Quantcast
Channel: Francis Godwin ::Mzee wa matukio daima::
Viewing all 2596 articles
Browse latest View live

TBC NA CRI YAZINDUA TAMTHILIYA YA KICHINA ILIYOTAFSIRIWA KWA LUGHA YA KISWAHILI

$
0
0

PIX 1 (1)Mkurugenzi Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Clement Mshana akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kwajili ya kuzindua rasmi Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika leo katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.
PIX 2 (1)Naibu Kati u Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Elisante Ole Gabriel akitoa hotuba yake mbele ya viongozi mbalimbali wakati wa Uzinduzi wa Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika leo katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.
PIX 4 (1)Mtendaji Mkuu Kampuni ya Star Media (T) Ltd Bw. Jack Czhou akieleza jambo wakati wa Uzinduzi wa Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika leo katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.
PIX 6Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Elisante Ole Gabriel akifurahi mara baada ya kukata utepe ikiwa ishara ya kukamilika kwa Uzinduzi wa Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika leo katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.
PIX 9Baadhi ya wafanyakazi toka Kampuni ya Star Media (T0 Ltd na wasanii waliotumika kuweka lugha ya Kiswahili katika Tamthiliya ya Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) wakisikiliza kwa makini hotuba toka kwa mgeni rasmi leo wakati wa Uzinduzi wa Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika leo katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.
PIX 11Picha ya pamoja ya mgeni rasmi, Watendaji na Viongozi mbalimbali mara baada ya Uzinduzi wa Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika leo katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA.
Na Benedict Liwenga – MAELEZO

SHIRIKA la Utangazaji Tanzania (TBC) na Shirika la Radio ya Kimataifa ya Jamhuri ya Watu wa China (CRI) leo kwa pamoja yameshirikiana katika sherehe ya Uzinduzi wa Tamthiliya ijulikanayo kwa jina la MAPENZI NA FURAHA YA KIJANA (Jin Tai Lang)  ambayo imechezwa na China na kuwekwa sauti kwa lugha ya Kiswahili na wasanii wa Tanzania.

Sherehe hiyo imefanyika leo katika Viwanja vya TBC ikishuhudiwa na mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Elisante Ole Gabriel akiwemo Mwakilishi wa Balozi toka Ubalozi wa China nchini Tanzania, Wajumbe wa Bodi ya Wakaurugenzi TBC, Mkurugenzi Mkuu Star Media Tanzania, Wakurugenzi na Wakuu wa Idara mbalimbali na wafanyakazi.

Hatua ya uzinduzi wa sherehe hiyo ni matokeo ya utekelezaji wa Sera ya Serikali ya kujenga mahusiano na ushirikiano na nchi rafiki kupitia nyanja mbalimbali ikiwemo habari, Utamaduni na michezo.

“Pamoja na kutekeleza sera za Serikali pia TBC tunatambua umuhimu wa kuwa na michezo ya kuigiza ambayo inazingatia utamaduni wa Watanzania na niwahakikishie kuwa Tamthiliya hizi zimeonesha hali hiyo.”. Alisema Mkurugenzi Shirika la Habari Tanzania Clement Mshana.

Mashirika ya habari ya TBC na CRI yamekuwa mstari wa mbele katika kuimarisha ushirkiano nah ii ni mara ya tatu kuwa na Tanmthiliya ya Kichina iliyowekwa sauti kwa lugha ya Kiswahili ambapo mwaka 2012 kulikuwa na tamthiliya ya MAU DOU DOU NA VISA VYA MAMA WAKWE ZAKE, ikifuatiwa na tamthiliya mbili nyingine ya MAISHA YA MAMA na FURAHA YA BABA ambazo zote zimepata umaarufu.

UONGOZI OFISI YA MAKAMO WA KWANZA WA RAIS WAZUNGUMZA NA DKT. SHEIN IKULU

$
0
0

IMG_0020Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Uongozi wa Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais katika kikao cha utekelezaji Mpango kazi wa Robo tatu ya mwaka Julai-Machi 2013/2014,katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Unguja leo asubuhi.]Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]IMG_0006Baadhi ya maafisa wa idara mbali mbali zaOfisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais wakiwa katika kikao cha utekelezaji Mpango kazi wa Robo tatu ya mwaka Julai-Machi 2013/2014,katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Unguja leo asubuhi,mwenyekiti wake akiwa ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.]Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

UTUMISHI YANYAKUA KOMBE NA KUTOA MFUNGAJI BORA MPIRA WA PETE MEI MOSI 2014

$
0
0

SAM_0156Mabingwa wapya wa Mei Mosi 2014,  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakiwa katika mazoezi mepesi kabla ya mchezo ambao waliifunga Uchukuzi na kunyaukua kombe la Mei Mosi 2014 iliyochezwa uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
SAM_0192Mchezaji wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Sophia Komba akijiandaa kumdhibiti mchezaji wa Uchukuzi (C) (mwenye mpira) katika mechi ya fainali iliyochezwa katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. 
SAM_0242Baadhi ya wachezaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi Umma, pamoja na mashabiki wao wakipongezana baada ya kuibuka mabingwa wapya wa Mpira wa Pete kwa kuifunga Uchukuzi katika mashindano ya Mei Mosi 2014 yaliyomalizika katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
SAM_0293Fatuma Machenga (GS) mfungaji bora katika Mpira wa Pete  wa mashindano ya Mei Mosi 2014 akiwa na kikombe baada ya kutangazwa rasmi katika hafla fupi iliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuru mjini Morogoro.
SAM_0361Baadhi ya wachezaji wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya  Utumishi wa Umma (jezi za kijani) wakishangilia kwa kutawazwa mabingwa wapya wa Mpira wa Pete Mei Mosi 2014 kwa kuifunga timu ya Uchukuzi. Mashindano hayo yalimalizika jana jioni katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Na James Katubuka
Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma imetawazwa rasmi kuwa bingwa wa mpira wa Pete wa Mashindano ya Mei Mosi 2014.

Utumishi imefanikiwa kuwa bingwa baada ya kuisambaratisha timu ya Wizara ya Uchukuzi kwa ushindi wa magoli 33 dhidi ya 21. Mchezo huo wa fainali ulifanyika katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Katika mchezo huo mchezaji Fatuma Machenga (GS) wa Ofisi ya Rais Utumishi ndiye aliyekua tishio kwa kuongoza wachezaji wa timu yake kufanikisha ushindi huo.

