Quantcast
Channel: Francis Godwin ::Mzee wa matukio daima::
Viewing all 2596 articles
Browse latest View live

Wakubaliana kusitisha vita Sudan Kusini

$
0
0


Rais Salva Kiir na Kiongozi wa waasi Riek Machar wakitia sahihi mkataba wa kusitisha vita kwa masaa 24 nchini humo.

Rais wa Sudan kusini Salva Kiir na kiongozi wa waasi nchini humo Riek Machar wametia sahihi mkataba wa kusititisha vita chini ya masaa 24.

Wawili hao pia wamekubaliana kuruhusu msaada wa kibinaadamu kungia nchini humo mbali na kubuniwa kwa serikali ya mpito.
Mazungumzo hayo yaliofanyika katika mji mkuu wa Ethiopi,a Addis Ababa yalisimamiwa na viongozi wa Shirika la IGAD pamoja na waziri mkuu nchini Ethiopia Hailemariam Desalegn ambaye ndio mwenyekiti wake.

Mwandishi wa BBC katika mazungumzo hayo amesema inatarajiwa kuonekana iwapo mkataba huo utaafikiwa kufuatia tofauti za kikabila zilizopo nchini humo ambapo maelfu ya watu wameuawa na zaidi millioni moja wengine kuachwa bila makao tangia mzozo huo uanze mnamo mwezi Disemba.

Wakati huohuo waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani John Kerry ambaye alishinikiza mkataba huo amefurahishwa na hatua hiyo.

katika taarifa yake Kerry amemuagiza rais Salva kiir na Riek Machar kuchukua hatua za haraka ili kuafikia mkataba huo na kuhakikisha kuwa vikundi vilivyojihami katika pande zote mbili vinaafikia mkataba huo.

Mpango huo unajiri baada ya ripoti ya umoja wa mataifa kuzishtumu pande zote mbili kwa kutekeleza uhalifu dhidi ya binaadamu ikiwemo mauaji ya kimbari,utumwa wa kingono pamoja na ubakaji wa kimakundi.

Afisa anayesimamia maswala ya kibinaadamu katika umoja wa mataifa Navi Pillay amesema kuwa ripoti hiyo ina maswala mengi yanayoweza kuchochea mauaji ya kimbari.

ManCity wanukia ubingwa England

$
0
0


Man City wanaelekea kileleni mwa ubingwa wa ligi ya Uingereza
Ilitarajiwa kwamba Manchester City itapiga hatua, lakini kwa mabao 4 - 0 dhidi ya Aston Villa, ilikuwa kweli mavuno yaliyowarejesha watakapo - kileleni na kuelekea ushindi wa dhahiri wa ligi ya England.

Yaya Toure ndiye aliyegonga bao hilo la mwisho, mengine wameyafunga kina Edin Dzeko mabao mawili na Stevan Jovetic bao moja.
Wakiwa na pointi 83 Man City wamewashinda Liverpool kwa pointi mbili na wingi wa mabao.

Wanachohitaji sasa ni pointi moja tu watakapokutana na West Ham hapo Jumapili ilhali Liverpool itakutana na Newcastle wakijua vyema kuwa matumaini yao ya kumaliza ukame wa kutwaa kombe hilo wa tangu miaka 24 iliyopita sasa yamefifia labda kutokee miujiza ya Man City wapoteze na wao washinde ndio waibuke na pointi 84.

Katika mechi nyengine Sunderland iliyokuwa mwanzoni inatishiwa kuteremshwa daraja wamenusurika kwa kuichapa West Brom 2-0.

Kwa matokeo hayo imeisukuma Norwich chini ya daraja, ambako imeungana na timu za Fulham na Cardiff katika safari ya kushuka daraja.

MABADILIKO UWANJA MECHI ZA RCL

$
0
0
Kutokana na marekebisho yanayofanyika katika Uwanja wa Sokoine kwa ajili ya ukaguzi wa CAF. Mechi za RCL za kituo cha Mbeya sasa zitachezwa kwenye Uwanja wa CCM Vwawa uliopo Mbozi mkoani Mbeya.
 
Boniface Wambura
Media and Communications Officer
Tanzania Football Federation (TFF)

PICHA YA MWAKA YA UTALII NCHINI TANZANIA

$
0
0


Following the pride: Lions in Tanzania spot a herd of buffalo in the distance and start walking in their direction. A safari vehicle is stationary as the predators walk past



Close encounter: Photographer Scott MacLeod captured the pack as they used the shade of the 4x4s during the hottest part of the day




In their sights: Two female lions stealthily walk in the long grass towards the herd of buffalo. A third circles closely behind them



Surrounded: The group of animals start chasing the buffalo as it begins its desperate struggle to get away



Attack: The lions begin to maul the helpless animal while it continues its attempt to break free from their grasp



Relentless: One of the lions uses its mouth to grab hold of the helpless animal's tail as they try and wrestle it to the ground



Grapple: One of the females takes the lead in the effort to bring the animal down, digging its claws into the buffalo's skin

BARAZA LA MAWAZIRI KIVULI MCHANGANYIKO (UKAWA)

PICHA; KINANA AFUNIKA IGUNGA

$
0
0

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi kwenye Uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine mjini Igunga leo, Mei 9, 2014, akiwa katika ziara ya siku kumi kukagua na kusimamia utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua na pia kuimarisha uhai wa chama mkoani Tabora
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape NNauye akizungumza kwenye mkutano huo
Maelfu ya wananchi wakinyoosha mikono kumshangilia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipohutubia mkutano wa hadhara Mei 9, 2014, kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Igunga
Mkuu wa wilaya ya Igunga mkoani Tabora Elibariki Kingu, akieleza utekelezaji wa ilani ya CCM kwenye mkutano huo wa Kinana auliofanyika, Mei 9, 2014 kwenye Uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine wilayani humo.

Kinana akirudi hotelini kwa miguu baada ya mkutano, pembeni yake ni Nape

KUIMARISHA UHAI WA CHAMA
Kinana akizindua Ofisi ya CCM tawi la Igogo, Kata ya Nanga Igunga, mkoani Tabora, leo Mei 9, 2014
 Kinana akizungumza baada ya kuzindua Ofisi hiyo ya CCM tawi la Igogo, Kata ya Nanga Igunga. Kulia ni Nape
Kinana akisalimia baadhi ya wazee baada ya kuzindua tawi hilo la CCM
Kinana akishiriki ujenzi wa nyumba ya walimu shule ya msingi Mihama, Igunga mkoani Tabora, Mei 9, 2014. Kushoto ni DC Igunga, Elibariki Kingu akisaidia kubeba tofali kumpa Katibu Mkuu Kinana.
 Kinana akiwa na bango lenye ujumbe maridhawa, kumkaribisha Kinana, alipotembelea shamba la alizeti la Vijana wajasiriamali, eneo la Iborogero, wilayani Igunga mkoani Tabora, Mei 9, 2014, ikiwa ni sehemu ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM katika muktadha wa ajira kwa vijana.
 Kinana akikagua shamba hilo la alizeti la Vijana la Iborogelo
 Kinana akitazama zao la alizeti alipokagua shamba hilo la alizeti la Vijana la Iborogelo
 HADI KULEEEE KOTE NI SHAMBA LETU: Kinana akimwambia Kinana wakati akimuonyesha shamba hilo la alizeti ambalo limesaidia vijana wa kada mbalimbali kujiajiri
 Katibu Mkuu, Kinana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na vijana wanaoshiriki mradi huo wa kilimo cha alizeti, Iborogero wilayani Igunga mkoani Tabora.
 Mwenyekiti wa Vijana SACCOS ya Igunga, Frey Cosseny (wapili kushoto) akiwatambulisha kwa Kinana maofisa wengine wa SACCOS hiyo, Mei 9, 2014 alipofika kukagua shuguli za SACCOS hiyo na kuzungumza na wanachama.
 Katibu Mkuu Kinana akiwasalimia wadau wa SACCOS hiyo
 Kinana akiendesha trekta la mradi wa Igunga Vijana Saccos kulizindua
 Kinana akishuka kwenye trekta baada ya kulizindua la Vijana SACCOS ya Igunga
Katibu Mkuu Kinana akikabidhi funguo kwa mmoja wa Wana-SACCOS hiyo, Joseph Kashindye, wakati alipokagua shughuli za SACCOS hiyo akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua katika mkoa wa Tabora, Mei 9, 2014. (Picha zote na Bashir Nkoromo

