AKIFANYA UTAMBULISHO WA UONGOZI WA KIOTA CHAKE
MC WA SHUGHULI ALAN KABASELE KUSHOTO AKIFANYA YAKE
HAPANA CHEZEA WADAU WA NDOVU WEWEEE

PICHA YA PAMOJA KATI YA WAFANYAKAZI WA TBL,WAMILIKI WA BAR MJINI KAHAMA PAMOJA NA VIONGOZI WA SERIKALI.
MKURUGEZNI WA SOCIAL PUB MR RICHARD SOKA AKIZUNGUMZA KWA NIABA YA WAFANYABIASHARA WA BAR,

HAYA NDIYO MAMBO YA CARABASH NI UPEPO KWA KWENDA MBELE UKITUPIA NA NDOVU NI SHIDAAAAAAAAA

MBELE YA LENZI YA CAMERA YA KIJUKKUU BLOG NIKAMNASA MDAU HUYU AKIFANYA YAKE.

WAREMBO NAO WALIWAKILISHA VIZURI NDANI YA USIKU WA NDOVU.

HAPANA CHEZEA USIKU WA NDOVU NI BALAAA SANAAAA.

WADAU WA USIKU WA NDOVU WALIWAHI MAPEMAAAAA NDANI YA CARABASH

WADAU WA USIKU WA NDOVU NDANI YA CARABASH

JAMAA ANAITWA ALLY TZ TOKA KAHAMA FM KULIA AKIWA NA MDAU NDANI YA KARABASH
WADAU NDANI YA KIOTA WAKIMWEMWELEKA NA NDOVU

UWAPO NA NDO U KILA KITU KINAKUWA POUWA SANAAAA

WADAU WAKIWA WANAFANYA YAO KWA USIMAMIZI MKUBWA WA NDOVU

KWELI HAKUNA KAMA MAMA,KINA MAMA NAO WALIKUWEPO KUHAKIKISHA USIKU WA NDOVU UNAKAMILIKA

WAFANYAKAZI WA TBL WAKIFUATILIA JAMBO KWENYE PROJECTOR KUBWA NDANI YA CARABASH.

MUDA WA MSOSI UKAWADIA HAPA WADAU WAKIFANYA YAO

MSOSI WA UKWELI NDANI YA CARABASH WADAU WAKIJIPIMIA HUKU WAKISHUSHIA NA NDOVU.

ASANTE KAKA MKUBWA,HAPANA CHEZEA TBL WEWE

MMOJA MMOJA NDIYO MPANGO

MSOSI TIME NDANI YA NYUMBA CARABASH

SAMBUSA ZA UKWELI NYAMA ZA UKWELI NI HATARI SANAA

MSOSI JUMLISHA STORY JUMLISHA NDOVU USIKU UNAKUWA MTAMU SANAAA

HATARI SANAA IN TOWN

WANAOTUMIA NDOVU DAIMA WANA FURAHA SANA

FANYENI YENU MAANA NO COMMENT UKIWA NA TBL

Viewing all 2596 articles
Browse latest View live