Mchezaji Subira Jumanne (WA) wa Uchukuzi akizungumzia hali ya mchezo baada ya mpira kumalizika alisema kuwa mchezo ulikuwa mgumu na wapinzani wao walikua wamejiandaa vyema.
 “Naamini wakati wa mashindano mengine tutafanya vizuri kwa kujiandaa vyakutosha, asiyekubali kushindwa si mshindani” Subira alisema.

Wakati huohuo, Fatuma Machenga (GS) wa Utumishi ameibuka kuwa mfungaji bora wa mpira wa Pete katika mashindano ya Mei Mosi 2014 kwa kufunga jumla ya magoli 136.

 “Tutahakikisha kuwa mwakani tunapambana zaidi kwa kufanya mazoezi ya kutosha ili kutetea ubingwa wetu” Machenga alisema.

Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma imenyakua kombe hilo lililokuwa likishikiliwa na timu ya Wizara ya Ulinzi iliyokuwa bingwa katika mashindano yaliyopita Mwaka 2013.
Mshindi wa Pili kwa mwaka 2014 ni Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mashindano hayo yalimalizika jana katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Wananchi waaswa kuzingatia usafi wa mazingira

$
0
0

IMG_6063Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Bw.Ernest Mamuya akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)kuhusu hatua zinazochukuliwa na Manispaa hiyo katika kuhakikisha  kuwa kanuni na taratibu za usafi wa mazingira zinazingatiwa na wananchi wote kwa kuyaweka mazingira yao katika hali  ya usafi ili kujikinga na magonjwa ya milipuko.
IMG_6115Afisa Afya wa Manispaa ya Temeke Bw.Willium Muhemu akifafanua kwa waandishi wa habari mafanikio yaliyofikiwa na Manispaa hiyo katika kuwaondoa wafanyabiashara wanaofanya biashara katika maeneo yasiyo rasmi pamoja na watu wote wanaochafua mazingira,Kulia ni Afisa Uhusiano wa Manispa hiyo Bi. Joyce Nsumba.
(Picha zote na FRANK MVUNGI-maelezo)

Na Hassan Silayo-MAELEZO
Wananchi wameaswa kuzingatia usafi wa mazingira kwa kuwa jukumu la kila mwananchi kulinda na kutunza na kuzingatia kanuni za usafi wa mazingira.

Hayo yamesemwa na Afisa Afya wa Manispaa ya Temeke Bw. Willium Muhemu wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

Bw. Muhemu alisema manispaa hiyo imeweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha kuwa kanuni za usafi, taratibu na sheria za usafi wa mazingira zinazingatiwa na wadau wote wa mazingira ili kuepusha mlipuko wa magonjwa.

“Moja ya mikakati iliyowekwa na manispaa ya Temeke ni kuhakikisha kwamba hakuna mtu anayefanya biashara katika maeneo yasiyo rasmi ili kuzuia uchafuzi wa mazingira na yeyote atakaye kiuka utaratibu huo atachukuliwa uchafuzi wa mazingira” 

Alisema  Bw. Muhemu
Naye Afisa Mazingira wa Manispaa hiyo Bw. Ernest Mamuya alisema kuwa ili kuhakikisha kuwa manispaa hiyo inakuwa katika hali ya usafi wakati wote wanao mpango mpango wa kuongeza magari ya kubeba taka , kuwa na dampo la kudumu la kuhifadhia taka na kuhakikisha taka zinazolewa kwa wakati.

Akitoa wito kwa wananchi Bw. Mamuya alisema kuwa wananchi wanapaswa kuzingatia kanuni za usafi katika ngazi za familia ili kuunga mkono mpango wa manispaa katika utunzani wa mazingira.
Maafisa afya wa kata wanaendesha zoezi la ukaguzi wa nyumba kwa nyumba kwa kushirikiana na wajumbe wa kamati za afya za mitaa husika ili kuhakikisha kuwa wananchi wanazingatia kanuni za usafi.

ASKARI 6 WAPENDA RUSHWA MBEYA WATIMULIWA

$
0
0


Kamanda wa Polisi  Mkoani Mbeya  Ahmed Msangi


Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya limewafukuza kazi Askari 6 wa kikosi cha Usalama barabarani  Wilaya za Rungwe na Mbeya kwa tuhuma za kuomba,kushawishi na kupokea rushwa.

Kamanda wa Polisi  Mkoani Mbeya  Ahmed Msangi amewatataja Askari hao kuwa ni pamoja na waliokuwa wakifanya kazi wilaya ya Mbeya barabara ya Mbeya/Tunduma eneo la Songwe ni Copro Jonson,PC Rymond na PC Simon.

Msangi amewataja wengine kuwa ni pamoja Sajini Hezron,PC Shaban na PC Kajolo ambao walikuwa wanafanya kazi barabara ya Mbeya/Rungwe wilaya ya Rungwe.

Askari hao walikuwa wanakabiliwa na makosa hayo na walifikishwa katika Mahakama ya Kijeshi na Hukumu kutolewa Aprili 24 mwaka huu na kupewa adhabu ya kufukuzwa kazi.

Aidha Kamanda Msangi amesema Jeshi lake halitasita kuwafukuza kazi Askari watakaokwenda kinyume na maadili ya Jeshi la Polisi na Askari yeyote atakayekwenda kinyume atakumbwa na adhabu kali ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi au kufikishwa mahakamani.

Askari wengine waliofukuzwa kazi hivi karibuni ni pamoja na PC James Kagomba ambaye amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa kutumia silaha,WP Prisca Kilwai anayekabiliwa na kesi ya wizi wa mtoto.

Wengine wliohukumiwa kifungo cha mwaka mmoja baada ya kukutwa na hatia ya kuua bila kukusudia ni DC Marcelino Venance mwenye namba 8084,PC Juma Idd mwenye namba 3117 na Askari wa Mgambo MG Jackson Mwakalobo ambao walidaiwa kusababisha kifo cha mwanafunzi Dentho Kajigili aliyekuwa mwanafunzi wa shule ya Sekondari Ivumwe ya Jijini Mbeya. 

Na Mbeya yetu

TANGAZO ,MALI ZINAZOSADIKIKA KUWA ZA MWANAFUNZI ZILIZOIBWA ZAOKOTWA IRINGA

$
0
0


,Mgambo wa Manispaa ya  Iringa ambao  wameokota  mali hizo  leo 
......................
Taarifa   kutoka katika ofisi ya Mgambo wa Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa zinadai kuwa  kuna mali  za mwanafunzi ambazo zimeokotwa  porini  eneo la Veta mjini Iringa hii leo .