KINANA AMALIZA ZIARA WILAYA YA NZEGA KWA KUKAGUA MIRADI MUHIMU YA HUDUMA ZA JAMII NA MIKUTANO MIKUBWA YA HADHARA.LEO KUANZA ZIARA WILAYA YA UYUI

$
0
0

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishuka kutoka juu ya tanki, wakati akikagua mradi wa maji wa Itobo, wilayani Nzega, jana Mei 11, 2014, alipokuwa akiendelea na ziara yake ya siku kumi katika mkoa wa Tabora, kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiwa juu ya tanki hilo la mradi wa maji wa Itobo, wilayani Nzega, jana Mei 11, 2014, akiambatana na Kinana katika ziara ya siku kumi katika mkoa wa Tabora, kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Mamlaka ya Maji  safi katika Halmashauri ya Nzega, Samweli Buyigi (kushoto), kuhusu bwawa la chanzo cha maji kilichopo katika halmashauri hiyo ambalo limekauka kutokana na kuota magugu maji. Watatu kushoto ni Mbunge wa Nzega, Hamis Kigwangala.
Kinana akikagua chujio la maji la Mamlaka ya Majisafi Nzega mkoani Tabora, Pamoja naye ni Mbunge wa Nzega, Hamisi Kigwangala,  na anayempa maelezo ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi Nzega, Samweli Buyigi Mkurugenzi (kushoto)
 Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akijadili jambo na Kigwangala wakati akikagua miundombinu ya  Mamlaka ya Majisafi mji wa Nzega, jana Mei 11, 2014.
Mbunge wa Viti Maalum Munde Tambwe (kushoto) akimsaidia kutia mchanga kwenye mashine ya kufyatulia mafotali, Katibu Mkuu wa CCM, Kinana aliyekuwa akishiriki kufyatua matofali ya mradi wa Jumuia ya Wanawake Tanzania (UWT) wilaya ya Nzega, jana Mei 11, 2014. Kushoto ni Kigwangala
Mjunbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, Hussein Bashe, akitaja mchango wake wa fedha taslim sh. 500,000 na ahadi ya kiasi hicho hicho cha fedha kuchangia mradi wa ufyatuaji matofali wa kina mama wa UWT wilaya ya Nzega mkoani Tabora ambao umezinduliwa na Kinana (kulia), jana Mei 11. 2014. Wapili kulia ni Mbunge wa Nzega Hamis Kigwangala na Mbunge wa Bukene wilayani Nzega, Suleiman Zedi ambaye pia alichangia mradi huo sh. 500,000.
Katibu Mkuu wa CCM Kinana na wakati Mbunge wa Nzega, Kigwangala wakitangaza kutoa mchango wa sh. 500,000, wakati wa uzinduzi wa mradi huo wa ufyatuaji matofali wa UWT Nzega
Bashe na Kigwangala wakimwaga kicheko wakati wa uzinduzi wa mradi huo wa ufyatuaji matofali wa kina mama wa UWT
Jengo la kisasa la soko jipya la Kata ya Itobo, Nzega ambalo limejengwa na serikali hili karibuni na Katibu Mkuu wa CCM, Kinana kulikagua jana Mei 11, 2014
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara aliofanya jana Mei 11, 2014 katika kijiji cha Itobo wilayani Nzega
Wananchi wa Itobo wakimsikiliza kwa makini Kinana alipohutubia mkutano wa hadhara katika kijiji hicho jana Mei 11, 2014
Katibu Mkuu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape akihutubia kwenye mkutano huo wa Itobo
Wanachama wa zamani na wapya wa CCM wakilakiapo cha utii wa CCM wakati wanachama wapya zaidi ya 85 walipokabidhiwa kadi za CCM
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akitazama bwawa ambalo hutumiwa na mwananchi wa kijiji cha Bukene, katika kilimo cha mpunga cha umwagiliaji
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akiwapungia mkono wananchi alipowasili katika Uwanja wa Taifa wa Bukene, wilayani Nzega kuhutubia mkutano wa hadhara jana Mei 11, 2014, mwishoni mwa ziara yake wilayani Nzega kabla ya kuanza kesho ziara katika wilaya ya Uyui. Picha zote na Bashir Nkoromo

MKUU WA UNDP DUNIANI HELEN CLARK ATEMBELEA HIFADHI YA RUAHA,APONGEZA USIMAMIZI MZURI WA MRADI WA SPANEST

$
0
0
Mkuu wa shirika la mpango la  Maendeleo  la umoja  wa  Mataifa (UNDP ) Bi Helen Clark kulia  akiwa na madereva wa greda  ambalo  limetolewa na UNDP kwa mradi  wa
Mkuu wa shirika la mpango la  Maendeleo  la umoja  wa  Mataifa (UNDP )Hellen Clark wa  pili kulia akiwa na mkuu wa UNDP Afrika Paul Harrison kulia na mkurugenzi wa TANAPA Allan Kijazi wa nne kulia na tano  kulia ni Mratibu wa SPANEST Bw  Godwell ole Meing'ataki  watatu  kulia ni afisa mahusiano wa TANAPA Bw
Pascal Shelutete
Mkuu wa shirika la mpango la  Maendeleo  la umoja  wa  Mataifa (UNDP )Hellen Clark wa  pili kulia akiwa na mkurugenzi wa UNDP Afrika Paul Harrison kulia na mkurugenzi wa TANAPA Allan Kijazi wa nne kulia na tano  kulia ni Mratibu wa SPANEST Bw  Godwell ole Meing'ataki
Afisa utalii ofisi ya utalii Nyanda  za juu kusini Risara Kabongo akipita kando ya mtando wa kutengeneza barabara  hifadhi ya Taifa ya Ruaha  uliyotolewa na UNDP kwa mradi wa Spanest
Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi kushoto akiwa na Mkuu wa shirika la mpango la  Maendeleo  la umoja  wa  Mataifa (UNDP ) duniani Hellen Clark jana  wakati akizungumza na askari  wa hifadhi hiyo kiboko wa  majangili nchini
Mwandishi wa BBC nchini ABOUBAKARI  FAMAU   kushoto akichukua matukio nyeti  wakati mkuu wa UNDP duniani akizungumza na  askari wa hifadhi ya Taifa ya Ruaha
Mkuu wa shirika la mpango la  Maendeleo  la umoja  wa  Mataifa (UNDP )Bi Hellen Clark  kulia akizungumza na askari wa hifadhi ya Taifa ya Ruaha Iringa
Mwandishi maarufu wa ITV nchini Vedasto Msungu  akichukua matukio
Mkuu wa shirika la mpango la  Maendeleo  la umoja  wa  Mataifa (UNDP ) Hellen Clark kulia  akizungumza na askari  wanaopambana na majangili  hifadhi ya Taifa ya Ruaha  Iringa jana
Mkuu wa UNDP Hellen Clark kulia  akiwa na watendaji wa TANAPA akiwemo mratibu Mratibu wa SPANEST Bw  Godwell ole Meing'ataki wa  pili kulia na mkurugenzi wa TANAPA Allan Kijazi
Mkuu wa shirika la mpango la  Maendeleo  la umoja  wa  Mataifa (UNDP )Hellen Clark akiwa  katika  gari  lililotolewa na UNDP
Mkuu wa shirika la mpango la  Maendeleo  la umoja  wa  Mataifa (UNDP ) Hellen Clark akiwa na mkurugenzi mkuu wa TANAPA Allan Kijazi  kushoto  kando ni gari  lililotolewa msaada wa UNDP
Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi wa  tatu kushoto akiwa na Mkuu wa shirika la mpango la  Maendeleo  la umoja  wa  Mataifa (UNDP ) Helen Clark wa pili kulia na Mratibu wa SPANEST Bw  Godwell ole Meing'ataki na mratibu wa UNDP Afrika  Paul Harrison  kulia nyuma yao ni gari lililotolewa na UNDP
Wahudumu  wa Hotel ya  kisasa ya Ruaha
Ndege iliyotumiwa na  watendaji wa UNDP
Wanahabari ni watumishi wa hifadhi  ya Taifa ya Ruaha mkoani Iringa  wakiitazama ndege  aliyopanda  Mkuu wa shirika la mpango la  Maendeleo  la umoja  wa  Mataifa (UNDP )Bi Helen Clark wakati akiwasili katika  hifadhi ya Ruaha  kutembelea  miradi inayofadhiliwa na UNDP
Mkuu wa UNDP duniani Helen Clark kulia akiagana na watumishi wa  hifadhi ya Taifa  ya Ruaha leo asubuhi
Mwanahabari  wa Chanel Ten Iringa Clement  Sanga akiwa kando ya ndege ya Mkuu wa shirika la mpango la  Maendeleo  la umoja  wa  Mataifa (UNDP ) Bi Hellen Clark
Simba  akiwa amepozi wakati mwandishi wa BBC Tanzania  Aboubakari Famau akimpiga  picha katika hifadhi  ya taifa ya Ruaha mkoani Iringa  wakati wa ziara ya mkuu wa UNDP duniani Helen Clark alipotembelea  hifadhi hiyo jana
mwandishi wa BBC Tanzania  Aboubakari Famau akiwapiga  picha simba katika hifadhi  ya taifa ya Ruaha mkoani Iringa  wakati wa ziara ya mkuu  wa UNDP duniani Helen Clark alipotembelea  hifadhi hiyo jana
mwandishi wa BBC Tanzania  Aboubakari Famau akiwapiga  picha simba katika hifadhi  ya taifa ya Ruaha mkoani Iringa  wakati wa ziara ya mkuu wa UNDP duniani Helen Clark alipotembelea  hifadhi hiyo jana
Mambo  akiwa  langoni mwa hifadhi ya Ruaha mkoani Iringa
Afisa Utalii wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Risala Kabongo akimvisha skafu Kiongozi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Helen Clark baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, jana. (UNDP Administrator, Ms Helen Clark is presented with a scarf by Risala Kabongo of Tanzania National Parks (TANAPA)
UNDP Administrator is greeted by Iringa District Commissioner, Dr Leticia Warioba and other staffs of the park and TANAPA
Giving thanks
Akishukuru kwa mapokezi mazuri (Giving thanks for her arrival)
Wanahabari wakiwa kazini (Journalists at work)