Mali hizo ambazo ni pamoja na godoro lenye futi  2 na nusu jipya , shuka la kijani la kimasai ,raba pea 2,kitabu cha kiswahili na kiingereza kimoja , nguo za kawaida , na begi limeandikwa  spotr mfuko mwekundu wenye viatu za  michezo na  nyingine  zimeokotwa na  zinadhaniwa  kuwa ni mali zilizokuwa  zimeibwa  na kutelekezwa  hivyo kwa mzazi  yeyote mwenye mtoto  wake  ambae ameibiwa  vitu kama  hivyo anaombwa  kufika ofisi ya mgambo Manispaa ya Iringa karibu na Posta  ili kuvitambua vitu hivyo kwa mawasiliano  piga namba 0753673028 ili uwasiline na kamanda wa mgambo Manispaa ya Iringa Bw Mhanga

IRINGA YAJIPANGA KUPUNGUZA MSONGAMANO WA MAGARI

$
0
0
Manispaa ya Iringa imejiwekea mkakati wa kuandaa mipango miji pembezoni mwa mji ili kupunguza msongamano wa magari katikati ya mji wa Iringa.

Akizungumza na mtandao huu wa www.matukiodaima.comofisini kwake Afisa Mipango Miji wa Manispaa ya Iringa Bi, Immaculate Senje alisema kuwa mji wa Iringa kwa sasa umekuwa sana tofauti na enzi za miaka ya 1940 ambapo magari yalikuwa machache sana.

“mji wa Iringa ni mji mkongwe sana ambapo ulianzishwa mwaka 1940 na maeneo yaliyokuwa yanatumika ni maeneo ya Kitanzini, Gangilonga na Mshindo ambapo maeneo hayo yalipimwa miaka hiyo ya 40 na watu waliokuwa wanamiliki magari walikuwa wachache sana wengi wao walikuwa ni wafanyakazi wa Serikalini kutokana na hali hiyo hata mipango miji hawakuwa wanatenga maeneo ya kuegeshea magari”, alisema Senje.

Hata hivyo alisema kutokana na ukuaji wa mji hitaji la kutafuta eneo maalumu ambalo litakuwa ni la kuegesha magari ni muhimu sana na mpaka sasa bado wana ramani inayoonyesha hakuna maeneo husika ya kuegesha magari kwa wakazi wa Iringa na wanaotoka nje ya mkoa huu.

“kutokana na kukosa maeneo husika kwa sasa ya kuegesha magari hivyo tulilichagua eneo la barabara ile ya Uhindini iwe maalumu kwa ajili ya kuegeshea magari kwa nini tumechagua eneo hilo tuliona ni eneo ambalo lipo katikati ya mji ambapo mtu yeyote anaweza akaenda kupaki gari lake pale na akashuka akaenda sehemu aliyokuwa akihitaji kwenda na kurudi pale bila usumbufu wowote,” alisema Senje.

Afisa mipango miji huyo alisema kuwa sababu za kuzuia magari yasipake pembezoni mwa barabara ni pamoja na kuzuia ajali za barabarani pili kutoharibu barabara na grisi sababu kuna watu wengine wanatengenezea magari yao barabarani.

“changamoto za ongezeko la magari halipo Iringa peke yake bali lipo sehemu mbalimbali za miji hivyo tunachowaza kufanya kwa siku zijazo ni maeneo ya katikati ya mji yote yatajengwa magorofa na kwa atakayejenga magorofa basi aweke maeneo ya kuegeshea magari ya wateja wanaokuja kununua bidhaa maeneo hayo pia tuna mkakati wa kuanzisha miji pembezoni mwa mjini na kuweka huduma zote maeneo hayo ambapo mtu atakuwa anapata huduma zake maeneo ya hukohuko sio lazima aje mjini kwa kufanya hivyo naimani itapunguza msongamano wa magari katikati ya mji” alisema.

Hata hivyo amesema kwa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kuegeshea magari basi wamiliki wa magari hayo itabidi walipie faini kila watakapokuwa wanaegesha magari yao na kwa yeyote atakayekiuka masharti hayo basi hatua kali zitachukuliwa.

NA DIANA BISANGAO WA MATUKIO DAIMA.COM, IRINGA

PLOT YA SHIRIKA LA NYUMBA YATEKETETEA NA MOTO

$
0
0
Jeshi la polisi mkoani Iringa linawashikilia watu watatu na wengine kupoteza mali zao katika matukio manne tofauti likiwemo la nyumba plot namba 8 zone II mali ya Shirika la Nyumba kuungua na moto na kuteketeza baadhi ya mali zilizokuwemo ndani.

Akizungumza na mtandao huu wa www.matukiodaima.comofisini kwake Kamanda wa polisi mkoani Iringa Ramadhani Mungi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea mnamo tarehe 28 Aprili majira ya saa 3:45 usiku maeneo ya barabara ya Uhuru kata ya Gangilonga.
Kamanda alisema kuwa moto huo uliteketeza mali mbalimbali za wafanyabiashara waliokuwa wanahifadhi humo ndani hata hivyo thamani ya mali hizo bado haijajulikana na hakuna madhara yeyote yaliyotokea kwa binadamu.
Tukio lingine, askari wakiwa doria maeneo ya Ipogoro kata ya Ruaha waliwakamata Abdi Ally (22) na Ibrahim Aska (20) wote wakiwa ni raia wa Ethiopia kwa kosa la kuingia Nchini bila kibali.

Wakati huohuo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina Mario Sylvester (18) mkazi wa Ipogolo anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kukutwa na mashina 25 ya bhangi yaliyokuwa yamepandwa kuzunguka nyumba yake.

Tukio lingine, watu wasiofahamika waliiba pikipiki aina ya Boxer yenye namba za usajili T 909 CPZ na namba ya Engine ni PFZWDE20021 yenye thamani ya shilingi 2,150,000/= ambayo ni mali ya Raphael Kidunu (24) ambaye ni dereva na mkazi wa Kihesa.
Tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 28 Aprili majira ya saa 2 kamili usiku huko maeneo ya Kihesa Mafifi hata hivyo watuhumiwa wanatafutwa.
 
NA DIANA BISANGAO WA MATUKIO DAIMA.COM, IRINGA


HALMASHAURI NA WADAU WA JIJI LA MWANZA WAANZA MAANDALIZI YA SHEREHE ZA KUADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA JUNI 16.

$
0
0

Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi inayoundwa na wadau wa watoto jijini Mwanza Bw. Godfrey Salumu akifafanua utaratibu mzima wa utendaji kazi wa kamati ndogo ndogo zilizoundwa kwa wajumbe (hawapo pichani) ili kuweza kufanikisha maadhimisho hayo.

Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya jiji la Mwanza Bi Eluminata Mwita akisikiliza jambo kwa makini toka kwa wajumbe (hawapo pichani). 

Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Haki za Wanawake na Wasichana, KIVULINI Bw Ramadhani Masele (kushoto) ambae pia ni mjumbe wa kamati ya ndogo ya Uratibu, Mipango na Fedha akiteta jambo na mjumbe mwenzake wakati wa kikao hicho.


Wajumbe wa Kikao cha kwanza cha maandalizi ya Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika itakayofanyika Juni 16 chini ya kauli mbiu ya “Kuondoa Mila Zenye Kuleta Madhara kwa Watoto ni Jukumu Letu Sote”. 


Uongozi wa kamati ya maandalizi ya sherehe ya siku ya Mtoto wa Afrika wilaya ya Nyamagana, Mwanza. Kulia ni Bw Godfrey Salumu ambae ni Mwenyekiti wa kamati, Bw. Devis Mrope (katikati) ambae na Katibu, kushoto ni Katibu Msaidizi Bi. Francisca Michael.

HABARI NA PICHA NA HASSAN MROPE WA MATUKIODAIMA.COM, MWANZA


Halmashauri pamoja na wadau toka mashirika na taasisi za kutetea na kulinda haki za watoto jijini Mwanza wameanza rasmi vikao vya maandalizi ya kuadhimisha sherehe za siku ya mtoto wa Afrika inayoadhimishwa kila Mwaka Juni 16.
Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri wa Jiji la Mwanza chini ya Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri hiyo Bi. Eluminatha Mwita wajumbe walikubaliana kuadhimisha siku hiyo katika Kata ya Buhongwa, kwa Wilaya ya Nyamagana.
Siku ya mtoto wa Afrika huadhimishwa kimataifa kote duniani kwa lengo la kutambua thamani, utu, na umuhimu wa mtoto duniani. Maadhimisho haya hufanywa kila juni 16 tangu ilipotangazwa kuwa siku rasmi mwaka 1991 na jumuiya ya umoja wa Afrika.
Akizungumza wakati wa kufungua kikao hicho Afisa Maendeleo Jamii wa Jiji la Mwanza Bi. Eluminatha Mwita alisema kuwa kauli Mbiu ya mwaka huu ni “Kuondoa Mila Zenye Kuleta Madhara kwa Watoto ni Jukumu Letu Sote”na kufafanua kuwa kauli hiyo inalenga kuwasisitiza wazazi na walezi kuacha mila potofu zenye kuleta madhara kwa watoto.
Bi Eluminatha alisema kuwa “Kauli mbiu hiyo ina lenga kuangalia mila zote kandamizi na potofu zinazotokana na jamii husika katika malezi ya mtoto na kusababisha madhara mbalimbali ikiwemo kuongezeka kwa watoto wa mitaani, kubakwa kwa watoto, kukosa elimu, afya na malezi bora pamoja na vifo kwa watoto hawa”.
Kikao hicho cha kwanza kiliweza kuchagua viongozi wa kamati hiyo ya maandalizi, mwenyekiti aliyechaguliwa ni Godfrey Salum huku katibu ni Devis Mrope na katibu msaidizi akichaguliwa Francisca Michael, baada ya kupata viongozi kamati nne ziliundwa na wajumbe, Kamati ya Uratibu, Mipango na Fedha, Kamati ya Usafiri na Ulinzi, Kamati ya Mapambo na Burudani pamoja na kamati ya Hotuba na Habari.

 

AJALI YAUA MMOJA YAJERUHI 40 WILAYANI SUMBAWANGA

$
0
0
Na Elizabeth Ntambala
Sumbawanga
MTU mmoja amefariki dunia na wengine 40 kujeruhiwa baada ya ajali ya gari lililokuwa likitokea  katika kijiji cha Mkima Wilayani Sumbawanga kuacha njia na kupinduka na kutumbukia mtaroni.

Gari hilo aina ya Fuso lililokuwa limebeba  wachezaji wa mpira ambao walikuwa wakielekea  kijiji cha Mkima wakitokea Ilembo kwa ajili ya mechi ya kirafiki na kusababisha ajali baada ya kutumbukia mtaloni.

Kamanda wa polisi Mkoani Rukwa Jacob  Mwaruanda alisema mara baada ya gari hilo kupinduka lilisababisha kifo cha mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Hassan Enani(18) aliyekuwa kapanda juu ya bomba na kusababisha kifo chake.

Kamanda Mwaruanda aliwataja baadhi ya majeruhi waliotibiwa na kuondoka kuwa ni Edmundy Nkalawa,Henrk Kaulule,Revokatus Malambika,Philibeth Zumba,Omary Jeusha,Joel Raphael na Lukas Kang’nga.

Wengine ni Daudi Sabino,Novakatus malambika,Seris Kisanzo,Aman Shaban,Crispin Nkalawa na Menady Msumbachika  ambao wote ni wakazi wa Lembo na  walitibiwa na kuondoka katika Hospital ya Mkoa.

Jeshi la polisi  lisema kuwa mara baada ya ajali hiyo kutokea dererva huyo alitoroka na upelelezi wa awali unafanyika na mara atakapo kamatwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayiomkabili.
MWISHO

HALMASHAURI KUU YA CCM LUDEWA YAMPONGEZA MBUNGE FILIKUNJOMBE

$
0
0
 Mwenyekiti  wa CCM wilaya ya Ludewa Stanley Kolimba akifungua kikao cha Halmashauri kuu ya CCM wilaya  leo kutoka kulia ni mbunge wa jimbo la Ludewa  Deo Filikunjombe na mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa (MNEC) kutoka Ludewa Elizabeth Haule 
........................................................................................................................................
CHAMA  cha mapinduzi (CCM) wilaya ya  Ludewa  mkoani Njombe  kimempongeza mbunge wa  jimbo  hilo Deo Filikunjombe kwa  jitihada zake  mbali mbali za utekelezaji  wa ilani ya CCM katika jimbo hilo.