Kutoka uwanja wa ndege, alisindikizwa sehemu ya mapokezi ( From the airstrip the Administrator proceeded to the rest house)
Mhifadh Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha akionesha njia (Chief Park Warden of Ruaha National Park, Dr cCristopher Timbuka shows the way) 

At rest house, Helen Clark helps herself at the self service section. Breakfast was a slap-up selection of sausage, fried eggs, breads, beans and fried bananas

UNDP Administrator together with the Director General of TANAPA, Allan Kijazi briefly speaks outside the rest house


Mkurugenzi wa UNDP Tanzania  (mwenye shati jeupe) na Naibu wake mwenye nguo nyekundu walikuwepo (UNDP Country Director, Phillippe Poinsot and his Deputy Mandisa Mashologu)

Mkuu wa wilaya na wakubwa wa TNAPA wakisikiliza (Dr Leticia Warioba (DC) and TANAPA's staffs listening )

Akisaini kitabu cha wageni Hifadhi ya Ruaha (Signing the visitors book)

RUCO MABINGWA WA POOL VYUO VIKUU NCHINI

$
0
0
Kikosi cha timu ya Ruco kikiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasili mkoani Iringa


 Meneja mauzo wa tbl mikoa ya Iringa,Njombe na Ruvuma Raymonda Degera akiwakaribisha wageni waalikwa na kuzungumza kuhusu mafanikio ya timu ya pool ya ruco.
 Nahodha wa timu ya Pool ya chuo kikuu cha Ruco , Said Mohamed akizungumza kuhusu mafanikio na changamoto mbele ya mgeni rasmi hayupo pichani
 Mgeni rasmi kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Iringa,Ramadhani Mungi akizungumza mara baada ya kukabidhiwa kikombe cha ubingwa wa pool na timu kutoka ruco



                             Na Denis Mlowe,Iringa

WANAFUNZI wa chuo kikuu cha Ruaha (RUCO) cha mkoani Iringa nchini wameshauriwa kuundeleza mchezo wa Pool sambamba na kufanya vema katika masomo yao na kuwapongeza kwa kuuletea sifa mkoa wa Iringa katika mchezo huo kwa vyuo vikuu.

Wito huo umetolewa na mgeni rasmi, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa, ACP Ramadhani Mungi katika hafla ya kuwapongeza  mabingwa wa mchezo huo kitaifa katika ngazi ya vyuo vikuu uliondaliwa na kampuni ya TBL kupitia kinywaji chake cha safari Lager na chuo cha RUCO kuchukua ubingwa kwa mara ya kwanza iliyofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Gentle Hill.

Mungi alisema wanafunzi wengi wanashindwa kuendelea na masomo kutokana na kubanwa na mambo ya burudani na michezo na kuwapongeza vijana hao kuwa na ratiba nzuri ya masomo na michezo hadi kufanikiwa kuchukua ubingwa wa vyuo vikuu kitaifa.

“Naupongeza sana uongozi wa chuo cha ruco kwa kuweka ratiba nzuri ya vipindi na michezo, utaratibu wa kujua ni wakati gani wa kusoma, wakati gani wa kufanya mazoezi hivyo bila uongozi wa chuo hicho msingefikia hapo na ndio chanzo hadi nyie kuchukua ubingwa huu na kuuletea sifa mkoa wa Iringa nawapongeza uongozi wa chuo cha ruco na vijana wangu” alisema Mungi

Alisema kuwa mchezo wa pool unazidi kukua kwa kasi kubwa nchini na lakini viongozi wake wanatakiwa kuwa makini na vijana wanaoweza kuharibu sifa ya mchezo huo hasa kwa vijana wanaofanya pool kama kijiwe cha kuvutia bangi.

Aliongeza asilimia kubwa ya vijana wanajiajiri kwa kuppitia michezo hivyo juhudi kubwa inatakiwa kuwekwa kuweza kuwawezesha vijana kuingia katika sekta ya michezo kwa kuwa ni ajira tosha katika maisha ya sasa.

Mungi alisema kupitia michezo hata uhalifu huwa unapungua kwa kuwa wengi wamekuwa wakijishughulisha hasa katika tasnia ya burudani kwa kuwa  hata wao wanapenda kujishughulisha katika michezo.

“Katika burudani uhalifu huo unapungua kwani wahalifu nao wanapenda kuburudika kwa hiyo tujitahidi sana kushughulikia michezo na burudani kuweza kupunguza uhalifu, mfano mmoja ni kuwa kuna tamasha kubwa liliwahi kufanyika hapa mkoani iringa katika kuripoti matukio siku ya pili kwa kweli polisi kulikuwa hakuna tukio lolote la uhalifu siku hiyo kwa kuwa wahalifu hao walikwenda nao kuburudika siku hiyo” alisema na kuwafanya wageni waalikwa kucheka .

Aliitaka serikali kuwa jirani na sekta ya michezo yote na kuiboresha kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana ambao asilimia kubwa hawana ajira na kuongeza kuwa michezo uleta afya ya akili na afya ya mwili hivyo ni jukumu la kila mmoja wetu kufanya mazoezi.

Mungi alivitaka vijiwe vyote vya mchezo wa pool kujiepusha na kuuza na kununua madawa ya kulevya na kuahidi kufanya msako mkali kwa kila kijiwe cha mchezo huo wanaojihusisha na biashara hiyo kwa kuwa vinajulikana na jeshi la polisi.
 
Alivitaja vijiwe vinavyojihusisaha na biashara hiyo kwa kigezo cha mchezo wa pool kuwa ni Mashine tatu, Ipogoro, Kihesa na Mlandege ndio vinaongoza kwa biashara hiyo inayoharibu sifa ya mchezo wa Pool.

Kwa upande wake nahodha wa timu ya mchezo wa Pool kutoka Ruco, Said Mohamed aliutaka uongozi wa chuo hicho kuwapa ushirikiano katika kuundeleza mchezo huo kwa kuwaandalia ratibu nzuri ya mazoezi na muda wa masomo.

Alisema kupitia mchezo huo wamefanikiwa kukitangaza chuo kitaifa na kimataifa hivyo ni jukumu la chuo sasa kuweka kipaumbele katika michezo mingine kuweza kukiletea sifa chuo na mkoa kwa ujumla.