Pongezi  hizo  zimetolewa na mwenyekiti  wa CCM wilaya  hiyo Stanley Kolimba  wakati  akifungua  kikao  cha Halmashauri  kuu ya CCM  wilaya mjini Ludewa leo

Kolimba  alisema  kuwa mbunge utendaji kazi  wa mbunge huyo umeendelea  kuwa chachu ya  kimaendeleo  katika jimbo  hilo na  kuwafanya wananchi kuendelea kuwa na imani kubwa na CCM.

Alisema mbunge huyo amekuwa mfano wa  kuigwa katika kufanikisha utekelezaji  wa ilani ya CCM na  kudai  kuwa jitiihada kubwa zinazofanywa na Filikunjombe zitasaidia  kuwafanya  wananchi  kuendelea  kuwa na mapenzi zaidi na CCM.

"Kweli  mbunge  wetu  amekuwa ni mfano wa  kweli katika kufanikisha maendeleo ya jimbo letu na wilaya  na hata majirani wamekuwa  wakipongeza utendaji kazi  wake "

Katika  hatua  nyingine CCM  wilaya  ya  Ludewa  kimewapa pore wananchi wa kata ya Rupingu ambao wamepatwa na majanga  ya mali zao mbali mbali yakiwemo mazao kuharibiwa na mvua kubwa  zinazoendelea kunyesha katika maeneo  mbali mbali  hapa nchini.

"Mbali ya  mvua  zinazoendelea  kunyesha kusaidia  kutupa neema  ya mazao  yetu  ila wenzetu  wa Rupingu  wamepatwa na majanga  makubwa  kutokana na mvua  hizo hivyo tunawapa pore kwa majanga  haya yaliyowakuta."

Hata  hivyo  baadhi ya wajumbe  wa Halmashauri kuu ya  CCM Ludewa  walipongeza  jitihada  za  serikali ya  awamu ya nne  na jitihada za mbunge  wao katika  suala  zima la uboreshaji wa miundo mbinu katika  wilaya  hiyo ya Ludewa kutokana na kuwa na miundo  mbinu rafiki isiyosumbua sana ukilinganisha na maeneo mengine.

Pia  waliiomba serikali kwa  mwaka huu  kuangalia  uwezekano wa  kutenga  bajeti  kubwa  zaidi ya fedha kwa ajili ya ununuzi wa mahindi ya  wananchi wote  kutokana na kuwepo kwa dalili nzuri  zaidi ya wakulima katika  wilaya  hiyo  kupata mazao zaidi  ukilinganisha  na miaka iliyopita.

Kwani  walisema kutokana na jinsi ambavyo  wakulima wengi  walivyopata mazao na kulima  zaidi  upo  uwezekano  wa  wakulima  kukosa  soko la mazao  yao yote ama  wenye  fedha  ndio  watakaonufaika  zaidi na soko  hilo.

Kwa  upande  wake  mbunge Filikunjombe  aliipongeza  serikali ya Rais Jakaya  Kikwete kwa  kuendelea  kuboresha maisha ya  wana Ludewa kwa  kufungua milango  mbali mbali ya kimaendeleo ikiwa ni pamoja na kuanza  uboreshaji wa miundo mbinu ya  wilaya  hiyo.

Kwani  alisema  mbali ya kuanza  uboreshaji wa miundo mbinu  hiyo tayari  wilaya ya  Ludewa  kwa mara  ya kwanza  toka nchi ipate  uhuru  wake  mwaka 1961  kwa  kipindi  hiki ambacho amekuwa mbunge wa  jimbo  hilo tayari  wananchi  wa Ludewa  wameanza  kuona ujenzi wa barabara ya lami ukianza pamoja na  wananchi wa pembezoni ambao hawajafanikiwa kuwa na umeme  hivi sasa zoezi la kuwafikishia  umeme  limeanza.

BILA UWEKEZAJI TUNAJIDANGANYA - WAZIRI MKUU

$
0
0
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema bila uwekezaji nchi haiwezi kusonga mbele na akawataka watendaji serikalini kubadili mtazamo wao kuhusiana na suala zima la uwekezaji.
Ametoa kauli hiyo jana usiku (Jumanne, Aprili 29, 2014) wakati akizungumza na wafanyabiashara na wajasiriamali mbalimbali wa hapa nchini kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa Taasisi ya Mkoba Private Equity Fund inayojishughulisha na utoaji mitaji kwa wajasiriamali wadogo na wa kati.

"Bila uwekezaji tunajidanganya... ni ukweli usiopingika kwamba uwekezaji mkubwa unatoka kwenye sekta binafsi, kwa hiyo watendaji wetu serikalini wanapaswa kubadili mtazamo wanaposhughulikia masuala ya sekta binafsi," alisema.

Alisema watendaji serikalini wanapaswa kubadili mitazamo yao hasa wanapokuwa wanawasiliana na watu wa sekta binafsi kwa sababu kwa mfanyabiashara yeyote wakati ni mali.

"Tanzania imejipanga kuelekea kuwa Taifa lenye uchumi wa kati, kama kweli tunataka kufika huko mapema ni lazima tuwachukulie wadau wa sekta kwa mtazamo wa tofauti. Siyo anakuja kutaka taarifa unaanza kumzungusha bila sababu, anataka kusajili kampuni unamwambia unajua mafaili hayaonekani wakati hakuna cha mafaili wala nini bali unatafuta mwanya wa kudai chochote," alisema.

Akizungumzia kuhusu utoaji mikopo kwa ajili ya mitaji ya kibiashara, Waziri Mkuu aliitaka Taasisi ya Mkoba Equity Fund ihakikishe inajenga kwanza uwezo wa wahusika ili waweze kuzalisha mali kama ilivyokusudiwa.

Akitoa mfano wake binafsi, Waziri Mkuu alisema wakati anaanza biashara ya ufugaji nyuki miaka mitatu iliyopita, hakuwahi kuandaa mchanganuo wowote (write-up) wala hakuwahi kuandaa mpango wa biashara (business plan). Matokeo yake, alikuwa anatoa tu fedha mfukoni na kununua vifaa kadri mahitaji yalivyokuwa yakijitokeza, jambo ambalo alisema si sahihi.

"Ninawasihi sana viongozi wa Mkoba Equity Fund wasitoe mikopo kwa watu wanaotaka kufanya biashara kama nilivyoanza mimi. Wekezeni kwanza kwa kuwajengea uwezo wajasiriamali watakaoomba fedha za mitaji kutoka kwenye taasisi hii," alisisitiza.

Akitoa ushauri kwa wajasiriamali wadogo waliotoa shuhuda zao kuhusu changamoto walizokabiliana nazo wakati wakianzisha biashara zao, Waziri Mkuu aliwataka wasirudi nyuma wala wasikate tamaa. "Fursa ni nyingi sana na mnaweza kufanya mambo mengi. Kitu cha msingi ni kuwa na nia thabiti (determination).

Wajasiriamali walitoa shuhuda zao ni Mkurugenzi wa kampuni ya Montage, Bi. Teddy Mapunda; Mkurugenzi wa kampuni ya Go-Financing, Bw. Geoffrey Ndossi, Mkurugenzi wa kampuni ya SIGA Ltd, Bw. Marwa Busigara na Mkurugenzi wa kampuni ya WIA, Bw. Eric Mwenda.

Wafanyakazi 'Katiba na Sheria' waaswa kuchapa kazi

$
0
0




 Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo (Jumatano, Aprili 30, 2014).

 Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) Mkoa wa Dar-es-salaam Bw. Hassan Kaumo akiongea na wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo jijini Dar es Salaam leo (Jumatano, Aprili 30, 2014). Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Fanuel Mbonde. (Picha na Martha Komba - Wizara ya Katiba na Sheria).

Na Martha Komba, Dar es Salaam
Watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza ufanisi katika utendaji wao.
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Fanuel Mbonde amesema hayo katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo uliofanyika leo (Alhamisi April 30, 2014) jijini Dar-es-salaam.
 
“Uwajibikaji ni suala muhimu sana katika utumishi wa umma,” alisema katika mkutano huo wa siku moja uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar-es-salaam.
 
Aidha, Katibu Mkuu huyo aliwasihi watumishi wote wa Wizara yake kuungana na wafanyakazi wote nchini na duniani kushiriki katika sherehe za Siku ya Wafanyakazi zinazofanyika kesho (Alhamisi, Mei 1, 2014).
 
Awali akiongea katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) Mkoa wa Dar-es-salaam Bw. Hassan Kaumo aliwataka watumishi wa Wizara hiyo kutimiza wajibu wao katika sehemu zao za kazi.
 
“Tunapodai maslahi ni lazima pia tusisitize kutimiza wajibu. Wafikishieni salamu hizi wafanyakazi wote, wachape kazi ili watupe viongozi nguvu ya kudai maslahi bora,” alisema Kaumo katika mkutano huo uliohudhuriwa na viongozi na wawakilishi wa wafanyakazi kutoka Idara na Vitengo vyote vya Wizara hiyo.
  
Mkutano huo, pamoja na mambo mengine, ulijadili maslahi ya watumishi na kupitia na kuridhia Taarifa ya Mpango wa Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka ujao wa fedha 2014/2015.

TANESCO WAAMUA KUCHUKUA UAMUZI WA KUFUNGA NYAYA JUU YA MTI BAADA YA NGUZO KUVUNJIKA

$
0
0
 Nguzo hii ina zaidi ya Mwezi mmoja ikiwa ndani ya nyumba ya mtu na hatari zaidi kwa sababu imelalia katika miti mibichi
 Hivi ndivyo nguzo hiyo inavyo onekana kwa Jirani ikiwa imelalia miti
Hizi  ni waya zilizopita chini kabisa katika Geti la mtu na ndani ya miti.

 Nguzo ya umeme ya TANESCO ikiwa imekatika katika eneo la Jirani na Daraja la Mlalakuwa ambapo ipo mpaka sasa ikiwa ni zaidi ya mwezi ipo eneo hilo.
 Hii ndio Njia Mbadala waliyo iona TANESCO kutumia kwa kufunga nyaya hizo juu ya Miti baada ya kubadirisha nguzo iliyo haribika
Hizi ni nyaya za umeme ambazo zimepita Chini ,pia ni hatari kwa watembea kwa miguu
*****

Kutokana na mvua zilizonyesha hivi karibuni   jijini Dar es salaam ambapo mvua hizo zimesababisha uharibifu mkubwa wa mali na  miundo mbinu mbalimbali .

Uharibifu mkubwa na wahatari  ni katika nguzo za umeme zilizo vunjika  na baadhi ya nyaya zinazo pitisha umeme kushuka chini ambazo ni hatari kwa wananchi.

Katika eneo la Mlalakuwa  mbele kidogo baada ya kulivuka daraja ukiwa unaelekea kawe  pana nguzo tatu ambapo nguzo moja imevunjika  kabisa na nyingine mbili zimelegea  katika nguzo iliyo vunjika ni mali ya Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) liliweza kufika katika eneo hilo wakachukua hatua ya kufungua nyaya za ile nguzo iliyo katika na kuzifunga juu ya mti ulio pandwa pembeni  mti huo si mkavu ni mbichi.

Je shirika la umeme la Tanzania madhara ya umeme wananchi watayafahamu vipi wakati ninyi wenyewe wataalamu wa kazi hiyo mnatupotosha, pili sehemu mulipo fungia na nyaya zilipo legea ni sehemu watu wanapo ishi ,hivi huku nikuwajali wateja wenu ?

Tunaomba  muchukue hatua harakaiwezekanavyo ili kuepusha madhara yanayo weza kujitokeza hapo baadae  kwani ni hatari sana

DOKTA ISHENGOMA KUWA MGENI RASMI MEI MOSI

$
0
0

Mkuu wa mkoa wa Iringa Daktari Christina Ishengoma anatarajia kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi duniani yatakayofanyika kesho tarehe 1 Mei ambapo kimkoa yatafanyika katika Tarafa ya Isimani wilaya ya Iringa Vijijini.

Akizungumza na mtandao huu wa www.matukiodaima.com ofisini kwake Katibu wa Chama Cha Wafanyakazi Sekta ya Kilimo na Mifugo Bwana Deus Magessa alisema kuwa lengo la kufanya sherehe hiyo ni wafanyakazi kutoa kero zao mbalimbali zinazowakabili katika sekta zao pili kwa waajiri kuwapa zawadi wafanyakazi wao waliofanya vizuri sehemu zao za kazi pamoja na kuonyesha jinsi gani wanavyofanya kazi zao pindi wanapokuwa maofisini.

“sherehe hii ya meimosi yani siku ya wafanyakazi duniani inatarajia kuanza saa mbili asubuhi ambapo maandamano yataanza saa 3:30 mpaka saa 4:40 ambapo kamati ya maandamano na viongozi wote wa vyama vya wafanyakazi wataandamana kuelekea uwanja wa Mission Roman Katoliki Isimani ambapo sherehe hizo zitafanyikia katika huo uwanja” alisema bwana Magessa.