Aliupongeza uongozi wa Tbl kuptia kinywaji cha Safari Lager kwa kudhamini mchezo huo na kuongeza soko la ajira kupitia michezo na kuutaka kuendelea  kudhamini mchezo huo.

Naye meneja mauzo mikoa ya Iringa,Njombe na Ruvuma Raymonda Degera aliwapongeza mabingwa hao na aliwataka kuongeza juhudi na maarifa ilikuweza kuuchukua tena mwakani katika mashindano mengine ya vyuo vikuu nchini wa mchezo wa pool

KATIBU MKUU OFISI YA WAZIRI MKUU AFANYA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI YA OFISI YA WAZIRI MKUU NA TAASISI ZILIZO CHINNI YA OFISI YA WAZIRI MKUU MKOANI DODODMA LEO 12 Mai 2014

$
0
0
Wakurugenzi wa Ofisi ya Waziri Mkuu waki kagua moja ya Mradi  uanao tekelezwa na ( CDA) Miradi hii nikatika   mpango wa matokeo makubwa sasa (BRN).
Katibu Mkuu Ofisi ya waziri Mkuu Dkt : Florens M Turuka  wa (katikati)  akitoa  maelekezo kwa Wakurugenzi wa OWM  walipo tembelea eneo la mradi wa Makaburi ya Viongozi  katika eneo la  Mlimani .
Kaimu  Mkurugenzi Mkuu wa  (CDA) Bw: Pascal Muragiri  akitoa maelezo ya mradi wa Barabara unaotekelezwa na CDA kwa msaada  wa  Benki  ya Dunia   wanao wakati wa Ziara ya Katibu Mkuu OWM Mkoani Dodoma
 
..............................................................................
(Na  Mwandishi Ofisi ya Waziri Mkuu)
Uongozi wa ngazi ya juu wa Ofisi ya Maziri Mkuu watembelea Miradi mbalimbali ya maendeleo inayo simamaiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
 
Akizungumza na Wakurugenzi wa Idara na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu  Dkt: Florens M. Turuka amesema lengo la kutembelea miradi ni kujionea mwenywe yeye na Wakurugenzi na wakuu wa Taasisi ili kuweza kujiridhisha na mana ya uwendelezaji wa Miradi hiyo inayao simamiwa na Serikali.
 
Miongoni mwa miradi iliyo tenmbelewa ni  Mradi wa Makaburi ya viongozi  ambapo mradi huu uko katiaka hatua za Mwisho za kukamilisha kuwalipa fidia wakazi wa eneo husiaka ili kupisha mradi huo uendelee .
 
Aidha pamoja na mradi wa makaburi pia waliweza kutembelea miradi ya upimaji viwanja vya makazi  na eneo la uwekezaji katiaka eneo la Njedengwa  njekidogo ya Manispaa ya Dododm unao tekelezwa na Mamlaka ya Uastawishaji Makao Makuu Dododma (CDA)
 
Naye kaimu Mkurugengenzi wa Mamlaka ya Ustawishaji  Makao Mkuu Dododma (CDA) Bw: Pascal  Murugiri  amesema mradi wa Njedengwa  umegarimu jumla ya ya kiasi cha Shilingi Bilioni 15 ikiwa kama mkopo kutoka benki hivyo nifursa sasa kwa wananchi  kuja (CDA) na kujipatia viwanja amabavyo viko tayari vikiwa na  huduma zote za msingi kama Barabara za lami Umeme na Maji.

NANI KUIBUKA NA MILIONI 20 KATIKA SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2014?

$
0
0
Wafuatao ni washiriki wa mashindano ya Mama Shujaa wa Chakula kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania ambao sasa wapo kijijini Maisha Plus wakiwania zawadi ya vifaa vya kilimo vyenye thamani ya Tzshs. Milioni 20.

MS 01: Elinuru M. Pallangyo - Arusha
MS 02: Dorothy D. Pallangyo - Arusha
MS 03: Leah D. Mnyambugwe - Dodoma
MS 06: Martina G. Chitete - Iringa
MS 08: Grace G. Mahumbuka - Kagera
MS 10: Zinaida J. Kijeri - Kigoma
MS 11: Upendo M. Msuya - Kilimanjaro
MS 12: Neema U. Kivugo - Manyara
MS 15: Elizabeth Simon - Morogoro
MS 16: Joyce N. Hassan - Mtwara
MS 17: Bahati Muriga - Mwanza
MS 18: Thereza Kitinga - Mwanza
MS 20: Santina Mapile - Njombe
MS 21: Mary A. Ndasi - Rukwa
MS 22: Fredina M. Said - Shinyanga
MS 23: Esther Kulwa - Simiyu
MS 24: Mary J. Mwanga - Singida
MS 25: Doricus M. Shumbi - Singida
MS 27: Kuruthum R. Mwengele - Tanga

Kumpigia kura mshiriki umpendae, andika namba yake mfano MS 00 kisha tuma kwenda +255689666662 au mtandaoni kupitia: http://voting.maishaplus.tv/index.php/voting/mamashujaa

Wekeza kwa wakulima wadogo wanawake. INALIPA.

EL- SHAMMA YAMUWEKA KAMBINI MWIMBAJI MAARUFU WA NYIMBO ZA INJILI CHINI GEORGE KAYALA

$
0
0

MWIMBAJI wa nyimbo za injili nchini, George Kayala aimeingia kambini kwa ajili ya kufanya mazoezi ya kurekodi video ya wimbo wa Siwema akiwa chini ya usimamizi wa El-Shamma Production ambayo ndiyo imechukua jukumu la kukirekodi kwa viwango vya juu kibao hicho ambayo kinafanya vizuri kwenye vituo mbalimbali vya redio nchini.

Akizungumza na mtandao huu jana, Kayala alisema kuwa El-Shamma imechukua jukumu la kumtafutia kambi ili apate muda mzuri wa kufanya mazoezi makali na vijana wake ili kuhakikisha anautendea haki wimbo huo unaomzungumzia mwanamke mrembo Siwema aliyekaidi kumgeukia Mungu wake.

“El-Shamma Production wameamua kugharamia ili niwe kambini kwa ajili yakufanya mazoezi kurekodi video ya wimbo wangu wa Siwema ambao ikimpendeza Mungu utaanza kuonekana kwenye vituo mbalimbali vya luninga nchini hivyo wanataka nifanye kazi hiyo kwa utulivu wa hali ya juu,” alisema Kayala.

Kayala alisema kuwa kambi hiyo itakuwa nje ya mkoa wa Dar es Salaam ambapo atakuwa nafanya usiku na mchana na huenda wiki ijayo kazi rasmi ya kuanza kurekodi video hiyo itaanza endapo watalidhika na ubora wa mazoezi uliofanywa.

Aidha,Kayala alisema mbali na kuingia kambini kwa ajili ya mazoezi lakini pia atakuwa anachomoka na kwenda kufanya marekebisho ya nyimbo nyingine sita ambazo bado zinamaliziwa kutengenezwa katika studio ya Best Records ya jijini Dar es Salaam.