Hata hivyo alisema katika sikukuu hiyo kutakuwa na michezo mbalimbali kama kuvuta kamba, kukimbia na gunia, kufukuza kuku pamoja na ngumi pia alisema kwaya na ngoma mbalimbali za asili zitakuwepo.Hivyo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya kesho kuja kushiriki maadhimisho hayo kama walivyofanya mwaka jana.

Sherehe hiyo ya siku ya wafanyakazi duniani inatarajia kuanza saa mbili katika viwanja vya Mission Romani Katoliki uliopo tarafa ya Isimani na kumalizika saa 9 Alasiri huku kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni “ Utawala bora utatue kero za wafanyakazi”.

NA DIANA BISANGAO WA MATUKIO DAIMA.COM, IRINGA.


JESHI LA POLISI LINAMSHIKILIA MTU MMOJA KWA TUHUMA ZA WIZI WA NG'OMBE

$
0
0
 
Jeshi la polisi mkoani Iringa linamshikilia John Luhogo (59) kwa tuhuma za kuiba ng’ombe 15 na mbuzi 20 ambao ni mali ya Rehama Sagamiko (28) mfanyabiashara wa Wenda.
 
Akizungumza na mtandao huu wa www.matukiodaima.comofisini kwake kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea mnamo tarehe 29 Aprili majira ya saa 9 kamili Alasiri huko maeneo ya Tarafa ya Mlolo wilaya ya Iringa Vijijini.
 
Kamanda alisema mifugo hiyo yenye jumla ya Thamani ya shilingi 8,500,000/= waliibwa wakati wakiwa kwenye zizi lao ambapo mtuhumiwa huyo amekamatwa kwa mahojiano zaidi.
 
NA DIANA BISANGAO WA MATUKIO DAIMA.COM, IRINGA

Wajawazito walalamikia ‘Rushwa’ Kituo cha Afya Simambwe

$
0
0
Mbeya Vijijini

 Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Simambwe, Salome Mwaipopo (kulia) akizungumza na mwandishi wa habari hizi. Kushoto ni mmoja wa manesi wa kituo.
 Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Simambwe, Salome Mwaipopo (kulia) akizungumza na mwandishi wa habari hizi.
 Sehemu ya jengo la Kituo cha Afya Simambwe, likitoa huduma.

BAADHI ya akinamama na wanakijiji wa baadhi ya vijiji vya Kata ya Tembela Wilaya ya Mbeya Vijijini wamewalalamikia wauguzi na wahudumu wa afya katika Kituo cha Afya Simambwe kwa kile baadhi yao kuwaomba kitu kidogo (rushwa) hasa kwa wajawazito wanapofika katika kituo hicho kupata huduma.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wanawake kutoka vijiji vinavyohudumiwa na kituo hicho vya Usoha Njiapanda, Shibolya, Simambwe, Garijembe, Ilembo Usafwa, Ngoha na Zunya walisema mjamzito amekuwa akiombwa kutoa shilingi 2000 kila anapojifungulia nyumbani kwa dharura baada ya kushindwa kufika katika kituo hicho.
Mmoja wa akinamama aliyezungumza na mwandishi wa habari hizi ambaye aliomba kutotajwa kwa kuwa huenda akapata taabu kihuduma za afya kituoni hapo, alisema kwa sasa ni jambo la kawaida wahudumu kuwaomba chochote wajawazito kituoni hapo.

“…Unajua vijiji vingi vinavyohudumiwa na kituo hiki vipo mbali na miundombinu ya barabara si mizuri, yaani hakuna usafiri zaidi ya bodaboda ambazo lazima zitoke Simambwe…sasa kutokana na hali hii inatokea mjamzito anajifungulia nyumbani kwa msaada wa wakunga wa jadi, akipeleka mtoto huyo kituo cha afya basi wanamuomba shilingi 2000 haijulikani ya nini, sasa hili si tunaamini sio haki,” alisema mama huyo.

Aidha baadhi ya wanakijiji walikilalamikia kituo hicho kwa kitendo cha kulalamika muda wote hakina dawa huku wahudumu wakiwaelekezwa kwenda kununua dawa jambo ambalo wanahisi kuna mchezo mbaya unafanywa na wahudumu hao.

“Muda wote ukienda kutibiwa utasikia kauli za hakuna dawa tunakuandikia nenda kanunue, tena wengine wanaelekeza hadi maduka ya kununua dawa hizo ndio maana baadhi yetu tunahisi kuna mchezo mbaya (kuhujumu dawa) unaofanywa na baadhi ya wahudumu.,” alisema Mzee aliyejitambulisha kwa jina la Kalamwa.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Simambwe, Salome Mwaipopo  alipinga vikali uwepo wa vitendo vya kuomba rushwa kwa watumishi wa kituo hicho na kudai malalamiko kwa wanachi wanaohudumiwa na kituo hicho imekuwa kitu cha kawaida hasa wanapotembelewa na mgeni.

“..Hakuna kitu kama hicho unajua wakazi wengi wa vijiji hivi wamezoea kulalamika hasa wanapotembelewa na mgeni…hakuna wanaoombwa fedha, mjamzito akijifungua nyumbani tunampokea bila masharti na kumpatia huduma anazostahili, si kweli wanachokilalamikia,” alisema Mwaipopo.

Hata hivyo alisema kituo hicho kinahudumia idadi kubwa ya watu zaidi ya uwezo wake jambo ambalo hukifanya kuelemewa kwa idadi ya dawa wanazoletewa, wahudumu na vifaa vingine tiba hivyo kuiomba Serikali kukiongezea mgao wa dawa.

“…Kituo kinahudumia idadi kubwa ya watu kupita uwezo wake hivyo unakuta hata baadhi ya changamoto kama ufinyu wa dawa na wahudumu vinatokana na hali kama hiyo…,” alisema Mganga huyo Mkuu wa Kituo cha Afya Simambwe.

ASASI TANO KANDA YA ZIWA ZINAZOPATA RUZUKU TOKA MFUKO WA MSAADA WA KISHERIA (LSF) ZAMALIZA ZIARA YA SIKU 3 SHIRIKA LA KIVULINI

$
0
0


Maafisa Miradi pamoja na Maafisa Wakaguzi na Tathmini Miradi toka mashirika matano ya Kiraia yanayopata ruzuku kutoka Mfuko wa Msaada wa Kisheria (LSF) Tanzania, yamemaliza ziara ya kimafunzo ya siku tatu katika Shirika la Kutetea Haki za Wanawake na wasichana Tanzania, KIVULINI la jijini Mwanza, ziara iliyolenga kujifunza na kuboresha ufanyaji kazi wa mashirika hayo kupitia Miradi mbalimbali inayoendeshwa na KIVULINI.
 