DAR YAZIZIMA KUFUATIA KIFO CHA BALOZI FLOSSIE GOMILE CHIDYAONGA

$
0
0
DSC_0051
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Zanzibar (Muungano na Utawala Bora), Mh. Mwinyi Haji Makame, akisaini kitabu cha maombolezo mara baada ya kuwasili kuhudhuria misa maalum ya kumwombea aliyekuwa Balozi wa Malawi nchini, Mh Flossie Gomile Chidyaonga kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam.(Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).
DSC_0063
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Zanzibar (Muungano na Utawala Bora), Mh. Mwinyi Haji Makame akibadilishana mawazo na Balozi wa Nigeria nchini Tanzania Dk Ishaya Samaila Majanbu (kushoto).
DSC_0099
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb), akiwasili kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. John Haule na kulakiwa na Makamu Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Mh. Chisiza.
DSC_0106
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb), akisubiri kwenda kutia saini kitabu cha maombolezo kabla ya kuanza kwa ibada maalum ukumbini hapo. Kushoto ni Makamu Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Mh. Chisiza.
DSC_0110
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb), akisaini kwa huzuni Kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Balozi wa Malawi hapa nchini, Hayati Flossie Gomile-Chidyaonga kilichotokea Hospitali ya Aga Khan Jijini Dar es Salaam tarehe 09 mei 2014. Kulia ni Makamu Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Mh. Chisiza.
DSC_0116DSC_0123
Balozi wa Finland Tanzania, Sikka Antila wakilia kwa uchugu pamoja na Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini, Bi .Joyce Mends-Cole wakati wa misa maalum ya kumwombea aliyekuwa balozi wa Malawi nchini Tanzania Mh. Flossie Gomile Chidyaonga kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam.
DSC_0124DSC_0131
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb), akisalimiana na Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini, Bi .Joyce Mends-Cole. Katikati ni Balozi wa Finland Tanzania, Sikka Antila.
DSC_0138
Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Bi .Joyce Mends-Cole (mwenye mtandio mweupe) akibadilishana mawazo na baadhi ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania nje ya ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam.
DSC_0146
Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Balozi wa Malawi nchini Tanzania Flossie Gomile Chidyaonga ukiingizwa kwenye ukumbi tayari kuanza kwa ibada maalum na kutoa heshima za mwisho.
DSC_0167
Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Balozi wa Malawi nchini Tanzania Flossie Gomile Chidyaonga.
DSC_0169
Mchungaji akiongoza ibada maalum ya kumwombea marehemu Flossie Gomile Chidyaonga.
DSC_0184
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Bi. Tonia Kandiero (kushoto) akiwa na baadhi ya mabalozi pamoja na wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa Tanzania wakati wa ibada maalum ya kumwombea marehemu Flossi Chidyaonga iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam.
DSC_0186DSC_0189DSC_0191
Nyuso za simanzi zikiwa zimetawala ukumbini hapo.
DSC_0192DSC_0194DSC_0197
Baadhi ya waombolezaji waliohudhuria ibada msiba wa Balozi Flossie Gomile Chidyaonga.
DSC_0198DSC_0203
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard K. Membe (Mb) akiwa mwenye huzuni kubwa kwenye misa ya kumwombea marehemu Balozi Flossie Chidyaonga.
DSC_0206
Familia ya karibu ya marehemu ikiongozwa na Makamu Balozi wa Malawi nchini, Mh. Chisiza (kulia).
DSC_0219
Huzuni, simanzi na majonzi vilitawala ukumbini hapo.
DSC_0221
DSC_0222
DSC_0264
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb), akitoa mkono wa pole kwa ndugu wa karibu wa familia ya marehemu mara baada ya kutoa heshima za mwisho.
DSC_0277
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha-Rose Migiro akitoa mkono wa pole familia ya balozi Flossie Gomile Chidyaonga.
DSC_0284
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akitoa mkono wa pole kwa wafiwa.
DSC_0289
DSC_0299
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Bi. Tonia Kandiero, akitoa mkono wa pole kwa wafiwa.
DSC_0308
Balozi wa Zambia hapa nchini, Mhe. Judith Kangoma Kapijimpanga, akishindwa kujizuia wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Balozi wa Malawi hapa nchini Hayati Flossie Gomile-Chidyaonga.
DSC_0318
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Mh. Filiberto Sebregondi, akitoa heshima zake za mwisho.
DSC_0324
DSC_0327
DSC_0333
Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Bi .Joyce Mends-Cole, akitoa pole kwa wafiwa.
DSC_0382
DSC_0387
DSC_0394
DSC_0380
DSC_0410
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania , Mizinga Melu,(wa tatu kulia) , Balozi wa Zambia hapa nchini, Mhe. Judith Kangoma Kapijimpanga (wa pili kulia) wakati wa misa maalum ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Balozi wa Malawi hapa nchini Hayati Flossie Gomile-Chidyaonga.
DSC_0407

DC KAHAMA ACHIMBA MKWARA MZITO KWA WANANCHI NA VIONGOZI WANAOJADILI HOTUBA ZAKE.

$
0
0
MH BENSON MPESYA
 
 Na  Wiliam Bundala  matukiodaima.com kanda ya  Ziwa 

Mkuu wa wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Benson Mpesya amewapiga marufuku wananchi na viongozi mbalimbali wilayani humo kuacha mara moja kuwa wanajadili hotuba zake kwa madai anapozitoa wajue ni tamko la serikali.

Marufuku hiyo ameitoa jana wakati akiongea na watumishi wa halmashauri ya ushetu wakiwa ni pamoja na baadhi ya madiwani  wa halmashauri hiyo ambapo amesema wamekuwa na tabia mbovu ya kuanza kujadili hotuba zake ambazo huzitoa katika maeneo mbalimbali.

Amesema tabia hiyo ni mbovu na kama itaendelea ataanza kuchukua hatua kwa mjibu wa sheria akitumia rungua lilopewa na Rais wa nchi kwa kuwa mamlaka hayo anayo na hakuna atakaye muuliza akianza kuwachukulia hatua watu hao.

Imedaiwa baadhi ya madiwani katika halmashauri hiyo ya ushetu wamekuwa wakiunda vikundi kupinga maelekezo  yake wakati akiyatoa kupitia hotuba zake hali ambayo ilimkera na kuamua kuwapiga marufuku kujadili hotuba zake .

Katika madai hayo madiwani hao wamekuwa wakipinga hasa kisiasa wakiona hotuba zake hizo zinawalenga wananchi katika michango mbalimbali ya maendeleo hali ambayo inapingana  na yeye kwa kuwa majukumu yake yeye ni ya kiserikali juu ya kuleta maendeleo ya wananchi.

Kufuatia hali hiyo mkuu huyo wa wilaya amesema ni utovu wa nidhamu kuingiza siasa kwenye utendaji wa serikali huku akisema kwa kuyasema hayo moyo wake umefunguka anaweza sasa kuongea nao juu maendeleo kwa kuwa kilichokuwa kinamkera hotuba zake kujadiliwa nje ya kikao.

Pamoja na hayo Mpesya ametumia nafasi hiyo kuwaonya vikali watumishi wanaotumia Elimu zao kuwakandamiza wananchi wa kijijini wasiokuwa na Elimu ama upeo wa kugeuza haki zao kuwa mitaji hali ambayo wale watakao bainika cha moto watakiona wakiwemo idara ya afya.

NEEMA YASHUKA LUDEWA MKATABA WA MABILIONI KUBORESHA BARABARA WASAINIWA , MBUNGE FILIKUNJOMBE AMUMWAGIA SIFA WAZIRI DR MAGUFULI

$
0
0
Mbunge  wa  jimbo la Ludewa  Deo Filikunjombe akimpongeza  waziri Dr Magufuli kwa  uchapakazi  wake

 Zoezi la makandarasi kusaini mkataba  wa uboreshaji wa barabara  jimbo la Ludewa  likifanyika jana
 Mkuu  wa  mkoa  wa Njombe Aser Msangi katikati akiwa na mbunge wa  jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe wa  pili  kushoto  waliokaa na mkuu wa wilaya ya Njombe Sarah Dumba,wa pili kulia ni Mhandisi Patrick Mfugale, na wawakilishi wa wakala wa  barabara  Njombe na mwakilishi  wa wizara ya ujenzi ,pamoja na makandarasi  walioingia mkataba  
...........................................................................................................................................


MBUNGE wa  jimbo la  Ludewa Deo Filikunjombe amempongeza  waziri wa Ujenzi Dk. John Pombe Magufuli kwa  uchapa kazi na  kutaka mawaziri mizigo wasiowajibika katika wizara zao kujiwajibisha  wenyewe kwa  kujiuzulu nafasi zao .

Amesema  kuwa wapo  baadhi ya  mawaziri ambao  wamekuwa wakifanya kazi kwa  kujisikia  huku  wizara  zao  zikiwa na changamoto mbali mbali na pale  wanaponyoshewa  vidole na  wabunge na wananchi bado wamekuwa  waking'ang'ania nafasi zao badala ya  kuwapisha  wenye uwezo wa kufanya kazi.

Akizungumza  katika hafla ya utiaji saini baina ya wakala wa Tanroad Mkoa wa Njombe na Wakandarasi wanne wazalendo kwa ajili ya ukarabati mkubwa wa barabara ya Itoni-Ludewa-Manda yenye kilomita 211.4, kwa kiwango cha changarawe kwa gharama ya sh. 7.8 bilioni, uliofanyika juzi  mjini Njombe mbunge  Filikunjombe  alisema anampongeza  waziri Dr Magufuli kwa amekuwa mfano wa utendaji kwa mawaziri  wengine .




“Napenda nichukue nafasi hii kumpongeza  zaidi waziri wa wizara ya ujenzi Dk. John Magufuli kwa kazi anayoifanya, kule bungeni huwa tunasema kuna mawaziri mizigo, lakini napenda kumtoa Waziri Magufuli katika orodha hiyo, Magufuli ni hodari ni mchapa kazi  na mimi nampenda, kama tungekuwa na mawaziri watano tu kama yeye tungefika mbali sana,”



Alisema  kuwa ujenzi  huo wa barabara umefungua  milango ya mawasiliano katika wilaya ya Ludewa kwa kujenga barabara kwa kiwango cha changarawe ili kuwezesha kupita kwa mitambo mikubwa ya uchimbaji wa madini ya makaa ya mawe Mchuchuma na chuma cha Liganga, hatua ambayo alisema itatoa fursa mbalimbali za ajira kwa wakazi wa Ludewa na mkoa  mzima wa Njombe .

Kuhusu makandarasi waliopewa kazi hiyo Filikunjombe aliwataka makandarasi hao  wazawa waliopewa kazi ya kupanua barabara hiyo kwa kiwango cha changarawe kuwa wazalendo wa kweli kwa kukarabati barabara hiyo kwa kiwango kinachotakiwa badala ya  kufanya  chini ya  kiwango.


Wakati mtendaji Mkuu wa Wakala wa barabara nchini Tanroads Mhandisi Patrick Mfugale, alisema kutokana na umhimu wa barabara hiyo kwa ajili ya ukuaji wa uchumi wa nchi kutokana na kuwepo kwa fursa za madini ya makaa ya mawe na chuma, serikali inakusudia kuijenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami. 

Alisema  kwa sasa Tanroads kwa niaba ya serikali imeingia mkataba na mhandisi mshauri Crown  Tech Consult Ltd kwa gharama ya sh.  1.782 bilioni kwa ajili ya upembuzi akinifu, usanifu wa kina na uandaaji wa makabulasha ya zabuni na kuanza kujenga barabara hiyo kuanzia Itoni hadi Manda.
Alisema kazi hiyo itajumuisha maeneo ya Mkiu hadi Linganga yaliko madini ya chuma na Nchuchuma yaliko madini ya makaa ya  mawe, kubainisha kuwa kazi hiyo itaanza mwaka wa fedha ujao.

Mfugale alisema  kwa sasa wameamua kujenga barabara hiyo kwa kiwango cha changarawe baada ya kuapata taarifa kuwa mwezi Juni mwaka huu kuna mitambo mizito ambayo itapitishwa kwa ajili ya migodi ya chuma na makaa ya mawe, ambapo hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Rais Jakaya Kikwete kufuatia ziara yake aliyoifanya mkoani hapa mwishoni mwa mwaka jana, huku akiwataka wakandarasi hao kumaliza ukarabati huo kwa wakati na kiwango kinachotakiwa, ambapo wanatakiwa kukamilisha kazi hiyo ifikapo Julai 12 mwaka huu.

“Makandarasi naomba muelewe kuwa mmepewa heshima kubwa kama wazalendo naomba muifanye kazi hii kizalendo kwa ubora umahiri na umakini, kwanza kwa kuanza kazi na kumaliza kazi katika muda wa miezi miwili tuliokubaliana kuanzia leo (Mei 12) au kabla ya hapo. Kama unaona huwezi usisaini mkataba huu leo,” alisema Mhandisi Mfugale.

 Wakandarasi waliopewa tenda ya hiyo ni Mtwivila Traders Contraction eneo la Mkiu-Ludewa kilomita 60 sh. 1.6 bilioni,  GS Contractors  eneo la Ludewa –Mkomang’ombe – Nchuchuma kilomita 37  sh. 1.6 bilioni na Canopies  eneo la Mkiu- Linganga kilomita 46 sh. 1.7 bilioni na Boimanda Modern Company Ltd atajenga eneo la Itoni-Mkiu kilomita 68 kwa gharama ya sh. 2.7 bilioni,

Aidha alisema kutokana na umhimu wa barabara hiyo kwa ajili ya ukuaji wa uchumi wa nchi kutokana na kuwepo kwa fursa za madini ya makaa ya mawe na chuma, serikali inakusudia kuijenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami.

"Kwa sasa Tanroads kwa niaba ya serikali imeingia mkataba na mhandisi mshauri Crown  Tech Consult Ltd kwa gharama ya sh.  1.782 bilioni kwa ajili ya upembuzi akinifu, usanifu wa kina na uandaaji wa makabulasha ya zabuni na kuanza kujenga barabara hiyo kuanzia Itoni hadi Manda."

Kazi hiyo itajumuisha maeneo ya Mkiu hadi Linganga yaliko madini ya chuma na Nchuchuma yaliko madini ya makaa ya  mawe, kubainisha kuwa kazi hiyo itaanza mwaka wa fedha ujao.

Uamuzi  wa  kujenga barabara hiyo kwa kiwango cha changarawe umetokana na  taarifa mwezi Juni mwaka huu kuwa kuna mitambo mizito ambayo itapitishwa kwa ajili ya migodi ya chuma na makaa ya mawe, ambapo hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Rais Jakaya Kikwete kufuatia ziara yake aliyoifanya mkoani hapa mwishoni mwa mwaka jana, huku akiwataka wakandarasi hao kumaliza ukarabati huo kwa wakati na kiwango kinachotakiwa, ambapo wanatakiwa kukamilisha kazi hiyo ifikapo Julai 12 mwaka huu.


TUTAENDELEA KUISAIDIA SERIKALI YA TANZANIA KTK VITA DHIDI YA UJANGILI -UNDP

$
0
0
Mkuu wa shirika la mpango la Maendeleo la umoja wa Mataifa (UNDP )Hellen Clark ( wa pili kushoto) akizungumza na askari wanaofanya kazi wa kupambana na majangili katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha baada ya kutembelea hifadhi hiyo juzi katika ziara yake ya siku mbili wa kwanza kushoto ni mkurugenzi mkuu wa TANAPA Bw Allan Kijazi
 ...............................................................................................................................
SHIRIKA la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) limesema  litaendelea kuisaidia serikali ya Tanzania katika vita dhidi ya ujangili pamoja na  kuhifadhi maliasili kwa ajili ya matumizi ya sasa na baadaye katika  hifadhi  

 Kauli  hiyo  imetolewa na mkuu wa UNDP duniani Bi Hellen Clark alipotembelea  hifadhi ya Taifa ya Ruaha na  kupongeza jitihada mbali mbali  zinazofanyika katika  hifadhi hiyo katika kukabiliana na majangili na usimamizi mzuri wa fedha  zinazotolewa na UNDP.

 UNDP kupitia mradi wa SPANEST ilitoa msaada wa Greda na magari matatu vyenye thamani ya zaidi ya Sh1.2 Bilioni, greda zaidi ya Sh570m na Land Cruser Pick Up Sh540m na kuwa gari moja litolewa kwa ajili ya hifadhi ya kitulo na mawili Ruaha mapema mwaka huu.

Bi Clark aliyasema  hayo  juzi wakati akizungumza na wanahabari mara  baada ya kutembelea hifadhi Taifa ya Ruaha Iringa pamoja na  maeneo mbali  mbali miundo mbinu yaliyoboreshwa  kupitia mradi  kuimarisha mtandao wa maeneo yaliyohifadhiwa Kusini mwa Tanzania (SPANEST) unaofadhiliwa na shirika hilo

Alisema  kuwa misaada hiyo inayotolewa na itakayoendelea  kutolewa  imelenga kuimarisha utendaji kazi wa watumishi katika kukabiliana na ujangili na uboreshaji  wa miundo mbinu katika hifadhi zetu .

"Mapambano dhidi ya ujangili yanahitaji mkakati wa pamoja kati ya Mashirika ya misaada, jamii, serikali na Mamlaka husika..... hivyo ni  UNDP litaendelea kusaidia zaidi ili kuendelea  kuhifadhi  zaidi maliasili kwa  faida ya baadae "

Alisema rasilimali zilizopo zinahitajika kulindwa kwa ajili ya matumizi ya vizazi vilivyopo na vijavyo hivyo inahitajika jitihada za makusudi kwa wadau wote wa maendeleo ndani ya nje ya nchi.