Mashirika hayo matano toka mikoa ya Kagera, Shinyanga, Mara, na Tabora yalianza mafunzo hayo Jumatatu ya tarehe 28 Aprili, 2014 na kumaliza mafunzo hayo tarehe 30 Aprili, 2014 kwa kutembelea Wasaidizi wa Kisheria wanaofanya kazi ya kutoa elimu na ushauri wa kisheria katika vijiji mbalimbali vya Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba chini ya shirika la KIVULINI kupitia mradi wa Msaada wa Kisheria unaofadhiliwa na LSF.
 
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa Ziara hiyo Mkurugenzi wa Shirika la KIVULINI Bw. Ramadhan Masele aliwashukuru maafisa wote toka mikoa hiyo mitano ya kanda ya ziwa kwa kuhudhuria mafunzo hayo lakini pia aliwashukuru Mfuko wa Msaada wa Kisheria kwa heshima waliyowapa KIVULINI kuwa kituo cha mafunzo kwa asasi nyengine.
 
“Ziara hii imetoa hamasa nzuri hasa kwa upande wa kimahusiano baina ya Asasi zinazotekeleza mradi wa msaada wa kisheria kwa kanda ya ziwa, pia uzoefu tuliobadilishana kwa siku zote tatu za mafunzo naamini utaenda kuimarisha utendaji kazi wa asasi zetu na kuinua hali ya maisha ya Watanzania kupitia sisi” alisema Mkurugenzi wa KIVULINI Bw Ramadhan Masele.
 
“Lakini pia tuwashukuru wadau wetu wakubwa katika mradii huu wa msaada wa kisheria, LSF, kwa ubunifu waliouleta wa kutuwezesha kukutana pamoja na kubadilishana uzoefu katika utendaji kazi, na hivyo hivyo shukrani zetu ziende kwa Foundation for Civil Society kwa kushirkiana na SLF kuwa pamoja nasi, tunaomba huu uwe ni mwanzo tu na usiwe mwisho” alimalizia Bw Masele
 
Ziara hiyo imeratibiwa na LSF kwa kushirikiana na Foundation For Civil Society kutoa hamasa na kuinua utendaji kazi wa Asasi za Kiraia nchini katika kuhakikisha asasi hizo zinatoa matokeo bora katika mradi wa Msaada wa kisheria.
 
Mashirika yaliyohudhuria ziara hiyo ya Kimafunzo ni Jamii Salama Development Volunteers (JSDV) toka Tabora, Centre for Widows and Children Assistance (CWCA) la mkoani Mara, Mama’s Hope Organization for Legal Aid (MHOLA), Paralegal Aid Centre Shinyanga (PACESHI), Sheria na Haki za Binadamu (SHEHABITA) la mkoani Mara.
 
**********************************************************************

MWIGULU NCHEMBA "THE RISING STAR" MTANZANIA-BRUNO AFUNGUKA

$
0
0

Mtanzania Ndugu Bruno aliyekaa Upande wa Kuliya ndiye aliyeshindwa kujizuia na Kuamua kuaniaka hisia zake kuwa Mh:Mwigulu Nchemba ni "RISINGI STAR"
Ni nadra sana mtu Kusimama mbele ya Umma na Kuonesha hisia Zake kuhusu Kiongozi Flani namna anavyomkubali Kiutendaji na kufikia hatua ya Kusema anatamani Kuona Siku moja Nchi yake Inaongozwa na Kiongozi huyo.Lakini imetokea kwa Mtanzania huyu(Pichani) aliyeamua kunika hisia Zake kwa Watanzania waliokusanyika pamoja kwenye Ufunguzi wa Shina la CCM-Maryland Nchini Marekani namna anavyopendezwa na Utendaji kazi wa Mh:Mwigulu Nchemba,na kudiriki Kusema "Watamdharau,Watamdhihaki,Lakini ipo siku Watamkubali na  Atawaongoza" akatolea Mfano kuhusu Rais wa Marekani Barack Obama alivyodhihakiwa hapo awali wakatia anajiandaa Kugombea Urais awamu ya Kwanza na yapili,lakini hii leo Obama ni nani kwa Marekani?
Hivyo anasisitiza Kunahaja kwa Watanzania Kumuunga Mkono Mwigulu Nchemba katika siasa Zake kwa sababu zimejikita kutetea Watanzania,Kuimarisha Uzalendo na Kupigania Umoja na Mshikamano ndani ya Taifa letu.Angalia Video hii hapa Chini ya Mtanzania huyu (Bruno)akitoa hisia zake kwa Mh:Mwigulu nchemba.
Hii hapa Chini ndio Video iliyomgusa sana Mtanzania huyu hadi Kufikia hatua ya Kusema Mh:Mwigulu Nchemba ni Rising Star na Kiongozi Mkubwa ambaye anategemewa Kuja Kutokea katika taifa hili la Tanzania.
Angalia Vidoe hii hapa.

MEI MOSI YAFANA MKOANI MWANZA LEO

$
0
0
 Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa wakipita ya mgeni wa heshima Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng.Evarist Welle Ndikilo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi mkoa wa Mwanza ,matembezi hayo yalihitimishwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
 Wafanyakazi wa Mkemia Mkuu wa Serikali wakiingia uwanjani CCM Kirumba Mwanza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi mkoa wa Mwanza .
 Wafanyakazi wa Idara ya Maliasili wakiingia uwanjani CCM Kirumba katika kuhitimisha siku ya wafanyakazi..
 Mahakama ya Tanzania wakiingia uwanja wa CCM Kirumba huku wakitanguliza ujumbe mzito.
 Kibanda cha Veta kilikuwa moja ya vibanda vilivyovutia kwenye maonyesho ya Siku ya Wafanyakazi zilizofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza.

 Wafanyakazi wa Hospitali ya Bugando wakielekea kuingia kwenye matembezi ya mshikamano katika kusheherekea siku ya Wafanyakazi kwenye Viwanja vya CCM Kirumba.
Wafanyakazi wa Halmashauri ya Jiji Mwanza wakipita ya mgeni wa heshima Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng.Evarist Welle Ndikilo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi mkoa wa Mwanza ,matembezi hayo yalihitimishwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
Viewing all 2596 articles
Browse latest View live