Aidha Bi Clark alisema ametembea katika hifadhi  hiyo na kuweza kujionea shughuli zinazofanywa na SPANEST hasa katika kuboresha utalii nyanda za juu kusini ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo kwa askari na watumishi wengine, kuboresha mawasialiano na  kujionea  jinsi  ambavyo mitambo iliyotolewa na UNDP inavyoendelea kufanya kazi vizuri  .

Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa (TANAPA), Bw Allan Kijazi alisema UNDP na mashirika mengine ya kimataifa yamekuwa msaada mkubwa katika mapambano dhidi ya ujangili na kuwa TANAPA wanathamini mchango huo na  kuwa  lengo la TANAPA ni  kuona  ujangili  unakomeshwa na utalii katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha  unazidi  kuboreshwa  zaidi  ili  kuvutia watalii wa ndani na wa nje .

Paul Harrison ambaye ni Mshauri wa wanyama wa UNDP alisema lengo la mradi huo ni kuboresha matumizi ya rasilimali na kukuza utalii katika eneo la nyanda za juu kusini kwa kuimalisha mifumo ya ulinzi, miundo mbinu na mawasiliano kwa watumishi wa hifadhi.

Alisema pia serikali inatakiwa kuwa na mkakati thabiti na kuchangia katika kuboresha utendaji wa watumishi ikiwemo kuwapatia malipo mazuri, vitendea kazi na mafunzo jambo litakalosaidia kupunguza vitendo vya ujangili kwa kiasi kikubwa.

Alisema eneo la ikolojia ya Ruaha ndilo lenye tembo wengi kwa sasa na inatakiwa wadau wa utalii waone kuwa tembo ni zaidi ya mnyama kwa kuwa anaweza kuboresha uchumi wao na Taifa.

Harrison alisema kinachofanyika ni kuwasiliana na wadau mbalimbali wa kimataifa na kusisitiza kutonunua bidhaa zitokanazo na meno ya tembo ili kusaidia kupunguza vitendo vya ujangili.

MKUU WA WILAYA YA KAHAMA AWAPA WALIMU SIKU 90 KUHAKIKISHA WANAFUNZI WASIOJUA KUSOMA NA KUANDIKA WANAJUA.

$
0
0



Photo: HONGERA DC KAHAMA KWA KUWAPA SIKU 90 WALIMU  Napenda kutoa pongezi zangu za dhati kwa Mh Mpesya Mkuu wa wilaya ya kahama kwa kuwapa siku 90 walimu kuhakikisha watoto wanajua kusoma na kuandika hii nakupa big up sana bro lakini utaweza kusimamia kauli yako kwa walimu hawa wa siku hizi wanaokaa juu ya meza wakipiga story huku wengine wakiwa bussy na facebook katika smart 4ne zao nakutakia utekelezaji mwema
Na  Wiliam Bundala matukiodaima.com kanda ya Ziwa
Mkuu wa wilaya ya Kahama benson Mpesya ametoa siku 90 kwa walimu wa shule za msingi ambao wanafunzi wao hawajui kusoma na kuandika wajue vinginevyo anaweza kuwachukulia hatua kali za kisheria watakaopuuza agizo hilo.
Kauli hiyo ameitoa hivi karibuni katika kata ya Igwamanoni wakati akihitimisha wiki ya Elimu iliyofanyika katika halmashauri ya ushetu katika kata hiyo.

Mpesya amesema tatizo hilo la wanafunzi kumaliza darasa la saba bila kujua kusoma na kuandika ni kubwa wilayani Kahama.
Katika hitimisho hilo Mpesya ameshangazwa na wanafunzi wa sasa kumaliza miaka saba shuleni bila kujua kusoma na kuandika hali ambayo wakati wa miaka ya sabini yeye akiwa mwalimu wanafunzi walikuwa wakijua kusoma ndani ya siku 21.
Amesema ili kumaliza tatizo hilo walimu lazima wafanye kazi ya ziada pamoja na wazazi wao kuhakikisha swala la elimu kwa watoto wao ni la muhimu na baada ya siku alizotoa atapita kukagua kila shule kuhakikisha wanafunzi wote kuanzia darasa la kwanza hadi la nne wanajua kusoma na kuandika.
Akizungumzia Elimu ya sekondari hasa katika masomo ya sayansi, baiolojia, fizikia na kemia amewataka Elimu hiyo ianzie kwa wazazi wao kuelimisha watoto wao kuanzia darasa la kwanza hadi la saba hali ambayo itasaidia watoto wao wakifika elimu ya sekondari watakuwa na uelewa juu ya masomo hayo.
Kabla ya hapo mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Ushetu Isabela  Chilumba amesema pamoja na changamoto hizo Elimu katika shule za sekondari imepanda ambapo matokeo ya mwaka jana shule nyingi zimefanya vizuri.

KUTOKA TFF LEO ,MKUTANO WA RAIS, KLABU ZA VPL

$
0
0

                                               Rais wa TFF Jamal Malinzi
Mkutano wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na wenyeviti wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kupata maoni yao juu ya changamoto zilizojitokeza katika ligi hiyo umefanyika juzi (Mei 11 mwaka huu).

Klabu za VPL zilizohudhuria mkutano huo ni Azam, Coastal Union, JKT Ruvu, Mbeya City, Mgambo Shooting, Mtibwa Sugar, Polisi Morogoro, Ndanda FC, Ruvu Shooting, Stand United na Tanzania Prisons.

Simba na Yanga hazikuhudhuria mkutano huo, na wala klabu hizo hazikutoa udhuru wowote wa kutokuwepo.

Maazimio ya mkutano huo ni kuwa kwa misimu mitatu ijayo kuanzia msimu wa 2014/2015 klabu zimekubaliana ziruhusiwe kusajili wachezaji watano wa kigeni. Kamati ya Utendaji ya TFF itatoa uamuzi wa mwisho juu ya suala hilo katika kikao chake kijacho.

Pia klabu hizo zimekubali timu zao za U20 kuanzia msimu ujao zicheze ligi ya mkondo mmoja. Hata hivyo, utekelezaji wa hilo utategemea na upatikanaji wa mdhamini wa ligi hiyo ambapo TFF inafanya jitihada za kumpata mdhamini huyo.

Vilevile Mwenyekiti wa Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake, Lina Kessy amezishauri klabu za VPL kuanzisha timu za wanawake, ambapo klabu hizo zimesema zitaufanyia kazi ushauri huo.

KIINGILIO MECHI YA TAIFA STARS 5,000/-
Kiingilio cha chini cha mechi ya kwanza ya raundi ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika 2015 nchini Morocco kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Zimbabwe (Mighty Warriors) itakayochezwa Jumapili (Mei 18 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 5,000.

Washabiki watakaolipa kiingilio hicho ni kwa wale watakaokaa kwenye viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani. Kwa upande wa VIP B na C kiingilio kitakuwa sh. 10,000 wakati kwa VIP A itakuwa ni sh. 20,000.

Tiketi zinatarajiwa kuanza kuuzwa siku moja kabla ya mechi hiyo katika vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam, na uwanja siku ya mchezo huo utakaoanza saa 10 kamili jioni.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ikiwa chini ya Kocha Mart Nooij inatarajia kurejea jijini Dar es Slaam kesho (Mei 14 mwaka huu) kutoka Mbeya kuendelea na maandalizi ya kuikabili Zimbabwe.

RAMBIRAMBI MSIBA WA MKUFUNZI KASINDE
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha Mkufunzi wa waamuzi nchini, Omari Kasinde kilichotokea jana (Mei 12 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.

Mbali ya kuwa Mkufunzi, Kasinde ambaye anazikwa leo (Mei 13 mwaka huu) mchana katika Makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam pia alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati iliyopita ya Waamuzi ya TFF iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Kapteni mstaafu Stanley Lugenge.

Msiba huo ni mkubwa katika fani ya mpira wa miguu nchini kwani, Kasinde enzi za uhai wake alitoa mchango mkubwa katika mchezo huu tangu akiwa mwamuzi na baadaye mkufunzi na kiongozi..

TFF tunatoa pole kwa familia ya marehemu Kasinde, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), na Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.

Bwana alitoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amina.


BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

RATIBA KUTOKA CECAFA HII HAPA

$
0
0



COUNCIL OF EAST AND CENTRAL AFRICA FOOTBALL ASSOCIATIONS
Affiliated to FIFA & CAF. Location: Nyayo stadium, Nairobi-Kenya

Date: Monday 12th May 2014

RE: CECAFA NILE BASIN CUP WINNERS CUP FIXTURE

Group   ‘A’
Group    ‘B’
Group   ‘C’
Group  ‘D’
El Merreikh 
El Merreikh Al Fasher 
Al Ahli Shandi 
Hey Al Arab 
Victoria University 
Mbeya City 
Al Masry 
Arab Contractors 
Malakia
Elman
Defence
Flambeau de l’Est  
Polisi 
AFC Leopards 
Dikhil 
Etincelles

No
Date
Fixture
Gp
Venue
Time
1.
Thr.22.05.14
Victoria University Vs Malakia
A
Khartoum
05:00 pm
2.
Thr.22.05.14
El Merreikh  Vs Polisi
A
Khartoum
08:00 pm
3.
Thr.22.05.14
Arab Cont. Vs Flambeau de l’Est  
D
P/Sudan
05:00 pm
4.
Thr.22.05.14
Hey Al Arab Vs Etincelles
D
P/Sudan
08:00 pm
5.
Fri. 23.05.14
AFC Leopards  Vs Elman
B
Khartoum
05:00 pm
6.
Fri. 23.05.14
El Merreikh Al Fasher Vs Mbeya
B
Khartoum
08:00 pm
7.
Fri. 23.05.14
Al Masry Vs Dikhil 
C
Shandi
05:00 pm
8.
Fri. 23.05.14
Al Ahli Shandi Vs Defence
C
Shandi
08:00 pm
9.
Sat.24.05.14
Polisi Vs  Victoria University
A
Khartoum
05:00 pm
10.
Sat.24.05.14
Malakia Vs El Merreikh 
A
Khartoum
08:00 pm
11.
Sat.24.05.14
Flambeau de l’Est  Vs Etincelles
D
P/Sudan
05:00 pm
12.
Sat.24.05.14
Arab Contractors Vs Hey Al Arab 
D
P/Sudan
08:00 pm
13.
Sun.25.05.14
Mbeya City Vs AFC Leopards 
B
Khartoum
05:00 pm
14.
Sun.25.05.14
Elman Vs El Merreikh Al Fasher 
B
Khartoum
08:00 pm
15.
Sun.25.05.14
Defence Vs Al Masry 
C
Shandi
05:00 pm
16.
Sun.25.05.14
Dikhil Vs Al Ahli Shandi 
C
Shandi
08:00 pm
17.
Mon.26.05.14
Polisi Vs Malakia
A
Khartoum
05:00 pm
18.
Mon.26.05.14
El Merreikh Vs Victoria University
A
Khartoum
08:00 pm
19.
Mon.26.05.14
Arab Contractors Vs Etincelles
D
P/Sudan
05:00 pm
20.
Mon.26.05.14
Hey Al Arab Vs Flambeau de l’Est  
D
P/Sudan
08:00 pm
21.
Tue.27.05.14
Elman Vs Mbeya City
B
Khartoum
05:00 pm
22.
Tue.27.05.14
El Merreikh Fasher  Vs  AFC Leopard
B
Khartoum
08:00 pm
23.
Tue.27.05.14
Dikhil Vs Defence
C
Shandi
05:00 pm
24.
Tue.27.05.14
Al Ahli Shandi  Vs Al Masry 
C
Shandi
08:00 pm

Wed.28.05.14
REST DAY





QUARTER FINALS



25.
Thr.29.05.14
B1 VS A2
-
TBD
TBD
26.
Thr.29.05.14
A1 VS B2
-
TBD
TBD
27.
Fri.30.05.14
D1 VS C2
-
TBD
TBD
28.
Fri.30.05.14
C1 VS D2
-
TBD
TBD

Sat.01.06.14
REST DAY

-
-


SEMI FINALS

-
-
29.
Sun.02.06.14
WINNER 25 VS WINNER 26

TBD
TBD
30.
Sun.02.06.14
WINNER 27 VS WINNER 28

TBD
TBD

Mon.03.06.14
REST DAY

-
-


FINALS & 3RD PLACE PLAY OFF

-
-
31.
Tue.04.06.14
LOSER 29 VS LOSER 30

TBD
TBD
32.
Tue.04.06.14
WINNER 29 VS WINNER 30

TBD
TBD

MRADI WA KILIMO ULIOGHARIMU ZAIDI YA MILIONI 300, WATELEKEZWA NA KUGEUKA MBUGA ZA WANYAMA KISHAPU

$
0
0

Naibu waziri wa kilimo chakula na ushirika Godfrey Zambi akikatisha kwenye kichaka eneo la mradi uliogeuka makazi ya nyoka huko Kishapu

 

Na William Bundala(KIJUKUU)

Matukio daima kanda ya ziwa


Wakulima wa mpunga 860 wa kijiji cha Itilima wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga wameshindwa kunufaika na mradi wa umwagiliaji uliojengwa kwa ajili ya kilimo cha mpunga, kutokana na kukosa chanzo cha maji ya uhakika na mradi kutelekezwa kugeuka kuwa sehemu ya kichaka cha wanyama huku milion 302 zilizotumika zikiteketea bila mafanikio.


Hali hiyo ilibainika hivi karibuni wakati wa ziara ya Naibu waziri wa kilimo chakula na ushirika Godfrey Zambi ,mara baada ya kutembelea eneo la mradi na kukutana na adha ya kukosa njia ya kuelekea mradi ulipo hivyo kulazimika kukatisha kwenye kichaka cha majani hali ambayo ilimpa wakati mgumu kutokana na mazingira yalivyokuwa.


Kutokana na hali hiyo,Naibu waziri alimuagiza mkuu wa wilaya hiyo Wilson Nkhambaku kuhakikisha eneo la mradi linafanyiwa usafi hata kama haufanyi kazi,huku akionyesha kusikitishwa jinsi fedha za walipa kodi zinavyoteketea kwa kuwekeza miradi ambayo haina tija kwa wananchi na viongozi waeneo husika wakishindwa kuisimamia.


“Hii hali inadhihirisha wazi hapa wataalamu hawatembelei miradi ,mnautelekeza mpaka eneo limekuwa msitu hivi kweli wilaya imeshindwa kusimamia mradi ukawa katika hali nzuri inaniuma sana,hapa mfano akitokea mfadhili aliyetoa fedha zake anaweza kutoa machozi jinsi hali ilivyo mbaya”alisema Zambi.


Naibu waziri Zambi aliwataka wataamu wa umwagiliaji kutoa ushauri mzuri kabla ya kujenga miradi hatua itakayosaidia kuokoa fedha za umma ambazo zimekuwa zikitumika vibaya kwa kujenga miradi isiyo na tija kwa wakulima hivyo kushindwa kufikia malengo yaliyokusudiwa na kuiacha kuwa vichaka licha ya kutumia fedha nyingi.


Akiwa wilayani humo alitembelea kijiji cha Nyenze ili kuona mradi wa umwagiliaji lakini hali ilikuwa tofauti baada ya kukuta eneo la hekta 450 lililotengwa hakuna shughuli iliyofanyika, hivyo kuishia kuangalia eneo la mbuga kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji huku wataalamu wakivutana baadhi wakipendekeza kujengwa bwawa na wengine mifereji ambapo fedha iliyotengwa ni million 298 kutoka TAMISEMI).


Awali mkuu wa wilaya hiyo Wilson Nkhambaku akitoa taarifa kwa Naibu waziri, alisema mradi huo ambao ulikamilika mwaka 2005 ,ulilenga kuwanufaisha wakulima lakini kutokana na mkondo wa mto Mumbu kuhama lengo limeshindwa kufikia ambapo shemu lililpjengwa banio kingo zake sio imara na ina mtelemko wa taratibu.


Naye mwenyekiti wa umoja wa watumiaji maji Dominic Philipo alisema kwa sasa wananchi wa kijiji hicho hawapati chakula cha kutosha kutokana nakushindwa kulima kilimo cha umwagiliaji na kuitaka serikali kuangalia uwezekano wa kuwasaidia ili waondokane na tatizo hilo,kwani awali mradi ulipokuwa unafanya kazi mazao yalistawi kwa kuwa na maji ya uhakika lakini sasa wamekwama kuendelea kulima na kusubili mvua za masika pekee.

Viewing all 2596 articles
Browse latest View live